Binti kaa mbali mita thousand hili goma la machizi nisijeonekana natafuta kiki

Igombe fisherman

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
2,027
3,565
Siku kadhaa hapo nyuma kuliletwa na uzi unaoongelea bikra. Uzi huo ulisema bikra ni kapu la ndoa. Uzi ule ulijadiliwa kwa mihemuko kwa kufuata jinsia kwa kila mmoja. mpaka uzi ule ulifika mbali kwa watu kutukanana na kuonana wabaya bila sababu za msingi. Ila nilipotazama mwanamke mmoja japo tulimzodoa sana ila hoja zake zilikuwa sawa endapo tutapima kwa fikra huru.

Wakati wanaume tukiwa tumesimamia kuwa bikra ni ule utando unaokuwa umeziba ndani ya uke wa mwanamke ila yeye alitaka bikra iwe kwenye mawazo na mtazamo na matendo ya mhusika. Yaani tusitumie ule utando kama kipimo pekee

Malengo ya ile mada ilikuwa ni kuwa mwanamke apasaye kuolewa ni yule tu atakayeonekana ana utando siku ya ndoa yenyewe. (Hajaingiza kitu chochote ndani ya uke) kinyume na hapo utakuwa hujaoa mwanamke anayetakiwa.

Sasa turudi nyuma kidogo.

Babu zetu walitumia bikra kama kipimo cha uvumilivu wa binti ila bikra kilikuwa ni mtihani wa mwisho sana kwa binti kuolewa.

Vitu walivyoangalia

1: Ushirikina. Walihakikisha familia ya binti haina historia hiyo

2: Magonjwa ya kulithi. Walihakikisha familia ya binti haina hilo tatizo

3: Maagano ya vifungo katika mfumo mzima wa maisha. Hapa nadhani ni mambo ya kiroho zaidi. Waliangalia ukoo huo wako vipi kiuchumi, upiga kazi. Maana kuna koo zingine ukoo mzima hakuna hata mtu anayemiliki aset ya milioni hata kumi tukilinganisha na pesa ambayo ndo kipimo cha mali kwa sasa. Ila kipindi kile walitumia mifugo na ardhi.

Sasa kwa misingi ya mada ile ilionyesha kuwa hayo yote niliyoyataja siyo ya kuangalia bali tuangalie bikra tu. Yaani ubomoe box la bidhaa siku ya kwanza ya fungate.

Hivyo basi kwa mwanamke yeyote ambaye itakuwa kinyume na hapo tukuhesabu hujaoa hata mtaani tukuzodoe we mwanaume kwa kujichanganya.

Sasa mi kuna maswali najiuliza endapo tutatumia bikra kama kipimio pekee cha ubora wa mwanamke sijui itakuwaje kwa watu wafuatao?

1: Wanawake waliojitunza na wakaolewa na bikra na zikatolewa na waume zao ila waume zao wakafa muda kidogo tu baada ya ndoa je nao wasiolewe maana watakuwa hawana tena tiket yakuolewa.

2: Katika uzi ule hakuna hata sehemu aliyosema mtoa mada wanaume tujitunze. Sasa swali: Endapa nitamwoa mwanamke bikra ila mimi nikawa kirukanjia kila malaya namjua uchi wake na wife akanifuma mara nyingi tu. Je, anatakiwa anisamehe bila kikomo ama aombe talaka? Maana hana tena tiketi ya kuolewa kwa misingi ya mada ile.

3: Kuna wasichana walitumia mlango wa uwani ili kulinda bikra zao mbele. Je, kwa misingi ya mtoa mada ile wanafaa kuolewa?

4: Kuna akinadada walijilinda sana tena sana ila wakaja fanyiwa ukatili kama kubakwa na wakapoteza bikra zao je nao wamepoteza tiketi ya kuolewa?

Katika mada ile hakuna mahara ambapo tumejipa jukumu wanaume kwa kulinda usichana wa wanawake ila huwa naona tunajisifia kwa kutoa bikra nyingi za wasichana.

Jamii yetu bado inachukulia kama mtoto wa kiume kufanya ngono ni urijari ila hatutaki kujua anafanya na akinanani.

Ili tuendelee kuwasifia wavulana kwa kubeba mademu basi tuondoe hii dhana ya kigezo cha kuolewa kiwe bikra
Ili wasichana wawe na bikra mpaka kuolewa basi itabidi wavulana waikose ile sifa ya urijali maana watakuwa wameshindwa kuwapata wasichana.

Na kama tunataka wavulana wetu wabaki na sifa yao ya urijali huku wasichana nao wakibaki na sifa yao ya kutunza bikra basi itabidi ku-share wanawake na watoto wetu wa kiume. Yaani kijana wako atembee na mwanamke mkubwa kama mke wako (mama yake) kwa kuwa wasichana wanatunza bikra zao na wamama ni wasichana wa zamani bikra zishatolewa na baba zao.

Wanawake wa humu katika mada ile walitaka tutumie matendo yao kama kipimo cha kuoa na si bikra. Maana matendo yanawakilisha fikra zake. Hivyo utakuwa umepata bikra wa fikra na si bikra wa papuchi.

Au munaonaje mabaharia kama siko sawa nikosolewe na siko upande mmoja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pia kuna imani kwamba kila mtu ana mwanamke wake aliyeumbwa aje amuoe, ubavu wake wa pili, je kama huyo ubavu wa pili alishakosea na bikra hana tena unafanyaje? Unaoa ubavu wa mtu mwingine? Je, nadharia ya mwanamke kuumbwa kwa ajili ya mwanaume husika ipo kweli?
 
Back
Top Bottom