Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,741
- 25,681
Kama mchumba wako anakuelekezea upotevuni kwa nini uendelee naye?
Kama mchumba wako anakupeleka mautini,kwa nini unakubali kufunga naye ndoa?
Kama mchumba wako anakuelekezea kuzimu,kwa nini bado unamng'ang'ania tu.?
Shtukaaa
Dada ulikuwa unaenda kanisani vizuri tu,lakini toka uwe na huyo mchumba wako,siku za ibada nyie ndio siku zenu za mtoko.Na walaa hushituki.
Dada ulikuwa mwana maombi mzuri tu,lakini toka umpate huyo mchumba muda wa maombi ndiyo muda wenu wa kuongea na simu na kupiga story zisizo na maana.Angalia usije ukashtuka uko kwenye ndoa tayari,utaumia.
Dada kabla ya kumpata huyo kijana mbona ulikuwa unafunga na kuomba sana tu,sasa iweje Leo anakwambia usifunge utapata vidonda vya tumbo halafu na wewe unakubali.Hushituki tu?
Dada mbona kabla ya kuwa na huyo kijana ulikuwa umezunguukwa na kanda za watumishi wa Mungu na vitabu vya watumishi wa Mungu na ilikuwa ndiyo maisha yako.Iweje Leo akuletee series/movie na kukufanya uwe unalala na kuamka nazo mpaka unasahau hata kula.Huwezi tena kusoma Biblia,huwezi tena kusoma vitabu.Muda wote unatamani uendelee kuangalia ulipoishia.Halafu unamsifia mchumba wako kwamba yeye ndiye amekufanya upende kuangalia series.
Shtuka dada angu
Dada huyo mchumba wako mbona kila mchungaji,nabii kwake ni wa uongo tu ina maana katika wooote hakuna wa kweli?Na wewe umekubali akakuingizia hofu umeacha hata na kusali eti unaogopa kisa amekwambia ana Mashaka na mchungaji wako kama ni wa kweli.Kila unapoenda anakwambia ni wa uongo.Umeacha hata Kumsikiliza Roho Mtakatifu siku hizi,umebaki kumsikiliza huyo mchumba wako tu.Angalia utaumia.
Dada mbona hauangalii Neno la Mungu siku hizi.Kila anachokwambia mchumba wako unakubali hata kama kinapingana na Neno la Mungu.Anakwambia kunywa pombe Mara moja moja kwenye sherehe si mbaya,na wewe unakubali.Halafu unamtetea kwa watu kuwa si mlevi anakunywaga kwenye sherehe tu.Dada angalia unapoelekea.
Dada mbona huyo mchumba wako anaingia kwenye ibada kachelewa halafu ibada ikiisha wa kwanza kutoka kama kafukuzwa.Dada mbona huyo mchumba wako hapendi ukimwambia habari za kanisani au msikitini
Wakati wa kumbadilisha ni sasa usidhani kwenye ndoa