Blackberry :Blackberry yafufuka kinamna nyingine.

article

Senior Member
Sep 10, 2016
183
344
1488016270438.jpg

Blackberry ni miongoni mwa kampuni ulimwenguni zinazoongoza katika ufumbuzi wa teknologia mbalimbali katika ulimwenguni wa mawasiliano wa kutumia simu za mkononi maarufu hivi sasa kama smatifoni .Toka kuanzishwa kwake 1984 imeshikilia uongozi wa soko la smatifoni kwa miaka kadhaa kabla ya kupitwa na Apple na na smatifoni zinazotumia mfumo wa "Android".kama vile Samsung,Sony, Huawei,Tecno na nyinginezo.

Baada ya kupata hasara kubwa ya kibiashara na kushuka kwa bei yake ya hisa kwa miaka kadhaa ya hivi karibuni,hali iliyochangiwa kwa kiasi kikubwa na kutofanya vizuri kwa smatifoni zake za "Blackberry 10" .Blackberry iliamua kufanya "restructuring" chini ya uongozi wa John Chen ili kurudisha heshima na sifa ya Blackberry kwenye soko la Smatifoni na wapenzi wake na baadhi ya hatua ilizozichukua hivi sasa zinemeanza kuzaa matunda.

Kutoa lesseni za kutengeza simu za Blackberry kwa Blackberry mobile chini ya TCL na Marah Putih , kuacha uzalishaji wa ndani wa smatifoni za Blackberry, kujikata kwenye "IoT" na kujikita zaidi kwenye "software" za kiulinzi ni miongoni mwa hatua zilizochukulia na na John Chen ili kuokoa Blackberry na kufilisika na sasa blackberry imekuwa ikilejea taratibu katika hatua yake ya mwanzo kwa umakini mkubwa.
1488016382933.jpg

Leo katika kuutangazia ulimwenguni kwamba blackberry smatifoni zitaendelea kuwepo na kutamba ulimwenguni, BlackBerry inazindua simu yake mpya ya Android inayojulikana kwa sasa kama "Blackberry mercury" huko Barcelona katika ufunguzi wa Mobile World Congress (MWC)(7pm CET) saa moja jioni kwa muda wa Ulaya ya kati.
1488016452583.jpg


Blackberry mercury inayotumia mfumo wa Android uliolindwa na software ya blackberry inayojulika kama Dteck inategemea kuirejeshea Blackberry heshima yake iloyopotea kwa kuwa ina vitu vingi vya kisasa vinavyokosekana kwenye smatifoni nyingi kwa mfano ina kibao bonye(keyboard) chenye kuhisi mguso,ina kibonye kwenye kibao bonye chenye uwezo wa kugundua harama za vidole kwa ajili ya usalama,ina kihisi taswira(image sensor) chenye uwezo mkubwa wa kukamata picha na video zenye ubora wa hali ya juu pia ina vitu vingine vizuri vingi ambavyo vinategemea kuwekwa wazi leo kwenye uzinduzi wa MWC baadae jioni huko Barcelona.
1488016472092.jpg

Kama wewe ni mpenzi wa blackberry naamini utaungana na mimi kuipongeza blackberry kwa mafanikio haya makubwa baada ya kutofanya vizuri kwa kipindi kilefu kwa kutuletea smatifoni yenye utofauti na kuturudisha enzi zetu za BBM na kuchati kwa kutomia kibao bonye,ili usipitwe na kitu kwenye uzinduzi huu unaweza kutazama matangazo ya moja kwa moja ya uzinduzi huu wa kipekee wa smatifoni kali ya Blackberry mercury kupitia hii linki.http://m.crackberry.com/bbmobilemwc2017

Nawasilisha kwenu,

Article.
 
Keyboards kwenye "latest Blackberries" kusema ni old school nakuwa napata shida kukuelewa Mkuu,kwa kuwa zipo " very smart and advanced ", nakushauri tumia blackberry passport, BlackBerry Passport silver edition au priv nategemea utanielewa ni ni ninachoongea.
 
Hapo kwenye phyisical kryboard ni Point ya muhimu sana. Simu nyingi zimepuuzia kuweka physical keyboard na huku kuna watumiaji wanahitaji. Natumaini atawashika wengi kwa sababu hiyo, na zingine...
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Bei bado haijatanganzwa lakini tunategemea itakuwa ni zaidi ya dola 900 za kimarekani kwa kuwa hii ni "high end blackberry device"
 
Nilikuwa naisubiri sana kwani sijawahi kufurahishwa na hizi smart phones zinazotamba sasa,BB wako vizuri mnoo!
 
Ila hata BlackBerry Porsche ilikuwa poa, nahisi ni ukanda huu Wa Africa mashariki, ndio hatupati simu kama Motorola Verizon, MANTRAC, Oppo, na nyingiezo.
 
Back
Top Bottom