Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,354
Mshambuliaji wa AC Milan, Kevin-Prince Boateng ameomba rasmi kurejea katika kikosi cha timu ya taifa ya Ghana.
Chama cha Soka cha Ghana kilithibitisha kupokea ombi la maandishi la mchezaji huyo ambaye alitangaza kustaafu kuichezea timu hiyo Novemba 2011.
Taarifa hiyo ina maana kuwa Boateng ataweza kuichezea Ghana katika mchezo ujao wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Zambia utakaochezwa mwezi ujao.
Boateng alikuwa katika kikosi cha Ghana kilichocheza Kombe la Dunia 2010 nchini Afrika Kusini, ameiwakilisha nchi yake katika mechi tisa na kufunga goli moja.
Chanzo; https://www.facebook.com/scoreboard1?ref=hl