Kwenye red, bima ya mkopo inamlinda mtoa mkopo dhidi ya kupoteza fedha zake ikitokea mkopeshwaji amefariki au amepata janga lolote linaloweza kupelekea ashindwe kulipa deni.
Kwa mfano, umekopeshwa na taasisi fulani ya kifedha na mkopo umekatiwa bima Shirika la Bima la Taifa (NIC), ikitokea umefariki, kwa kuzingatia Kipengele Na. 6.0 cha Sera ya Bima (Credit Life Assuarance Policy), mkopeshaji atapeleka madai ya kulipwa kiasi cha fedha ambacho ulikua bado hujalipa pale umauti ulipokukuta.