The Fixer
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 1,365
- 599
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Blandina Nyoni, ambaye amesimamishwa kupisha tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi yake, ameibuliwa kashfa mpya ya kuhamisha mashine na kuzipeleka katika hospitali binafsi.
Tuhuma hizo ziliibuliwa juzi bungeni na mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Tabora, Magdalena Sakaya (CUF), wakati akiuliza swali la nyongeza.
Sakaya alitaka kujua kama mashine hizo za kisasa za kusafisha figo zilizoletwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na kisha kuhamishwa kinyemela na kupelekwa katika hospitali binafsi ya Agha Khan zimerejeshwa.
Mheshimiwa Spika ziko taarifa za kuaminika kuwa katika hospitali ya Muhimbili zililetwa mashine za kusafisha figo-
lakini aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Blandina Nyoni, kwa kushirikiana na daktari mmoja wa figo pale Muhimbili, walizihamishia hospitali binafsi, serikali inasemaje? alihoji.
Hata hivyo, Spika Anna Makinda alimtaka Sakaya aitaje hospitali hiyo binafsi, ndipo akasema ni Agha Khan na kusisitiza kuwa serikali inafahamu lakini imekaa kimya.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Afya, Dk Seif Rashid, alimshauri mbunge awasilishe suala hilo kwa utaratibu wa swali jipya ili liweze kupatiwa majibu sahihi.
Alisema ni vigumu kwake kuzungumzia suala hilo wakati hana taarifa kamili.
Februari 9 mwaka 2012, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliwasimamisha kazi Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Blandina Nyoni pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali, Dk Deo Mtasiwa baada ya kuonekana kuwa walikuwa chanzo cha mgogoro wa madaktari uliotikisa nchi mwaka jana.
Awali katika swali lake la msingi, Sakaya alitaka kufahamu ni wagonjwa wangapi waliopoteza maisha kutokana na mgomo wa madaktari na wale waliousababisha walichukuliwa hatua gani. Dk. Seif katika majibu yake alisema hakukuwa na ongezeko la vifo vilivyohusishwa moja kwa moja na mgono huo kwa mujibu wa hospitali nyingi.
Alisema kuwa madaktari waliosababisha mgomo huo walichukuliwa hatua kadhaa ikiwa ni pamoja ya kushitakiwa mbele ya Baraza la Madaktari na kutakiwa kujieleza.
Naibu Waziri alifafanua kuwa madaktari waliofutiwa mashitaka kutokana na kukosekana kwa ushhidi ni 49, walipewa onyo 213, onyo kali 66, waliosimamishwa kati ya mwezi mmoja hadi sita ni 30, walioahirishiwa mashtaka wanne na ambao hawakufika mbele ya baraza kujibu mashtaka 22.
Taarifa ya Bungeni-
via TanzaniaDaima
Source : Wavuti
The Fixer,
Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums