Biometric voter registration kits

Biometric voter registration kits

sodoliki

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
2,593
Reaction score
2,019
Jamani, tunazungumza utumbo mno, toka January hadi disemba. Ushindi wa ccm unatoka na na Mtaji wa majina yaliyo kkwenye daftari la wapiga kura. Leo Kenya wameleta BMI kits 18000' ambazo zinatumia finger prints na macho ya Mtu. Tukifanikwa Hilo ushindi Ni wetu, kwa daftari la sasa anzeni Kulia kilio kabla ya2015.changia
 
Hapo umenena mkuu lakini utasikia tu wakuu wanatusemea mbofu kuwa hatuna fedha za kununulia hiyo kitu. Sio mbaya uchaguzi wa Kenya ukiisha tutaomba watuazime nasi tutumie... au imekaaje?
 
Hapo umenena mkuu lakini utasikia tu wakuu wanatusemea mbofu kuwa hatuna fedha za kununulia hiyo kitu. Sio mbaya uchaguzi wa Kenya ukiisha tutaomba watuazime nasi tutumie... au imekaaje?

Inabidi kuwaombe majirani kama tunaomba chumvi vile..
 
Hahahahahah Mpinga kristo anaandaliwa mazingira
 
Hapo umenena mkuu lakini utasikia tu wakuu wanatusemea mbofu kuwa hatuna fedha za kununulia hiyo kitu. Sio mbaya uchaguzi wa Kenya ukiisha tutaomba watuazime nasi tutumie... au imekaaje?

kweli mkuu omuregi. baada ya march watuazime tuanze kuvifanyia mazoezi kabisa. maana tukiwambia tununue kama nchi, watasema kuwa vina gharama kubwa sana ambayo ni bajeti yetu ya miaka mitano na mchakato wa manunuzi huichukua muda mrefu na sisi km nchi tumechelewa. tunawahaidi watz kuwa tutanunua bajeti ya 2014/2015.
 
biometric data kama finger prints au iris scan ni ngumu kufoji ingawa wataalamu wanaweza kufoji pia.
itasaidia sana katika uchaguzi kuwa na mshindi halali
changamoto bado kubwa kwani itahitaji wataalamu, vifaa,central data base itakayohifadhi hizo data
na pia usahihi wa data zitakazokusanywa kwani ni rahisi kuchanganya data za mtu na mtu ukapata wrong subject
inahitajika pia sheria itakayolinda biometric data kwani ni sensitive data hivo haki ya privacy lazime iheshimiwe na kulindwa sana.
pia ni garama kuweza kuimplement hasa vifaa vya ukusanyaji wake na uhifadhi ni garama kubwa
kwa hivo lazima bunge liazimie kwa kauli moja na wananchi tupige kelele fedha zitengwe.
sijaweza kutumia kiswahili sanifu lakini ujumbe ndio huo
 
Back
Top Bottom