Binafsi siwezi kupongeza

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,506
Wanaochimba madini yetu wameruhusiwa na Serikali ya CCM kwamba wakivuna sh 10,000 (elfu kumi) sisi watuachie sh. 400 (mia nne) tu inatutosha (na mali ni yetu)! Nazungumzia 4% tu ya mrabaha wa mavuno rasmi yanayojulikana! Vipi tunalia na kisichojulikana, au gawio la 4% ni sawa??

Nashangaa wagonga meza wazee wa Ndiyoooo! wanashangilia michanga kama mazuzu, michanga ambayo bado ni ya wavunaji hata ikiwa na dhahabu tani zote! Uzuri Mikataba yote huridhiwa na Baraza la Mawaziri, Rais akiwa Mwenyekiti wake. Bunge limetengwa.

#Mbu_Hawezi_Kutibu_Maleria_Kamwe
_______
Major Mines in Shamba la Bibi (Tanzania)
1. Buzwagi Gold Mine
2. Bulyanhulu Gold Mine
3. Geita Gold Mine
4. Golden Pride Mine
5. TanzaniteOne Mine
6. Williamson Diamond Mine
7. StamiGold Biharamulo Mine

Hebu watafute wazawa wa maeneo hayo, angalia maisha yao, afya zao..., ni kama wamezaliwa kwenye laana!
 
Kajifunze Maana ya mrabaha uje uandike upya.
Au kwa nini migodi ilipe mirabaha 4% na sio kodi Ile ya 3o%.
Na ni wakati gani mrabaha unalipwa na wakati gani kodi halisi inalipwa
Jifunze pia kwa nini Geita GGM wanalipa kodi na sio mrabaha tena...
Sio kitu cha tanzania ni duniani kote....
 
Natamani hili suala liendelee... Atumbuliwe yule.. Atumbuliwe na yule... Na yule.... Na yule...mpaka mwisho wananchi wajue kuwa mbaya wetu ni ccm..!
 
Rais anajitahidi. Lakini aende mbali zaidi. Ajiulize kwa nini alipokuwa kwenye cabinet hakushawishi Tanzania ifuate mwendo wa busara wa Botswana iwapo tuko nao kwenye SADC? Botswana inafanya vizuri mno. Kila kiongozi hapa anajua. Kwa nini tulishindwa kufuata mfano wao?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom