Vifo 6 vya Bodaboda vinavyodaiwa kutokea kwenye Mashindano Arusha ni uzembe mkubwa sana, Waandaaji wanapaswa kuwajibishwa

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
4,011
10,666
Huwa nasema kila siku humu, CCM mtaji wao mkuu namba moja ni Ujinga wa hili taifa na pili na umasikini.

Bodaboda ni watu wanatumika kisiasa sana na kwa sababu ya kiwango chao cha juu cha ujinga walicho nacho hawajui kama wanatumika kiasiasa.

Kule Arusha jumapili kulikuwa na mashindano ya Pikipiki, na inaaminika Bodaboda 6 wamefariki kwwnye hayo mashindano hao ni kuacha walio Mount Meru Hospital kwa sasa wakiwa wamevunjika vunjika miguu.

Ila tukirudi kwenye Uhalisia je BODA BODA ZILE TOYO NI PIKIPIKI ZA MSHINDANO? hapa tu Africa kuna nchi hizi Toyo haziruhusiwi make hazina hata quality ya kubeba binadamu na kuwepo barabarani.

Kwa sababu sisi ni Taifa la wajinga tumezigezua kuwa ni mtaji wa kisiasa na ndio maana zinachinja watu daily.

Kama kuchinja watu barabarani hakutoshi sasa wakina Makonda wameamua kuzitumia kwenye mashindano ya pikipiki kutafuta mailage.

Ujinga na Umasikini vitaendelea kuwa mitaji ya wana CCM kwa muda mrefu sana

Kwenye utawala wa Sheria waandaaji wa hayo mashindano walipaswa kuwa ndani kwa sasa ila hilo haliwezekani Tanzania hii ya wajinga.

Chanzo: Nipashe
 

Attachments

  • Screenshot_20240716_181836_com.facebook.katana.jpg
    Screenshot_20240716_181836_com.facebook.katana.jpg
    714.7 KB · Views: 4
Waliokufa hawakufia uwanja wa mashindano na wala hawakuwa kwenye mashindano ni bodaboda washabiki waliofia barabarani kuonyesha mbwembwe barabarani wakienda kuona mashindano

Sio wahusika wa mashindano
Na Traffic wakikataza wakakaidi wakagongana bodaboda kwa bodaboda
Lema aache uongo
.kwenye mashindano kulikuwa na proffesinal watupu hakuna aliyekufa
 
Waliokufa hawakufia uwanja wa mashindano na wala hawakuwa kwenye mashindano ni bodaboda washabiki wakiofia barabarani kuonyesha mbwembwe barabarani wakienda kuona mashindano

Sio wahusika wa mashindano
Na Traffic wakikataza wakakaidi wakagongana bodaboda kwa bodaboda
Lema aache uongo
.kwenye mashindano kulikuwa na proffesinal watupu hakuna aliyekufa
Lengo wachafue tu hali ya hewa na Makonda aonekane mbaya!
 
Hata huyo RC wa Arusha hakutakiwa kabisa kuwa kapo, nchi hii thamani y uhai wa walalahoi ni kama thamani ya uhai wa paka shume tu. Yaani RC anakwenda kuzindua mashindano ya kihuni kabisa, hakuna standards zilizokuwa set before, ubora wa pikipiki, qualifications za madereva, utimamu wao, protective gears n.k. Na bado kuna wapumbavu wanasifu na kusujudu
Mashindano hayo yapo muda mrefu na Makonda kayakuta! Hao waliokufa hawakufia kwenye eneo la mashindano!
 
Back
Top Bottom