Binti matata asababisha maamuzi magumu

Binti matata asababisha maamuzi magumu

malimi katoro

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2015
Posts
358
Reaction score
154
Habari zenu wanaJF,

Mwaka jana nilipokuwa JKT kwa mujibu wa sheria nilikutana na binti toka Iringa ambaye ni mhehe,kiufupi binti si mrembo kivile ila kilichonivutia kwake ni ule ukaribu alionesha kwangu kipindi chote cha mafunzo.Pia ni mcha mungu a.k.a mlokole kitu ambacho mi napenda sana.

Sikusita kumtamkia kuwa nampenda sana na hata kumuoa nilikuwa tayari,tofauti na matarajio yangu alinijbu kuwa ana mpenzi wake,kwa vile mi king'anganizi nilizidi kuchokoza fikra zake lakini alizidi kunibania eti ana jamaa mwingne na hawezi kuvua chupi yake kwa mtu mwingine.

Baada ya muda wa mafunzo ya JKT kuisha kila mtu alienda kwao ila niliendelea kumkumbusha ombi langu.

Siku moja ambayo sikutegemea kabisa nilipokea namba ya simu kwa namba mpya na jamaa kujitambulisha kuwa ni boyfriend wa binti ambaye mimi nilikuwa namtongoza,jamaa alikuwa msatarabu tu alinisihi nisimfuatilie yule binti,ok sikuwa na hiana nikaamua kumuacha na sikuwasiliana tena na yule binti.

Bada ya kutoka ajira binti yule alinipigia simu na kunijulisha kuwa kapangiwa mkoa fulani na hapo ilikuwa ni baada ya kutowasiliana naye kwa muda wa miezi mitatu,na tangu hapo alianza kunipigia simu na kuchati kwa kila namna,wakati mwingine ananipigia simu lakini anakuwa hana hata cha maana cha kunieleza.

Muda umeenda uvumilivu umemshinda imebidi aniambie kuwa eti ombi langu amelikubali na alikuwa akinipima uvumilivu na imani yangu sasa ameridhia kuolewa na mimi na anadai ananipenda sana.

Juzi kanitumia elfu 50,000/= eti ya vocha,sasa niko njia panda. Je, nifanye nini wadau?

Je, huyu mdada ananipenda kweli au ni maigizo tu?

Vipi kuhusu jamaa yake aliyenipigia simu na kunisihi nimwache na yeye(binti) ndio alimpa namba zangu anipigie?

Karibuni kwa ushauri!
 
hivi viroba mnavyokunywa usiku vinakuharibu sana akili hii hadithi mpekee Shigongo utauza sana.
 
Part 2 umeitungia hapahapa bigup lakini
 
Hii thread inanikumbusha mbali! nakumbuka kuna thread style ya hii jamaa ali comment utumbo na kupigwa life ban! kesho yakn asubuh nikapokea ujumbe mfupi wa mms kuwa jamaa aliyepigwa life ban amejinyonga!
 
INAENDELEA HAPA!,Bada ya kutoka ajira binti yule alinipigia cmu na kunijulisha kuwa kapangiwa mkoa fulani na hapo ilikuwa ni baada ya kutowasiliana naye kwa muda wa miezi mitatu,natangu hapo alianza kunipigia cmu na kuchati kwa kila namna,wakati mwingine ananipigia smu lakini anakuwa hana hata cha maana cha kunieleza,muda umeenda uvumilivu umemushinda imebidi aniambie kuwa eti ombi langu amelikubali na alikuwa akinipima uvumilivu na iman yangu sasa amerzia kuolewa na mimi na anadai ananpenda sana,juzi kanitumia elfu 50,000/= eti ya vocha,sasa niko njia panda,je nifanye nini wadau,na je huyu mdada ananipenda kweli au ni maigizo tu,na vpi kuhusu jamaa yake aliyenipigia smu na kunisih nimwache na yeye(binti) ndo alimpa namba zangu anipgie,karibuni kwa ushauri!


haya ndo matatizo ya kuwa na vivulana huku jf
 
Back
Top Bottom