Binti mfalme wa Japan kupoteza hadhi yake

nankumene

JF-Expert Member
Nov 12, 2015
7,340
8,127
Binti mfalme wa Japan, Mako, mjukuu wa Mfalme Akihito, atavuliwa hadhi hiyo maana ameamua kuolewa na mchumba ambaye hatoki katika familia ya kifalme

Mako mwenye umri wa miaka 25 ambaye ndiye binti mkubwa wa Mwanamfalme Akishino ataolewa na Kei Komura, ambaye pia ana umri wa miaka 25 na walisoma pamoja katika Chuo Kikuu.

Lakini ndoa hiyo ina madhara yake..

Kwa mujibu wa sheria za kifalme, jamaa wa kike wa familia ya kifalme hupoteza hadhi yao kama mmoja wa familia hiyo kama wataolewa na mtu asiyetoka kwenye familia ya kifalme.

Licha ya hayo, Mwanamfalme Akishino, na mkewe Kiko wametangaza kuwa na furaha na mipango ya ndoa ya binti yao. Binti mfalme Mako ni mjukuu wa kwanza kati ya wanne wa Mfalme Akihito na mkewe, Malkia Michiko, kuvikwa pete ya uchumba.

Familia ya kifalme ya Japan ndio yenye kizazi kirefu zaidi duniani, kilichoanza miaka 2,600 iliyopita.

Binti mfalme wa Japan kupoteza hadhi yake | Masuala ya Jamii | DW | 18.05.2017
 
Ningekuwa mimi nisingekuwa radhi kupoteza hadhi hiyo mahsusi kwa ajili ya mahaba...maana mapenzi hayatabiriki aisee...
pesa na hadhi havikidhi thamani ya penzi la kweli toka moyoni hata mimi ningekataa pia sasa uozeshwe jitu hulipendi
furaha ya maisha dunia ya sasa iliolaaniwa ni mapenzi tuu toka kwa pekee mnayependana
pesa na hadhi kamwe haviwezi kuleta furaha ya kudumu moyoni
 
Nimetoa mawazo yangu....
 
Ningekuwa mimi nisingekuwa radhi kupoteza hadhi hiyo mahsusi kwa ajili ya mahaba...maana mapenzi hayatabiriki aisee...
Mbona kuna hadhi ulipoteza (bikra) maana bado huja olewa ulipata hasara gani!!!
 
Hata kuku anaweza kuwa bikra kabla ya kutotoa,hapo nimeongelea hadhi ya uprincess...haya kwaheri!!
Ukiona hivyo mwenzako kunasehemu kaguswa kachanganyikiwa na kitu cha kumtoa hapo ni kifo ipo siku utaguswa alipo guswa nakuombea mungu uguswe hapo!!!!
 
Ukiona hivyo mwenzako kunasehemu kaguswa kachanganyikiwa na kitu cha kumtoa hapo ni kifo ipo siku utaguswa alipo guswa nakuombea mungu uguswe hapo!!!!
Amina...nilishawahi kuguswa kuliko alipoguswa.Sema mimi ni commoner sikupoteza hadhi ya uprincessa...
Nilijifunza ndio maana nasema mapenzi hayatabiriki.
 
Kwani familia za kifalme ziko ngapi jamani? Au ilitakiwa aolewe na ndugu yake ili aweze kubakia na hadhi yake ya kifalme
 
Amina...nilishawahi kuguswa kuliko alipoguswa.Sema mimi ni commoner sikupoteza hadhi ya uprincessa...
Nilijifunza ndio maana nasema mapenzi hayatabiriki.
Usiogope yana tabirika sana inawezekana macho yenu hayakugusana pia au yaligusana kiuwongo!!!
 
Hivi hizi falme na mila zake bado ziko hadi sasa mi nilidhani ni kwenye movies za Kikorea tu, kweli sehemu zingine za Afrika zimeshapiga hatua kubwa hata zaidi ya Ulaya na Asia.

Hata si wa kwanza kuna huyu, Edward III UK. "for the woman I love"
 
Kwani familia za kifalme ziko ngapi jamani? Au ilitakiwa aolewe na ndugu yake ili aweze kubakia na hadhi yake ya kifalme
Tatizo umetazama familia ya kifalme kwa mtazamo wa baba, mama, na watoto. Kuna kitu kinaitwa family tree; na pia kuna first cousin, second, third, fourth, etc. cousin. First cousin ni ndugu (kaka/dada) kwa baba/mama mdogo/mkubwa; wenzetu wanaita tu uncle/aunt. Second cousin unapanda ngazi mbili kwenye family tree halafu unashuka na tawi lingine level ya babu yako; hao ni second cousin wako.

Third cousin unapanda ngazi tatu juu halafu unashuka na matawi ya line nyingine; yaani wajukuu wa babu wa baba yako. Vivyo hivyo hivyo kwa fourth, fifth, sixth .... n.k. Utaona kadiri level inavyoongezeka ule ukaribu wa damu unapungua lakini bado hao wanatambulika kama familia ya kifalme kwa sababu at some point ni kizazi cha ufalme huo; sorry nazungumzia ufalme (monarchy) na sio mfalme (king/queen).

So, kwa mtirirko huo kuna ngazi fulani ni ruksa kuoana. Of course ukienda kwa utaratibu huo at some point sote tumetokana na watu wawili tu - Adam na Eve lakini tunaona na kuzaliana bila tatizo. Muhimu umbali wa damu uliokubaliwa uzingatiwe kabla ya kuoana.
 
Back
Top Bottom