Binti uliyeachana naye ukagundua ana Mimba yako

Imposibo_

JF-Expert Member
Feb 1, 2016
2,746
2,121
Wasalaam..
Rafiki angu alikuwa na uhusiano na Binti fulani wa Kingoni.. Wakiwa katika uhusiomano Binti alipata ujauzito baada ya mwezi kupita hakuona siku zake akamwambia mwanaume wake .. Mwanaume wake akamuuliza Binti utaweza kulea? Binti akajibu Hapana siwezi basi Mwanaume akamwambia sasa itabidi tuitoe Mwanamke akakubali Mwanaume akatafuta hela akampatia Binti ili akatoe.. Binti akaondoka alipokua anaishi kwa siku 4 siku ya 5 akarudi akasema ameshatoa ile Mimba.. Baada ya hapo uhusiano wao uliendelea ila haukua na hamasa kama Mwanzo baadae Binti akaanza kua mkorofi anamtukana jamaa bila mpangilio jamaa ikabidi amuache aendelee na maisha mengine ila yule binti akawa sitaki nataka haeleweki kila kukicha jamaa anatumiwa sms za matusi tu .. Yule Binti akamwambia Jamaa yule kua kapata Bwana mwingine ivo anaondoka mjini kabisa anaenda Singida.. Baada ya Muda jamaa akaona picha mwanamke yule kapiga yuko Ubungo anasafiri kwenda Iringa .. Kufika Iringa huko akawa anaendelea kumtukana yule Mwanaume aliyekua naye katika uhusiano.. Ila yule Mwanaume aka kaza kamba akaona uyu mtu tumeshaachana akawa anajitahidi kumpotezea.. Yule Binti wa Kingoni kaishi Singida kwa uyo Mwanaume wake Mpya kwa miezi 4 wakagombana wakaachana akarudi Mjini Bunju akakutana na mtu Barabarani mtu akamtomgoza akakubali.. Akamwambia wakaishi wote Binti akakubali.. ILIKUJA JULIKANA KWAMBA ILE MIMBA HAKUITOA ALIENDA SINGIDA NA MIMBA NA ALIPOKUTANA NA UYO MTU MWINGINE BUNJU ALIKUWA NA MIMBA NA UYO MTU ALIMPOKEA YULE BINTI BILA KUMUULIZA MIMBA NI YA NANI NA ILIKUAJE MPAKA AKAWA IVO..

Ivo basi akaanza maisha mengine mpaka akajifungua mtoto huku yule mwanaume akijua sio mwanae ila alijikabidhi jukumu la baba akampa mtoto majina yake yeye akambatiza kwa majina yake yeye na akaenda kutoa mahali kwao binti huku wazazi wake na ndugu zake (isipokua mama wa binti) wakijua yule mtoto sio wa Mwanaume yule..

Jamaa yangu akaja kupata habari kwa watu mbali mbali kwamba yule dem wako mbona ana mtoto ila anafanana wewe.. Jamaa yangu ni mtu wa kusikilizia vitu mara mbili sio mtu wa kukurupuka maneno yalivozidi kua mengi kila mtu aliyekua anafahamu ule uhusiano anamwambia fulani kazaa mtoto anafanana wewe ebu fuatilia usije ukawa una mtoto alafu anaishi mahali pasipo salama.. Ikabidi jamaa afanye jitihada za kumtafuta yule binti kupitia marafiki zake akapata mawasiliano akamtumia ujumbe wa salam na kuulizia kuhusu mtoto aliyemzaa.. Yule Binti wa Kingoni bila kusumbua alisema ndio ile mimba hakuitoa na mtoto ndio uyo na anayemlea anajua sio baba yake..

Jamaa angu akauliza majina gani umempa akasema majina ya mlezi .. Akataka kumuona mtoto ikabidi Yule binti wa Kingoni amwambie mama yake sasa kwamba yule mwenye mtoto kajitokeza na akamwambia yule mzazi mlezi kwamba Baba ake Mwanangu kajitokeza.. Ilizua Taflani sana katika uhusiano ya uyo binti wa Kingoni akawa anapigwa kila siku na mama mzazi wa binti aliongea na jamaa yangu akasikitika sana jinsi binti yake alivomtia aibu ila akahaidi kushughulikia suala ilo.. Binti ikabidi amuondoe yule mtoto pale kwa mzazi mlezi akamsafirisha kabisa bila ruhusa ya mzazi mwenzake ila mzazi (jamaa yangu) alimuona mtoto siku 1 akamuelewa tokea hapo hajamuona tena mtoto .. Binti naye akatoka katika ile nyumba akaja akawa anaishi na mama yake mkubwa Sinza ila wakati mwingine anaenda kwa mzazi (jamaa angu) anaishi huko kama week mbili anachezea dushe kama kawaida na ana wivu sana yule Binti kwa io akiona hata simu inapigwa kwa jamaa yangu anaanzisha ugomvi anaondoka anarudi kwa mama yake mkubwa .. Ni miezi 8 sasa hajarudi kule kwa mzazi mlezi..

Tatizo lililopo kwa uyu Binti ni kwamba hajui nini anataka..
Hataki kubadili majina ya mtoto
Anamtishia sana jamaa yangu kuhusu kumpoteza mtoto
Ana majigambo sana yasio na maana na jamaa yangu anampenda sana yule mtoto japo hakujua kama binti hakuitoa ile mimba ila alivoambiwa kuwa hakuitoa akapiga hesabu zake akaona ni kweli..

Tumshauri..
Jumapili njema..
 
Aisee taaabu kwelikweli..vipi vikao vya wazazi na wakwe wakikaa...suluhu inaweza kupatikana nadhani..ila jamaa ana haki kutetea damu yake
 
Aisee taaabu kwelikweli..vipi vikao vya wazazi na wakwe wakikaa...suluhu inaweza kupatikana nadhani..ila jamaa ana haki kutetea damu yake
Mama mzazi wa Binti alimwambia jamaa yangu (ambaye ndio mzazi) kwamba wakae waelewane kwanza kabla mambo mengine hayajaendelea ila binti ndio kama ivo leo + kesho - duble duble
 
Tabu ni alikataa kubeba majukumu ya mimba ya mtoto, akae chini na kumuomba mama mtoto msamaha haswa haswa na ende kutubu. Alikosea mwanzoni sana sana sanaaaa kutaka mtoto huyo afe kabla ya kuzaliwa.

Acha mwanamke afanye lolote, lazima aliumia sana sana alipoambiwa atoe mimba sababu ilimuonyesha mwanaume hampendi. Msimlaumu kabisaaaaaaa
 
Mama mzazi wa Binti alimwambia jamaa yangu (ambaye ndio mzazi) kwamba wakae waelewane kwanza kabla mambo mengine hayajaendelea ila binti ndio kama ivo leo + kesho - duble duble

sasa hakuna vita kati ya baba Og na baba feki..vipi kuhusu matunzo ya mtoto??
 
sasa hakuna vita kati ya baba Og na baba feki..vipi kuhusu matunzo ya mtoto??
Matunzo jamaa hajaanza kutoa maana wameonana mwezi February mwaka huu alafu mtoto kapelekwa pasipojulikana .. Jamaa yangu huwa anamuona uyo dem tu hamuoni mtoto matunzo kwa dem anampa pia na dem naye anafanya kazi pia kwa io ana jeuri fulani
 
Tabu ni alikataa kubeba majukumu ya mimba ya mtoto, akae chini na kumuomba mama mtoto msamaha haswa haswa na ende kutubu. Alikosea mwanzoni sana sana sanaaaa kutaka mtoto huyo afe kabla ya kuzaliwa.

Acha mwanamke afanye lolote, lazima aliumia sana sana alipoambiwa atoe mimba sababu ilimuonyesha mwanaume hampendi. Msimlaumu kabisaaaaaaa
Binti angesema ndio anataka kulea jamaa angeilea yeye alimsikiliza yule binti.. Na binti alikua na maisha ambayo hayaeleweki na kukataa kwamba hawezi lea ilikuwa ni sahihi kabisa ..
 
Nina asili ya ungonini, lakini mama yangu aliwahi kisema mabinti wa kingoni wana mdomo sana na hivyo kunishauri nisijeoa huko, ingawa naye mngoni. Ushauri akomae achukue mwanae.
 
Matunzo jamaa hajaanza kutoa maana wameonana mwezi February mwaka huu alafu mtoto kapelekwa pasipojulikana .. Jamaa yangu huwa anamuona uyo dem tu hamuoni mtoto matunzo kwa dem anampa pia na dem naye anafanya kazi pia kwa io ana jeuri fulani


Mkuu hata kutoa ushauri inashindikana kwa sababu ya huyo mwanamke pasua kichwa
 
Back
Top Bottom