Binamu Bananga aipa darasa CHADEMA

Binamu Bananga aipa darasa CHADEMA

Hivi yule jamaa aliyeongea kwa ubabe na jeuri akisema yaani mimi nikupe gari ya kutembelea,posho ya dereva na umtanganze mpinzani ni mbunge hiiiiiiii haiwezeni’ yuko wapi siku hizi?

Wakina kabudi waliwahi mpk kumuita ni. Mh mungu sijui yuko pande gani siku hizi.
Jamani mpendwa jalalani na kenda kimemsibu nini siku hizi
 
Anaweza akaongea sana maana siku hizi amekua mjinga mjinga tangu mkewe apate ule ubunge wa covid-19.
Jibu hoja sio kumshambulia Bananga.

Tatizo lenu hamtaki kuambiwa ukweli mnajiona MALAIKA amkosei.

Bananga yupo sahihi,jaribuni kuwa na AJENDA yenye kufikia TAMATI sio leo katiba mpya mara kesho mnarukia JAMBO lingine,mnatakiwa mnalolianzisha linapata RESULTS kabla kurukia AJENDA mpya.

Tokea nijue CHADEMA nimeona MOVEMENT For CHANGE, OPERASHENI SANGARA etc lakini pia mmebaki kwenda na MATUKIO hamna msimamo kama chama mwisho wa siku wafuasi wenu watakata tamaa watajua hamna MSIMAMO na pia VIONGOZI wenu MAKUNGURU(yaani kunguru hata ukiokota jiwe tu wanaruka na kukimbia).

Viongozi wapo TWITA wanachama wa kawaida wanaenda FRONT(kwenye maandamano).

Kwanini jana HECHE,MSIGWA,SUGU awakuwepo KISUTU?
 
I dont care wether uzi wa kweli au uongo, huyo Bananga kuwa na ushoga na kina Msando anaweza sema chochote, alipotafuta nafasi ya kugombea Arusha Mjini akashindwa na Lema kwa kukataliwa na wajumbe ndio hasira zake kwa Chadema zimezidi, ni mtu alietafuta maslahi Chadema kwasababu ameyakosa ana hasira na chama.
 
Jibu hoja sio kumshambulia Bananga.

Tatizo lenu hamtaki kuambiwa ukweli mnajiona MALAIKA amkosei.

Bananga yupo sahihi,jaribuni kuwa na AJENDA yenye kufikia TAMATI sio leo katiba mpya mara kesho mnarukia JAMBO lingine,mnatakiwa mnalolianzisha linapata RESULTS kabla kurukia AJENDA mpya.

Tokea nijue CHADEMA nimeona MOVEMENT For CHANGE, OPERASHENI SANGARA etc lakini pia mmebaki kwenda na MATUKIO hamna msimamo kama chama mwisho wa siku wafuasi wenu watakata tamaa watajua hamna MSIMAMO na pia VIONGOZI wenu MAKUNGURU(yaani kunguru hata ukiokota jiwe tu wanaruka na kukimbia).

Viongozi wapo TWITA wanachama wa kawaida wanaenda FRONT(kwenye maandamano).

Kwanini jana HECHE,MSIGWA,SUGU awakuwepo KISUTU?
Kwa sababu mungu wenu wa chato hayupo.
 
Bananga Mario endelea kubwabwaja kumfurahisha mkeo kovid19 ili uendelee kula.
 
Angalau wasioijua CHADEMA wanaanza kupata mwanga japo kwa mbali CHADEMA ni nini. Ni kundi la wahuni fulani waliobobea ambao wanatumia njia chafu lakini kwa siri ili watimize uroho wao wa madaraka na pesa. Sasa mkiambiwa ni nani anahusika na kupotea kwa Ben Saanane mtaanza kuelewa!

lakini kwa wenye akili sakata la Dr Slaa na Lowasa lilihitimisha ukweli kuhusu rangi halisi ya CHADEMA!
 
Kama uchaguzi uliopita CDM wangepewa nchi huyu mwamba angekuwa ndo waziri wa ulinzi,mpaka sasa angekuwa keshauza siri za nchi.
Kuna siri gani nchi hii ya kiusalama wakati miundombinu yote ya jeshi inajengwa na wachina, na mafunzo wanatoa hao wachina na US? Ama hujui siri ni nini?
 
Binamu Bananga ni Diwani wa zamani wa Sombetini Arusha kupitia CHADEMA.

1. Viongozi wa Kanda ya Pwani wameshindwa kushawishi Wanachama kujitokeza kwa wingi Mahakamani, ushawishi wa mitandaoni umeshindwa kufanya kazi, Wito aliotoa RPC umekuwa na nguvu, kwa maandalizi tuiliyofanya sijutegemea idadi ndogo ya watu kiasi kile pale Mahakamani, Kesi ya Mdude tuliweza kujaza Mahakama lakini hii ya mwenyekiti tumetia aibu.

2. Kwa upande wa mahojiano, aliyeandaa anastahili pongezi, tumefanikiwa, ingawaje tulilipa watu 20 wa kuhojiwa na 40 wa kubeba mabango lakini waliofika wakikuwa wachache, hakuna aliyefahamu kama walilipwa lakini kesho kuwe na value for money, wote watakaolipwa usiku huu, wafike, na tuboreshe mapungufu machache kwenye setup, tuhakikishe vyombo vyote vya habari vinakuwepo.

3. Mama tuliyempanga ajitambulishe kama Mama mlezi wa Mbowe, na kusema ametoka Hai, ni mama n'tilie pale Mkwajuni. Tunajua kabisa pale Mkwajuni ndio zilipo ofisi za CCM kinondoni lakini bado tukamtumia mtu wa maeneo yale, Aliyepanga hilo kama ni kiongozi awajibishwe. Amekiabisha chama.

4. Najua tulilenga kufikisha ujumbe, lakini kwanini tuliruhusu Mabango yaandikwe na mtu mmoja na uumbaji wa herufi kufanana? Tunapoteza credibility kwa Wananchi, na kwanini tupange watu sehemu moja, kwanini hatukufikiria kwamba haiwezekani watu 10 wenye mabango kujipanga mstari mmoja kama hawakupewa maelekezo. Naumiabkuonwa tunavyosemwa mitandaoni kwa kusgindwa kupanga vizuri.

5. Tunategemea matukio na propaganda kuliko kujenga Chama kwenye misingi, Tukiendelea na Siasa za aina hii Chama kitakufa, Tulikuwa na Wabunge wengi Dar 2015 - 20 lakini leo tumekosa hata Wananchi 200 wa kutuunga mkono pale Kisutu, hii wake up call kwetu, sidhani kama ACT wangekosa watu.

6. Mtaani imejengeka Taswira kwamba Viongozi walipanga kutoa kafara wanachama, walihamasisha kwenda wanachama waende Mahakani, halafu wao wakabaki majumbani kunywa juice bariid, mambo yote wamefuatilia Twita. Waliofika Mahakamani hawakuzidi watatu. Kesho viongozi tuwepo.

7. Chama kiwe na msimano thabiti, tulisema mwanachama wetu akikamatwa hatutasumbuka kumdhamini, lakini bado tumeshawishi wanachama kwenda mahakamani (ingaswaje wamegoma) na Kibatala amesikika pale akiahidi kuwatoa kwa dhamana Wanachama wale jamaa waliokamatwa baada ya kukaidi maagizo ya polisi. Tumesahau msimamo wetu?

8. Tukiendelea kuamini tutawashinda CCM kwa kushinda Twita, tutakufa tukiwa wapinzani, tujenge Chama Uraiani, confidence ya Wananchi mitandaoni isitudanganye, kwa ground mambo ni tofauti, Au kuna aliyewaona wale wanaotweet na kuretweet sana?

9. Bila Mbowe chama chetu hakina tofauti na kikundi cha watoto wa 'Sunday School', matamko yanaandikwa pale Triple 7 - Bar, yanatoka muda wowote hata usiku wa manane, mepesi, hayana uzito, sio yale matamko ya CHADEMA tuliyozoea, ndio maana wananchi wameyapuuza kwa kutokuja Mahakamani.

10. Kuna haja ya kuanzisha madarasa ya Itikadi, kwenye hili tumuige polepole, tumekuwa Chama cha Matukio na kuchambua hotuba za CCM, Mipango yetu haifiki Mwisho, leo tunakuja na Sera Mbadala, kesho inakufa, tunakuja na CHADEMA ni msingi, mara Katiba Mpya, ni kama tunaongozwa na matukio, hatuna Itikadi inayotuongoza.View attachment 1882740View attachment 1882741

Hizi propaganda msumuwekee Bananga tu maana kwa sasa iwe ni yeye ameandika, au mmemlisha maneno, hakuna mwenye imani na yeye maana ameamua kusimama na mke wake. Katungeni ya Slaa, ama kamuulizeni myalete humu jukwaani.
 
Back
Top Bottom