BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,789
- 288,009
wakati rasilimali zetu zikiendelea kuwatajirisha wageni na mafisadi. Ni kitu gani kinachochelewesha kuibadilisha mikataba ya uchimbaji wa madini ili iwe na maslahi kwa nchi yetu!? JK anaingia mwaka wa nne tangu aingie madarakani kuna ugumu upi wa kutekeleza ahadi zake za kuipitia upya mikataba ya madini? inahitaji miaka mingapi kufanya hivyo!?
Date::12/2/2008
Serikali yakiri udhaifu katika madini
Exuper Kachenje
Mwananchi
SERIKALI imekiri udhaifu katika kusimamia shughuli mbalimbali zinazohusu rasilimali ya madini, ambayo mchango wake katika Pato la Taifa bado ni mdogo.
Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alisema hayo jana wakati alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili iliyoandaliwa kujadili "Rasimu ya Sera ya Madini ya Mwaka 2008" na kufanyika katika Hoteli ya Blue Pearl Ubungo, Dar es Salaam.
Waziri Ngeleja alisema kuwa sekta ya madini imeendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uwezo mdogo wa kubaini gharama halisi za uwekezaji, utafutaji, uzalishaji na biashara ya madini.
"Sekta ya madini bado imeendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali, hususan uwezo mdogo wa serikali kusimamia shughuli za madini, kubaini gharama halisi za uwekezaji, utafutaji, uzalishaji, biashara ya madini, utunzaji wa mazingira na usalama migodini," alisema Ngeleja.
Alifafanua kuwa changamoto nyingine ni pamoja na mchango mdogo wa sekta hiyo katika Pato la Taifa ikilinganishwa na ukuaji wa sekta hiyo, madini mengi kuendelea kuuzwa nje ya nchi yakiwa ghafi, kasi ndogo ya kurekebisha na kuwaendeleza wachimbaji wadogo pamoja na kiwango kidogo cha kushirikiana na wadau wengine katika uchumi.
Aliongeza kuwa, katika kipindi cha mwaka 1997 hadi 2007 serikali ilichukua hatua mbalimbali za kukabiliana na changamoto hizo pamoja na kuimarisha sekta ya madini ikiwemo kuunda kamati mbalimbali za kuishauri serikali namna ya kuimarisha sekta hiyo ya madini.
Alibainisha kuwa, katika kipindi hicho kamati tano tofauti zimeundwa kwa malengo mbalimbali ikiwemo kutoa maoni kwa serikali, kupitia mikataba, kutekeleza na kutoa mapendekezo juu ya usimamizi wa sekta ya madini nchini kwa ujumla.
Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Waziri Ngeleja alisema kuwa, rasimu ya madini inayojadiliwa katika warsha hiyo inatarajiwa kukamilika na kuanza kufanya kazi katika sera na kisheria mwezi Aprili mwaka 2009.
Alisema kuwa, katika kipindi cha miaka kumi tangu sekta ya madini ilipoanza kushika kasi, serikali imejifunza mengi na kwamba zipo changamoto zisizokwepeka ili taifa lifaidike zaidi na madini.
Ngeleja alieleza kuwa, lengo la serikali ni kuhakikisha taifa na wawekezaji wote wanapata faida katika hali ya usawa kutokana na ukweli kwamba, ingawa rasilimali ni ya Tanzania, serikali haina uwezo wa vifaa kuwezesha kutekeleza miradi mikubwa ya madini aliyosema inahitaji mtaji mkubwa.
"'Win-win situation (mkakati wa kila mmoja kufaidika) tunaamini ndiyo nzuri. Tunaamini madini yanahitaji mtaji mkubwa. Tukifanikiwa manufaa yake ni mengi," alisema Njeleja akisisitiza zaidi.
Hata hivyo, alisema kati ya mwaka 1997 na 2007 mchango wa sekta ya madini umeongezeka, akiweka bayana kuwa uwekezaji ulikua kutoka dola za Kimarekani bilioni 1.3 hadi bilioni 2.5, mauzo ya nje yakiongezeka kutoka asilimia moja hadi 52 ya mauzo yote huku ajira ikipanda kutoka wafanyakazi 1,700 hadi 13,000 katika migodi mikubwa kwenye kipindi hicho.
Kamati zilizoundwa tangu mwaka 2002 ni pamoja na Kamati ya Kuchunguza Chanzo cha Migogoro baina ya Kampuni ya AFGEM (Tanzanite One) na wachimbaji wadogo Mererani iliyoundwa mwaka 2002, Kamati ya Kudurusu Sera ya Madini ya mwaka 1997 iliyoundwa mwaka 2004 na Kamati ya Kupitia Mikataba na Mfumo wa Kodi katika Sekta ya Madini ya mwaka 2006.
Nyingine ni pamoja na Kamati ya Majadiliano ya Mikataba baina ya serikali na kampuni za madini, ambayo matokeo ya majadiliano yake yamewezesha baadhi ya kampuni kukubali kuondoa unafuu wa ziada wa asilimia 15 ya gharama ambazo hazijakombolewa na kuanza kulipa tozo kwa halmashauri zinazozunguka migodi.
Kamati ya Rais ya Kuishauri Serikali Kuhusu Usimamizi wa Sekta ya Madini ya mwaka 2008 ndiyo kamati ya mwisho na ambayo ilichambua mapendekezo ya kamati zilizotangulia na kutoa mapendekezo mbalimbali.
Mapendekezo ya kamati hiyo ni pamoja na kufanya marekebisho ya Sera ya Sheria ya Madini, kurekebisha mfumo wa kodi, ushiriki wa serikali katika madini mkakati na kuimarisha usimamizi wa sekta hiyo ili iweze kuongeza mchango katika uchumi wa taifa.