Binadamu watu wa ajabu sana!

Mitchell

JF-Expert Member
Oct 29, 2010
740
722
Kulikuwa na Mfalme mmoja mpenda haki aliyetawala miongo ya nyuma. Sasa wakati anaingia katika ufalme akasikia katika wale anaowaongoza yaani watu wake kuwa kuna maadui wawili wakubwa ambao hawapatani kabisa. Sasa mfalme akawaita na kuwaambia jamani mie ndio nimetawazwa kuwa mfalme mpya na katika vitu ambavyo nitavizingatia katika kipindi changu cha uongozi ni amani. Hivyo nawaagiza leo hii hii mpatane na mmalize ugomvi wenu na baada ya kupatana nitawapa zawadi. Hivyo mtu wa kwanza kutamka zawadi atakayo wa pili atapokea mara mbili. Maadui wakaangaliana nani aanze kwani ukianza tu mwenzio anapokea mara mbili.


Basi wa kwanza akasema Mtukufu Mfalme naomba nitolewe jicho moja, mfalme akashangaa ila kwa kuwa mfalme akisema ni sheria basi akatolewa jicho moja na yule wa pili akapokea zawadi yake mara mbili yaani akatolewa macho yote mawili.
 
..............Hadithi hii inatufundisha nini!.............
 

Ingekuwa fresh hizo sheria zingetumika kwenye hii serikali ya Magamba
 
<br />
<br />
nlikuwa darasa la pili ama la tatu vile..kind of memory heeh.!
 
Inavyoonekana we ni mswahili ila hujui kiswahili hivi kuandika binadamu ni watu ni sahihi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…