Blog,Web au App.. Kipi zaidi?

Blog,Web au App.. Kipi zaidi?

bachelor sugu

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
2,689
Reaction score
3,651
Habari zenu wana JF mliomo humu, kwa heshima na adabu naombeni msaada katika kueleweshwa kuhusiana na mambo yafuatayo:

-Hivi kati ya Blog, website na application ni kipi chenye ushawishi mkubwa zaidi kwa wasomaji endapo vitakuwa na content sawa??

-Ni kipi hasa kina uwezo wa kubeba content nyingi zaidi kuliko kingine??
Nikihitaji kufanyia biashara ya matangazo kupitia mitandao ya matangazo kama Google AdSense na mingineyo ni kipi hasa kinaweza kuwa na return nzuri zaidi km vyote vitakuwa na content sawa??

-Je bei za hivyo vitu vitatu(3) yaani blog, website na application zipoje kiuhalisia kwa anayekutengenezea hasa hasa akiwa expert na sio mwanafunzi??

Baada ya kutengenezewa kuna process yoyote ya kufuata ili uwezo kuwa mmiliki halali na usiibiwe content zako na wajanja maana nimesikia mara nyingi kuhusu hiki kitu KUNUNUA DOMAIN but sijajua nini maana yake.

Je, baada ya kutengenezewa blog, web au app nitasaidiwa kufeed na content za information ninazotaka kupost au nafundishwa namna ya kufeed mwenyewe??

Mwisho ningependa kupewa tahadhari yoyote kuhusiana na blog, web au app nitakayokuwa nimetengenezewa ili nisilizwe pindi ambapo itakuwa na mvuto hivyo kupata viewers wengi.

Tafadhali naombeni msaada kwa maswali niliyouliza na pia kama kuna nyongeza kwa kile ambacho sijauliza basi mwenye kujua namkaribisha.

Ahsanteni.
 
Ni vizuri Ukawa na website pamoja na app, Kama Hutaweza kuvimudu vyote unaweza kuanza na Website halafu baadae ukijiweza ukatengeneza app.

Kama utatengeneza website kupitia CMS ya wordpress ni nzuri kwakuwa ina feature nyingi ambazo huwezi kuzipata kwenye Blogger,

Pia Upatikanaji wake wa Template/plugin ni rahisi na nzuri kuliko za Bloger napia uwekaji wake matangazo ni mzuri tofauti na Blogger.

Ugumu unakuja kuwa website itakubidi ulipie Hosting+Domain kitu ambacho kinawafanya wengi kukimbilia kwenye blogger ambako kule hawalipii lakini kuna limit kwani domain lazima utumie jinalako.blogspot.com tofaut na website ambayo ni jinalako.com japo kwenye blogger unaweza ukatumia jinalako.com
 
Ni vizuri Ukawa na website pamoja na app, Kama Hutaweza kuvimudu vyote unaweza kuanza na Website halafu baadae ukijiweza ukatengeneza app
Thanxs very much brother nadhani safari yangu ya kujifunza inaanzia kwako maana wadau wenye utaalamu wameususa Uzi wangu licha ya kwamba mafundisho yangetufaa wengi so nadhani mahitaji msaada wako na kamwe usichoke na maswali yangu coz sina utaalamu wowote katika maswala haya.
 
Je gharama hizo za kutengenezewa Website,kulipia hosting na Domain zina range ktk kiasi gani?
 
Gharama ya Domain godady.com kwa mara ya kwanza unapata mpaka kwa $1.99/year na hosting pia zipo wanatoa gharama ndogo na kubwa ila nimeona pia godady wanatoa kwa $1.00/month ambayo ina 100gb storage ila kwenye kurenew nazani inakuwa zaidi ya hiyo. Kwa mimi natumia Hostinger bei zao nikubwa ila wana huduma nzuri (support) bei zao ni kuanzia $2.15/month. Hivyo jumla hapo unatakiwa walau usikose 80,000 Kwa kuanzia.
 
PAWAHOST.COM sasa inatoa offa kabambe kwa huduma mbalimbali,Kama ilivyoorozeshwa hapo chini:-
1. Utengenezaji wa Website kwa gharama kuanzia 150,000/=
2. Utengenezaji wa mifumo mbalimbali kama ya Kibiashara ,shule ,Hospitali 250,000/=
3. Utengenezaji wa Application Mbalimbali zinazoweza kuanzia 75,000/=
4. Utengenezaji wa forums na chatting websites 250,000/=
5. Website Kwa Ajili ya Kuuza Vitu Mbalimbali Online(Kama Amazon)=350,000/=

Pia tunatoa huduma ya Domain Reseller na Hosting kwa package zifuatazo:-
1 GB Disk Space
20GB Bandwidth
UNLIMITED Email Accounts
Free Data Backup
Free SSL Configuration per domain

Kwa package hizo hapa juu gharama ni 60,000 Tu kwa Mwaka,Tupigie sasa kwa namba +255687 535650 ,Email :info@pawahost.com ,Website :www.pawahost.com
 
Ku design Website inategemea na mtakavyoelewana na atakayekutengenezea. Ila kwa website za habari inaanzia 50,000- 300,000 au zaidi kutokana na mahitaji yako.
 
Gharama ya Domain godady.com kwa mara ya kwanza unapata mpaka kwa $1.99/year na hosting pia zipo wanatoa gharama ndogo na kubwa ila nimeona pia godady wanatoa kwa $1.00/month ambayo ina 100gb storage ila kwenye kurenew nazani inakuwa zaidi ya hiyo. Kwa mimi natumia Hostinger bei zao nikubwa ila wana huduma nzuri (support) bei zao ni kuanzia $2.15/month. Hivyo jumla hapo unatakiwa walau usikose 80,000 Kwa kuanzia.
Ni hiyo ya goddady ni promo tu mwaka unaofuata utalipa zaidi ya dollar 15 ,na hata support yake utakesha endapo litatokea tatizo.
 
Mimi Nilinunua Domain godady ina miaka miwili nilirenew kwa $13, Mwanzo huwa wanakupa discount kubwa ila wakati wa kurenew unalipia gharama halisi.
 
PAWAHOST.COM sasa inatoa offa kabambe kwa huduma mbalimbali,Kama ilivyoorozeshwa hapo chini:-
1. Utengenezaji wa Website kwa gharama kuanzia 150,000/=
2. Utengenezaji wa mifumo mbalimbali kama ya Kibiashara ,shule ,Hospitali 250,000/=
3. Utengenezaji wa Application Mbalimbali zinazoweza kuanzia 75,000/=
4. Utengenezaji wa forums na chatting websites 250,000/=
5. Website Kwa Ajili ya Kuuza Vitu Mbalimbali Online(Kama Amazon)=350,000/=

Pia tunatoa huduma ya Domain Reseller na Hosting kwa package zifuatazo:-
1 GB Disk Space
20GB Bandwidth
UNLIMITED Email Accounts
Free Data Backup
Free SSL Configuration per domain

Kwa package hizo hapa juu gharama ni 60,000 Tu kwa Mwaka,Tupigie sasa kwa namba +255687 535650 ,Email :info@pawahost.com ,Website :www.pawahost.com
Mfano nikihitaji kutengenezewa hiyo website je ni huduma gani zaidi napatiwa?
 
Gharama ya Domain godady.com kwa mara ya kwanza unapata mpaka kwa $1.99/year na hosting pia zipo wanatoa gharama ndogo na kubwa ila nimeona pia godady wanatoa kwa $1.00/month ambayo ina 100gb storage ila kwenye kurenew nazani inakuwa zaidi ya hiyo. Kwa mimi natumia Hostinger bei zao nikubwa ila wana huduma nzuri (support) bei zao ni kuanzia $2.15/month. Hivyo jumla hapo unatakiwa walau usikose 80,000 Kwa kuanzia.
Mh yaani kweli elimu mali maana hapa mida mingi natoka kapa sijui Domain ni nn,hosting naweza kisia kuwa ni umiliki but kwa kuwa nipo na nyie ndugu zangu wataalamu nitaelewa tu.
 
Kuna kitu kinaitwa E- Newsletter. Huwa natamani nitengeneze na kuifanyia biashara katoka matangazo. Je mnatengeneza? Nayo inafaa kibiashara??
 
E- Newsletter Unamaanisha Bulk-Email? Kama ndo hiyo ni nzuri na inafaa kibiashara. Kampuni maarufu zinazotoa hiyo huduma nikama Mailchimp,Mailerlite,Drip na nyingine zipo nyingi inategmea na feature unazokuwa unahitaji
 
Kwa upande wangu kulingana na uzoefu katika career hii inategemea na mahitaji yako, kwa kibongobongo unaweza kuanza na blog, kwa maana ni nzuri kuanza kwa mtaji mdogo. Kwa upande wa website unaweza kuanza endapouuna mtaji wa kutosha kuanzia.

- App inapendeza zaidi ikiambatana na website au blog ili kuweza kufikia audience tofauti tofauti katika platform na mazingira tofauti pia, hii wengi wanatengeneza baada ya blog/site yako kupata jina na watumiaji (kwa maana ikishaanza kua biashara serious)
 
Shukrani sana kwa ushauri nzuri pia,hata mm nililiona hili nikawa za bora kuanza na blog ambayo gharama zake kidogo zipo chini as long bado hujakuwa na uhakika wa namna utakavyopata audience wa kutosha na namna watakavyokubali kazi yako hapo ndipo unaweza kutanua mbawa zaidi.
 
Karibu mkuu,
 
Back
Top Bottom