"Binti Yatima Amerudi Analia....'' Ninawaza tu!

1954tanu

JF-Expert Member
Jul 19, 2013
1,038
487
Tangu wiki hii iianze mjadala mkubwa ni sakata la wanafunzi wa yudom wale wa Kozi Maalumu ya Stashahada ya Ualimu kutimuliwa. Mengi yamesemwa na mapya yameibuka.

Miye nawaza tu hivi. Binti mmoja yatima kutoka mkoani Arusha ni mmoja wa wanafunzi waliotimuliwa huko yudom. Ni binti yatima wa umri wa miaka 17; ana wadogo zake watatu. Amerejea nyumbani kwao Arusha akilia. Leo kaja kanisani kuabudu. Baada ya ibada kumalizika. Akapewa nafasi ya kusalimia kanisa na kushukuru. Akionekana kuwa ana majonzi, amekata tamaa. Macho yamevimba kwa kulia akaanza kwa kusema:

Ilipofika Jumapili tukavurushwa pale chooni. Palija askari kila kona, mimbwa mikubwa mikubwa na polisi. Nikatoka mbio na begi langu. Nilifika stendi ya basi nikiwa na sh.2500 tu. Nikaweka begi langu chini na kulikalia. Machozi yakinimwagika. Sikumbuki kama nililia kwa sauti au la. Na sijui nilikaa vile kwa muda gani. Baadaye nikiwa ningali nimeinama nikashutuka naguswa begani nilipoinuka nikakutana na kaka mmoja simjui. Akaniuliza shida ni nini. Nikamweleza. Akahuzunika sana. Akaniambia atanisaidia. Akasema inuka nifuate. Nikamfuata hadi nje ya stendi ya basi. Tukaelekea kwenye taxi mojawapo. Akanisaidia kupakia begi kwenye buti ya gari. Tukaondoka kwa gari ile. Huyo kaka ndiye alikuwa dereva wa hiyo taxi.

Tukafika nyumba moja ya kulala wageni. Akachukua begi langu hadi ndani humo. Akalipia chumba. Akaniacha hapo chumbani, akaahidi anakuja baada ya muda kuniletea chakula. Ilipotimia saa nne usiku akarudi mkononi akiwa na soda baridi ya kopo na mfuko mweusi wa plastiki ambao alinikabidhi. Ulikuwa na chakula aina ya chips, mayai na mishikaki. Akaniambia kula, kesho utaanza safari ya kurudi nyumbani. Nikamshukuru sana kwa wema wake.

Muda mfupi baadaye nikajisikia kuchoka kichwa kizito. Niliposhituka, nilikuwa nasikia maumivu makali ya kichwa. Pia sikuwa nimevaa nguo. Niko kitandani. Muda kidogo nikahisi kama nina maumivu pia sehemu za siri; maziwa nyangu nayo yana maumivu kwa mbali. Nilipoinuka nikabaini nimeingiliwa kimwili. Nilikuwa sijajua mwanaume kabla. Hapo nikaanza kulia tena. Baadaye nikajipa moyo, nitalia hadi muda gani.Nikainuka kwenda bafuni kuoga. Niliporudi toka bafuni ndipo nikagundua pale mezani palikuwa na sh.7000. Nikavaa nikachukua begi langu nikaondoka. Hapo nje pembeni ya nyumba ile pana kiduka kidogo. Nikanunua dawa za kutuliza maumivu na maji nikameza dawa.

Nilienda hadi stendi ya mabasi. Nikajaribu kupepesa macho huku na kule kwamba labda nitamwona yule kaka. Sikumwona. Nikajikalia hapo stendi. Mara wakaja wanafunzi wawili tuliofukuzwa pamoja pale chuo. Tukasalimiana na wakaanza kuniuliza kwamba nitaondoka na basi gani. Nikawajibu kwamba sijapata nauli na sijui kama nitapata. Nina sh.7500 tu. Mmoja akaniambia yeye ametumiwa nauli na wazazi wake; akaniongezea sh.10,000. Nikawaza moyoni mwangu, kama ningekuwa sijanunua dawa, maji na nauli ya bodaboda ningekuwa na sh.19,500.
Wenzangu wakanishauri kwamba nisibaki Dodoma, bora nipande basi nikashukie mbele kwa mbele nauli yangu inapoishia. Basi, tukaagana kila mmoja wetu akipanda basi kuelekea aendako.

Nikaingia kwenye basi. Safari ikaanza. Nilikaa seat moja na kaka mmoja anaweza kuwa na umri wa miaka 27 na 32 hivi. Muda wote yeye alikuwa ana chat kwenye simu yake. Muda ukawa unasonga mbele na basi limeshika mwendo. Baadaye akaniongelesha. Akaniuliza jina langu nimetoka wapi na naenda wapi. Nikamjibu maswali yake vizuri tu. Akaanza kunihoji mambo mengi kuhusiana na chuo. Kiwango cha elimu yangu, ufaulu wangu nikamjibu. Akasema, ungejua kwa ufaulu wa division two bora ungenda kidato cha tano tu. Akaniuliza kwa kunilaumu vile, ni kwa nini nilienda kusoma kozi hiyo. Ndipo nikamwelezea wasifu wangu. Akabadilika uso, akawa na uso wa huzuni. Akainamisha uso wake chini. Akabaki amenyaza kimya.

Akaniuliza akitaka kujua safari yangu ilikuwa kuelekea nyumbani. Nikamwambia nitashukia njiani. Akaniuliza unaenda salimia ndugu. Nikawaza nimjibu ndiyo. Nikawaza tu nimwambie ukweli. Nikasema nashukia njiani, pale nauli yangu inapokomea. Akaacha mdomo wazi.

Akaniongezea nauli ya kufika Arusha. Ndipo machozi yakani bubujika tena. Nikamshukuru huyo kaka. Nashukuru kwa maombi yenu nimerejea nyumbani. Ila kuna jambo linaniumiza moyo. Sina uhakika, Je! Nitakuwa nimenusurika kushika mimba? Ama kuambukizwa magonjwa. Inaniuma sana. Sitaki kupata lolote kati ya hayo. Bw.aniepushe! Na ikitokea nimepata ujauzito, mtoto huyo bila kujali jinsia nitamwita jina la ( ".....") mheshimiwa mkuu ili kuwa kumbukumbu ya dhahama iliyonipata.

Kanisa limeangua kilio na kuomboleza.

HAYA NI MAWAZO TU, NAJARIBU KUWAZA KWA SAUTI KUBWA KABISA
 
Huzuni sana
 
this is true

yamewakuta watoto wetu
vijana wetu
dada zetu na ndugu zetu
ama kwrli machozi na kilio chao BWANA MUNGU amekisikia
huyu mungu wa ccm sijuh kama ataishi milele maana maumivu ya waja wa ALLAH yamekuwa makubwa sana
 
Back
Top Bottom