Blandes apata mpinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Blandes apata mpinzani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mutekanga, Feb 10, 2010.

 1. M

  Mutekanga Member

  #1
  Feb 10, 2010
  Joined: Aug 26, 2007
  Messages: 34
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbunge wa Karagwe, Mheshimiwa G Blandes, amepata mpinzani katika kugombea kiti cha Karagwe. Mpinzani wake ambaye ni Mweka Hazina wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani Karagwe, Karim Amil.

  Karim Amil, ni mtoto wa Marehemu Amri Amil, ambaye alikuwa rafiki mkubwa wa Mheshimiwa Blandes. Uchaguzi wa 2005, magari ya ya Marehemu Amri, yalitumika kumfanyia kampini Mheshimiwa Blandes. Kijana Karim, ndiye alikuwa kiongozi wa msafara katika kampeni za Mheshimiwa Blandes.

  Swali la kujiuliza ni kwanini Karim, ameamua kumgeuka Blandes? Majibu ni mengi! Je Karim, anaweza? Kisomo chake ni mashaka! Lakini pia ile ali yake ya kuwa na asili ya Uarabuni, inaweza kumletea shida.

  Hata hivyo kuna watu wengine, kupitia chama Cha Mapinduzi, wanaojiandaa kupambana na Blandes. Bwana Karugaba, mstaafu wa shirika la reli naye ana mpango wa kugombea. Amejaribu mara nyingi bila ya mafanikio. Profesa Innocent Ngalinda, naye ameonyesha nia ya kugombea.

  Chadema, inajipanga pia kuweka mgombea. Kwa ufupi ni kwamba Mheshimiwa Blandes, ana wakati mgumu sana katika jimbo la Karagwe. Inasemekana 2005, alisaidiwa na Sir G Kahama. Je atamsaidia na mwaka huu? Kuna habari kwamba Sir G Kahama, bado anataka kiti hicho kiwe cha familia. Eti, anamshawishi mke wake agombee, akikataa basi mtoto wake anayeifahmu Karagwe, kwenye ramani, atagombea. Jeuri yafedha itafanya kazi hata kama Mtoto wake hafahamiki vizuri kule Karagwe, kutokana na tabia ya Sir G Kahama, kutopenda kuileta familia yake Karagwe.
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,434
  Likes Received: 2,089
  Trophy Points: 280
  Kama ni ndani ya chama sisi hatuwaangalii hao. Muhimu ni kutoka nje ya CCM kama hao chadema. Kuendekeza wagombea wa CCM ni another continuation and inbreeding of internal crazy politics.
   
 3. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,520
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  Wananchi wa Karagwe, kwa mtizamo wangu walifanya chaguo lisilo sahihi. Blandes amewaangusha sana wapiga kura wake kwa kuamua kukaa kimya bungeni. Sijawahi kumsikia akichangia hoja yoyote pamoja na kwamba ni msomi (Degree ya sheria ya UDSM). Repalcement ni muhimu!!!

  Tiba
   
 4. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Tangu hapo Mzee Kahama anataka kiti cha Ubunge Karagwe kibakie kwenye himaya yake. Mwaka 2005 hakuwa na mrithi ndani ya familia yake ndio maana alifanya juu chini kumfagilia Blandes akijua fika ni dhaifu badala ya Cyril Pesha. Alijua Blandes atavurunda tu ili baadae akirudishe kiti chake kundini hivyo sitashangaa kama mtoto wake mmojawapo atajiingiza katika kinyanganyiro.
   
 5. Monsignor

  Monsignor JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 523
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Swala la kisomo sidhani kama lina mantiki yeyote kwa wadanganyika. Kama Chitalilo samuel Mchele ni mbunge huyo burushi sidhani atashindwa. Pia habari ya asili yake nayo si neno kwani Rostam Aziz si ni mbunge na pia Rais wa nji hii by 'de facto?'
   
 6. Kamakabuzi

  Kamakabuzi JF-Expert Member

  #6
  Apr 12, 2010
  Joined: Dec 3, 2007
  Messages: 1,525
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wapinzani wa Blandes ni wengi sana. Kwa ujumla ni wananchi karibu wote wa Karagwe. Suala la Karim si elimu yake wala uasili wake, bali tabia yake ndiyo itamwangusha. Amewadhalilisha sana akina dada wengi! Ni mpenda starehe sana kiasi kwamba hawezi kuwawakilisha vyema wana Karagwe. Bado ana mambo ya ujana sana - hajatulia. Hana tofauti na Blandes - hatakuwa na muda na wananchi wake bali ujana na hasa katika vidosho. Yuko wapi yule msichana wa taasisi moja ya fedha - maskini alimdhalilisha hadi akasababisha mchumba wake kuji...... Wa Kragwe watakuwa wanajua kesi ile na mke wa fulani..... Poleni wana Karagwe, hamjapata mtu!
   
 7. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2010
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mtoto wa Sir. George anayetaka kugombea anaitwa Joseph Kahama na hivi ninavyoandika yuko bukoba tangu wiki iliyopita na anafanya ziara za mara ka mara huko na watu wameshaanza kumfahamu, anaifahamu karagwe vizuri
   
 8. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,616
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Kweli watu wameamua, kuna kijana mmoja amepata MBA yake ya ESAMI mwaka jana anaitwa Theogenes Babwanga naye nasikia anatarajia kuweka jna lake kuchuana na Blandes. Mambo moto kweli!
   
 9. m

  miner Member

  #9
  Apr 13, 2010
  Joined: Dec 14, 2009
  Messages: 76
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante Tiba, wale wanaodhani elimu ni kigezo wanakosea sana hata jimbo la jirani Ngara kuna Profesa mambo ndio haya wanachotakiwa kujua wapiga kura ni kupata kiongozi ili mradi ajue kusoma na kuandika kama lilivyo hitajio la Katiba na si digrii maana wenye digrii wameisaliti nchi hii vya kutosha.
   
 10. M

  Mpingo1 Member

  #10
  Apr 13, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 91
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kazi kwako Gosbert
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...