Boda boda waandamana Arusha.

Boda boda waandamana Arusha.

security guard

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
799
Reaction score
603
Vijana waendesha pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda mkoani Arusha wafanya maandamano ya Amani kuelekea katika ofisi za jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na kuomba kukutana na kiongozi wake ambapo walimueleza kero zao na changamoto wanazokabiliana nazo katika kazi zao hasa kero ya usumbufu na uonevu kutoka kwa Askari wa barabarani (trafic).

Kiongozi wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ndugu Robinson Meitinyiku amepokea maandamano hayo ofisini kwake na kuzungumza na vijana hao waendesha boda boda na kuwahakikishia kuwa suala lao atalitafutia ufumbuzi kwa haraka na wa kudumu.

Suala na bodaboda limeendelea kuwa gumzo nchini hasa katika miji mikubwa kama Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya, ambapo Vyombo vya usalama likiwemo jeshi la polisi mkoani Dar es salaam limepiga marufuku pikipiki kuingia maeneo ya katikati ya jiji kwa kile kilichodaiwa kupunguza matukio ya uharifu hasa wa kutumia bunduki za moto na kusababisha ajali za mara kwa mara baina ya magari na pikipiki hizo.

Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuwa kimbilio la Vijana wa kada mbalimbali hapa nchini, kuanzia wasomi, waajiriwa, na wale waliojiajiri pamoja na wasio na ajira rasmi na wasio na ajira kabisa. Tayari viongozi wa Chama wakiwemo wabunge mkoani Dar es salaam wanafuatilia kwa Umakini hatua za kiutaratibu ambazo zinatumiwa na jeshi la polisi katika kuendeleza operesheni zao bila kuathiri kipato na biashara ya boda boda nchini.

attachment.php
 
Attachments

  • BtNotCsIEAA-5ik.jpg
    BtNotCsIEAA-5ik.jpg
    26.3 KB · Views: 333
  • BtNoNMOIEAADzbb.jpg
    BtNoNMOIEAADzbb.jpg
    32.2 KB · Views: 1,012
huu unafiki wa ccm utaisha lini? serikali iliyopo ni ya ccm and then mnawadanganya wa tz ... ama kweli mtaji wa ccm ni ujinga wa watz
 
Tuwaache askari wa usalama wafanye kazi yao kama utaratibu unavyotaka. Mkoa wa Arusha ndio unaoongoza kwa madereva hasa wa bodaboda kuvunja shera za usalama barabarani. Hakuna dereva hata mmoja wa bodaboda anayesimama kwenye zebra au kwenye mataa. Hata kama taa inawaka nyekundu wao wanapita kibabe. Polisi fanyeni kazi.
 
Vijana waendesha pikipiki za abiria maarufu kama bodaboda mkoani Arusha wafanya maandamano ya Amani kuelekea katika ofisi za jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) na kuomba kukutana na kiongozi wake ambapo walimueleza kero zao na changamoto wanazokabiliana nazo katika kazi zao hasa kero ya usumbufu na uonevu kutoka kwa Askari wa barabarani (trafic).

Kiongozi wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ndugu Robinson Meitinyiku amepokea maandamano hayo ofisini kwake na kuzungumza na vijana hao waendesha boda boda na kuwahakikishia kuwa suala lao atalitafutia ufumbuzi kwa haraka na wa kudumu.

Suala na bodaboda limeendelea kuwa gumzo nchini hasa katika miji mikubwa kama Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya, ambapo Vyombo vya usalama likiwemo jeshi la polisi mkoani Dar es salaam limepiga marufuku pikipiki kuingia maeneo ya katikati ya jiji kwa kile kilichodaiwa kupunguza matukio ya uharifu hasa wa kutumia bunduki za moto na kusababisha ajali za mara kwa mara baina ya magari na pikipiki hizo.

Chama Cha Mapinduzi kimeendelea kuwa kimbilio la Vijana wa kada mbalimbali hapa nchini, kuanzia wasomi, waajiriwa, na wale waliojiajiri pamoja na wasio na ajira rasmi na wasio na ajira kabisa. Tayari viongozi wa Chama wakiwemo wabunge mkoani Dar es salaam wanafuatilia kwa Umakini hatua za kiutaratibu ambazo zinatumiwa na jeshi la polisi katika kuendeleza operesheni zao bila kuathiri kipato na biashara ya boda boda nchini.

Achani kukuza mambo hao vijana ni wamandamano sasa? wache kuchezea watu ccm Arusha ni kama haipo tena na hao vijana ni kati ya wale mnaowakodishaga kuja kwenye mikutano yenu
 
Tuwaache askari wa usalama wafanye kazi yao kama utaratibu unavyotaka. Mkoa wa Arusha ndio unaoongoza kwa madereva hasa wa bodaboda kuvunja shera za usalama barabarani. Hakuna dereva hata mmoja wa bodaboda anayesimama kwenye zebra au kwenye mataa. Hata kama taa inawaka nyekundu wao wanapita kibabe. Polisi fanyeni kazi.

nakuunga mkono
 
Natamani bodaboda Arusha wapigwe marufuku mjini...Ni kerooooo....Wengi ni wanywa viroba, wavutaji bangi na wasaga gomba....
 
Hawa hawa bodaboda ambao Lowassa na January wanasema bodaboda ni ajira kwa vijana au unamaanisha bodaboda wepi hao?
 
huu unafiki wa ccm utaisha lini? serikali iliyopo ni ya ccm and then mnawadanganya wa tz ... ama kweli mtaji wa ccm ni ujinga wa watz
HAHA HAHA HAHA! hivi hawa vijana na makada wa CCM hawajui kuwa kuna watu wako mtaani ambao ni mavetarani wa CCM au walioachana na CCM wanayoijua CCM ? hizi mbinu tulishapiga sana ! hizi za kujitekenya na ujicheke mwenyewe! mblaaa
 
Kuna wanasiasa hadi ifike 2015 watakuwa wamefirisika.
 
Haysee arifu hao machalii ni noma. Jamaa wamepiga gomba asubuhi.
 
Back
Top Bottom