Binti wa Miaka 10 Ajifungua


kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2009
Messages
3,073
Likes
23
Points
135
Age
42
kilimasera

kilimasera

JF-Expert Member
Joined Dec 2, 2009
3,073 23 135
Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10 wa nchini Hipsania amejifungua mtoto baada ya kufanya mapenzi na mtoto mwenzake.
Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka 10 amejifungua mtoto katika mji mmoja wa kusini mwa Hispania na mamlaka husika zinachunguza tukio hilo ili kuamua kama wamnyang'anye mtoto huyo au mwachie amlee.

Msichana huyo mwenye umri mdogo alijifungua mtoto mwenye uzito wa kilo 2.8 wiki iliyopita kwenye mji wa Jerez de la Frontera, alisema Bi. Micaela Navarro, ambaye ni wa waziri wa masuala ya jamii wa kitongoji cha Andalusia.

Bi. Navaro aliwaambia waandishi wa habari kuwa baba wa mtoto aliyezaliwa naye ni mtoto mwenye umri mdogo ambaye jina lake limewekwa kapuni.

Wizara ya Afya ilisema kuwa msichana huyo na mtoto wake wote wana afya njema.

Magazeti ya Hispania yalinukuliwa yakisema kuwa msichana huyo alikuwa ni raia wa Romania.

Gazeti la Diario de Jerez liliwanukuu madaktari wakisema kuwa mama wa mtoto huyo aliwaambia kuwa ni jambo la kawaida nchini Romania wasichana wenye umri mdogo kuzaa watoto.

Wataalamu wanaonya kuwa wasichana wenye umri mdogo wanapopata mimba huyatia maisha yao katika hatari kubwa.

Utafiti umeonyesha kuwa wasichana wenye umri chini ya miaka 16 wanapopata ujauzito wana uwezekano mkubwa wa kuzaa watoto njiti na watoto wao wachanga huenda wakafiri ndani ya mwaka mmoja.
 

Forum statistics

Threads 1,236,300
Members 475,050
Posts 29,253,370