Bin zubery na uongozi wa simba kuna nini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bin zubery na uongozi wa simba kuna nini?

Discussion in 'Sports' started by JATELO1, Aug 15, 2012.

 1. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #1
  Aug 15, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Wana-JF,
  Baada ya majuzi tu kuwa na makala iliyoandikwa zaidi ikimdhalilisha mwenyekiti wa Simba S.C, ndugu Aden Rage, na pia kuwa na mifululizo ya habari za kuikashfu Simba hasa Viongozi wake mara simba wamewapigia magoti viongozi wa Azam kuhusu Redondo, na baada ya muda mfupi huyo huyo anaibuka tena kwenye blog yake ya Bin Zubeiry na kukanusha habari hizo anazoziandika mwenyewe, leo tena kuna makala kaiandika tena na hasa akimshambulia benchi la ufundi la Simba chini ya Maestro. ebu som amwenyewe na hasa kwenye alama nyekundu hapo chini. Swali moja najiuliza na sijapata jibu lake, kwamba kuna nini kati ya viongozi au klabu ya Simba na huyu Bin Zubeiry?


  Na Mahmoud Zubeiry

  KATIKA Simba Day, Agosti 8, mwaka huu Simba SC ilitangaza usajili na kuonyesha jezi za wachezaji zikiwa na majina mgongoni kupitia screen kubwa la Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam- lakini wakati dirisha la usajili linafungwa leo saa 6:00 usiku, klabu hiyo inatarajiwa kufanyia ‘editing video ya Simba Day’.


  Katika Simba Day, ilionekana jezi ya Mbuyu Twite, Danny Mrwanda na Kanu Mbivayanga, lakini hivyo ni vipande ambavyo leo vinatolewa na kuingizwa vipande vipya kama vya picha za Paschal Ochieng kutoka AFC Leopard ya Kenya na Daniel Akuffo kutoka Hearts Of Oak ya Ghana.
  Simba imelazimika kurekebisha usajili wake dakika za mwishoni, baada ya kugundua mapungufu makubwa, yaliyotokana na ushauri mbaya wa Kamati yake dhaifu ya Ufundi, inayoongozwa na Mwenyekiti asiye na uzoefu wala ujuzi wa kuendana na hadhi ya klabu hiyo, Ibrahim Masoud ‘Maestro’.


  Katika marekebisho hayo, Simba imewatema beki Lino Masombo na kiungo Mbivayanga kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), ili kuwasajili Ochieng na Akuffo. Lakini pia, Simba imemtema Mrwanda wakati habari zaidi zinasema kuna wachezaji wengine watatu, wawili kutoka Mali na mwingine mmoja kutoka Ivory Coast, miongoni mwao wanaweza kusajiliwa.
  Mapema jana, ilielezwa kiungo Mganda, Mussa Mudde angetemwa, lakini baadaye ikaelezwa huyo hataaachwa tena, badala yake wanasubiriwa wachezaji kutoka Mali na Ivory Coast waonekane, kisha walinganishwe na Ochieng kabla ya klabu kuamua imsajili nani.


  Simba ina kutwa moja tu hadi saa 6:00 usiku wa leo kuhakikisha inakamilisha usajili wake, tayari kwa msimu mpya wa Ligi Kuu, wao wakiwa mabingwa watetezi.

  Source: Bin Zubeiry blogpot.com
   
 2. mndwadage

  mndwadage JF-Expert Member

  #2
  Aug 15, 2012
  Joined: Jul 15, 2012
  Messages: 345
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hajadanganya kitu.!
   
 3. M

  MTUNZA AMANI Senior Member

  #3
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 2, 2012
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ni kweli tupu,mleta thread ni kipi BIN ZUBERY alichodanganya hapo?? Hebu usituletee habari za udaku humu JF, kama unafikiri humu ni jamvi la wajinga nenda kafanye hivo facebook siyo humu.
   
 4. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #4
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  positive, tafta meaning ya word BlackOut in journalism
   
 5. m

  makumvi Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 26, 2012
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nakubaliana na mwandishi kuhusu mabadiriko ya usajili wa timu ya simba, binafsi ni mpenzi wa simba lakini nakerwa sana na mwenendo mzima wa usajiri wa wachezaji katika timu hii msimu huu, viongozi wamekuwa na majigambo pale wanapompoint mchezaji fulani aje kuchezea simba, sifa zinakuwa nyingi kwamba mchezaji fulani ni baabkubwa, halafu baada ya muda fulani unasikia mchezaji anakatishiwa mkataba wake, hii inamaanisha nini ? kama mchezaji anakuja kwenye timu na mnaona hamna uhakika wa kumsajiri kwanini ujigambe kwamba umepata mchezaji mzuri, unamsajiri na baada ya mwezi moja au miwili unatangaza kumtema kwamba hanasifa ya kucheza kwenye timu? mbona mambo haya hatuyasikii kwenye vilabu vingine, kwanini simba tu ? ni kweli kunamadhaifu sana kwenye kamati nzima ya usajiri ya simba na siyo kumtaja mtu moja kama Maestro maana itakuwa ni uonevu na uchonganishi kwa wapenzi na wanachama wa simba
   
 6. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Hayo ni ya Bin Zubeiry: lakini kwa hakika benchi la ufundi la timu ya Simba linayumba, Ibrahim Masoud ''Maestro'' kama mwenyekiti hanabudi kutupa maelezo ya kutosha juu ya utendaji kazi wao hususani ktk kipindi hiki cha usajiri.
   
 7. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  ukweli unauma vibaya sana
   
 8. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nimechelewa sana kuuona uzi huu,ajabu ndo nauona sasa hivi kwa mara ya kwanza,anyway nimependa kitu kimoja hapa...kumbe hata wewe PrN kuna kipindi huwa una think great!!!!
  Nimekuongeza kwenye list yangu ya Wana Simba wanaoonekana vichwa ambayo ilikuwa imekaa na mtu mmoja (Masuke) kwa muda mrefu sana.
   
 9. mtu chake

  mtu chake JF-Expert Member

  #9
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 20, 2010
  Messages: 4,094
  Likes Received: 1,269
  Trophy Points: 280
  .muandishi yuko sahihi kabisa...
   
 10. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,021
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280
  Wazembe hao.........
   
 11. LUCIFER

  LUCIFER Senior Member

  #11
  Aug 16, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 181
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Agent wa Mafisadi thanx kwamba watu washakujua......
   
 12. afrique

  afrique JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 495
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  afadhali na wewe mwana smba umeona,sasa hayo majibu ya maestro yamabase wapi?mi sijamuelewa kabisa
   
Loading...