Binti, tafakari kabla hujachukua uamuzi wa kuhamishia majeshi kwa boyfriend wako

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,599
6,669
Huu ndio UKWELI MCHUNGU

1. Kamwe usiishi na mwanaume ambaye hujaolewa naye, usiishi na 'boyfriend' wako kinyumba hata kama ni mchumba wako, utaonekana uko 'cheap' na ndoa unaweza ukaisikia kwenye bomba.

Labda kama mmeamua kuishi hivyo hivyo bila Ndoa halali inayotambulika serikalini au na dini zenu.

2. Usibebe mimba ya boyfriend wako. Siyo busara. Zuia kupata mimba kabla hajakuoa. Kumbuka kwamba kamwe huwezi kutumia ujauzito kama kigezo cha kumfanya akuoe. Wanaume wangapi wana watoto nje ya Ndoa?

3. Jitahidi kuzuia kutoa mimba, mmefanya, umepata mimba itunze kutoa mimba kunaweza kukakufanya uwe mgumba maisha.

4. Kamwe usiwatenge wazazi wako kwa sababu ya mwanaume, muda mwingine mapenzi hufanya watu waonekane wapumbavu. Usiruhusu mapenzi yatawale akili yako, penda kwa akili na sio kwa moyo.

5. Usifikirie kujiua kisa 'boyfriend' wako kakutosa, hana thamani hiyo, siyo mwanaume mzuri pekee katika dunia..

6. Usipoteze masomo yako kwa sababu mwanaume amekutaka umtembelee kwake.

Hii itakufanya uonekane uko 'cheap' pia na kumbuka kesho yako ni muhimu kuliko huyo 'boyfriend' wako mlikokutana ukubwani..

7. Usimwombe mwanaume akuoe, hustahili kufanya hivyo na wewe una thamani yako, usijiweke kuwa wa rahisi kiasi hicho..

8. Hakuna kitu mwanaume hapendi kama majibizano, kubaki kimya ni adhabu kubwa sana kwa mwanaume mkorofi. Niamini mimi katika hili.

9. Katika ndoa Usimchunguze mwanaume kama unampenda na unajua huwezi kumuacha. Mwanaume siku zote huhitaji nafasi na uhuru, hapendi kuingiliwa katika mambo yake, mnaweza mkapinga ila huo ndio ukweli toka enzi na enzi. Kama una uwezo wa kuachana naye mchunguze tu bila wasiwasi wowote.

10. 'Wavulana' hutizama mwili wa mwanamke na kumhitaji kwa ajili ya kuburudisha maungo yao, ila 'wanaume' hutizama hulka na tabia za mwanamke katika malezi, uvumilivu, usaidizi, ushauri wa maendeleo na amani ya moyo (piece of mind).
 
Hapo namba saba..... Wale ambao jua limeshazama lazima wakulazimishe tuu
Kddng...

Good msg though......
 
Hata uwapigie magoti watakuona wewe huna akili uliyeyaandika hadi hapo yatakapowakuta ndio wataanza kuhaha...

Yanaingilia sikio moja yanatikea la pili
 
11. Usigawe gawe nyapu hovyo hata Kama ni boyfriend wako. Kwan ladha ikizoeleka hukinaisha na mwisho wa siku atataka ladha nyingine mpya. Jitunze. Mbanie,we siyo kiburudisho Bali tunda la utamu!
 
Kwa hiyo mtafeli asee

Alaf hvi kwani ukioa nyapu ndo haikinai!!?, kwa wale wanao sema subir adi kuolewa/kuoa
 
Huu ndio UKWELI MCHUNGU

1. Kamwe usiishi na mwanaume ambaye hujaolewa naye, usiishi na 'boyfriend' wako kinyumba hata kama ni mchumba wako, utaonekana uko 'cheap' na ndoa unaweza ukaisikia kwenye bomba.

Labda kama mmeamua kuishi hivyo hivyo bila Ndoa halali inayotambulika serikalini au na dini zenu.

2. Usibebe mimba ya boyfriend wako. Siyo busara. Zuia kupata mimba kabla hajakuoa. Kumbuka kwamba kamwe huwezi kutumia ujauzito kama kigezo cha kumfanya akuoe. Wanaume wangapi wana watoto nje ya Ndoa?

3. Jitahidi kuzuia kutoa mimba, mmefanya, umepata mimba itunze kutoa mimba kunaweza kukakufanya uwe mgumba maisha.

4. Kamwe usiwatenge wazazi wako kwa sababu ya mwanaume, muda mwingine mapenzi hufanya watu waonekane wapumbavu. Usiruhusu mapenzi yatawale akili yako, penda kwa akili na sio kwa moyo.

5. Usifikirie kujiua kisa 'boyfriend' wako kakutosa, hana thamani hiyo, siyo mwanaume mzuri pekee katika dunia..

6. Usipoteze masomo yako kwa sababu mwanaume amekutaka umtembelee kwake.

Hii itakufanya uonekane uko 'cheap' pia na kumbuka kesho yako ni muhimu kuliko huyo 'boyfriend' wako mlikokutana ukubwani..

7. Usimwombe mwanaume akuoe, hustahili kufanya hivyo na wewe una thamani yako, usijiweke kuwa wa rahisi kiasi hicho..

8. Hakuna kitu mwanaume hapendi kama majibizano, kubaki kimya ni adhabu kubwa sana kwa mwanaume mkorofi. Niamini mimi katika hili.

9. Katika ndoa Usimchunguze mwanaume kama unampenda na unajua huwezi kumuacha. Mwanaume siku zote huhitaji nafasi na uhuru, hapendi kuingiliwa katika mambo yake, mnaweza mkapinga ila huo ndio ukweli toka enzi na enzi. Kama una uwezo wa kuachana naye mchunguze tu bila wasiwasi wowote.

10. 'Wavulana' hutizama mwili wa mwanamke na kumhitaji kwa ajili ya kuburudisha maungo yao, ila 'wanaume' hutizama hulka na tabia za mwanamke katika malezi, uvumilivu, usaidizi, ushauri wa maendeleo na amani ya moyo (piece of mind).
Dah! Hii kumbe inawahusu wavulana sio wanaume,ngoja nipite mbaaaliiii.
 
11. Usigawe gawe nyapu hovyo hata Kama ni boyfriend wako. Kwan ladha ikizoeleka hukinaisha na mwisho wa siku atataka ladha nyingine mpya. Jitunze. Mbanie,we siyo kiburudisho Bali tunda la utamu!
unaongelea dunia ya leo au dunia ya kina Kwame Nkuruma
 
Back
Top Bottom