Binafsi, huu ndo uzalendo wa kweli

Binafsi, huu ndo uzalendo wa kweli

dustless

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2016
Posts
796
Reaction score
714
Ni hivi karibuni tumeshuhudia washika mpini wa ngazi za juu kabisa wakionesha uzalendo wao kwa kuwatumikia wanyonge.

Mkulu kakabidhiwa majengo na mkapa foundation kwenye kijiji cha wanyonge sana maeneo fulani kanda ile ya kule.

Waziri mkubwa nae amekabidhi magari ya kisasa ya wagonjwa kwa wanyonge sana wa kusini. Hii ni katika kubalance kero maeneo mahususi ya wanyonge sana nchini.

Hili ndo watanzania tulilolitarajia, kushughulika na wanyonge sana kwanza, kwa maana kila mtanzania mpenda haki analifahamu hilo.

Unajua, ukweli ni kwamba kuna wanyonge sana, wanyonge, na maskini. Sasa waneamua kwa dhati kabisa kudili kwanza na wanyonge sana.

Ni sawa na kuhudumia wagonjwa tu, nguvu kubwa huelekezwa ICU baada ya hapo wagonjwa wa kawaida wanafuata.

Ni jambo la subira tu, wakimaliza huko watahamia kwa wanyonge na kuhitimisha na maskini. Hili halihitaj phd ya Harvard kulitambua.

Nawasilisha.

Sent from my Infinix HOT 4 Lite using JamiiForums mobile app
 
Pole kwa kuwa bado upo katika ulimwengu wa kuamini ili kitu kiitwe maendeleo ni pale lami inapojengwa lepurko monduli
 
Sijui lini kwetu kutakuwa kwa Wanyonge sana...

Maana majuzi tu tulimpata Waziri Mkubwa kwa miaka nane lakini akatuona sisi ni matajiri au wanyonge kidogo tu, yaani hata barabara ya kuunganisha mkoa wetu na ile mitatu ya jirani hatukujengewa.
Wanyonge wenye bahati sasa hivi wameshapata international airport...

Ngoja nisubiri second chance huenda ikajitokeza.
 
Tatizo kwenu mna hela mno, firisikeni muone misaada inavyomiminika.

Sent from my Infinix HOT 4 Lite using JamiiForums mobile app
 
Tatizo kwenu mna hela mno, firisikeni muone misaada inavyomiminika.

Sent from my Infinix HOT 4 Lite using JamiiForums mobile app
Kwetu hatuwezi kufilisika kamwe. Unafilisikaje wakati haujawahi kutajirika?
 
Back
Top Bottom