B'moyo wajipanga kukusanya Sh22 bil

B'moyo wajipanga kukusanya Sh22 bil

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,073
Reaction score
34,844
HALMASHAURI ya Wilaya ya Bagamoyo, mkoani Pwani, inatarajia kukusanya zaidi ya Sh22 bilioni kutoka katika vyanzo vyake mbalimbali vya mapato, katika mwaka ujao wa fedha.

Fedha hizo ndizo zitakazoiwezesha halmashauri hiyo, kugharimia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika mwaka wa fedha wa 2010/2011.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kikao cha bajeti jana, Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wa wilaya hiyo, Samweli Salianga, alisema fedha kwa ajili ya utekelezaji wa bajeti, zitatokana na vyanzo mbalimbali.

Salianga alisema katika kipindi cha mwaka ujao, halmashauri inatarajia kukusanya Sh 1,169,396,997 kutoka katika vyanzo vyake vya ndani na kiasi kingine cha Sh 14,911,886,229, kitatolewa serikali kuu, kama ruzuku.

Mkurugenzi huyo, alisema halmashauri pia inatarajia kukusanya Sh 3,812,850,077 kutoka kwa wadau wengine na wahisani, watakaosaidia utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika sekta za kijamii, miundo mbinu, elimu ya msingi na sekondari.

"Katika bajeti hiyo, halmashauri pia itapokea michango kutoka kwa wahisani na wadau mbalimbali, wanaotaka kuisaidia katika utekelezaji wa shughuli za kijamii na kiuchumi na hii itarahisisha utekelezaji wa miradi hii kwa haraka,"alisema Salianga

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya hiyo, Almasi Masukhuzi, aliwaasa watendaji wa idara mbalimbali kutumia vizuri fedha za miradi ya maendeleo.


Masukhuzi alisema fedha hizo lazima zitumike katikia kuleta maendeleo kwa wananchi na si vinginevyo.

Chanzo:
Gazeti la Mwananchi
 
Back
Top Bottom