Kaka Ndallo kuna fomu ulitakiwa ujaziwe kwenye hicho kituo ulichokosa huduma ukachukue hizo dawa kwenye duka ambalo limesajiliwa na NHIF, kila kituo cha matibabu ambacho kimesajiliwa na Mfuko huo kinatakiwa kuwa na fomu hizo wakiwa hawana dawa lazima ujaziwe ili ukachukue dawa ulizokosa kwenye pharmacy au duka la dawa muhimu lililosajiliwa na Mfuko!!Mimi ni mmoja wa familia ninayetumia kadi ya bima ya taifa, lakini chakushangaza huduma ya bure niliyoiona ni kua niliandikiwa dawa lakini dawa nilizopewa bure kupitia bima hii ya taifa ni Paracetamol lakini dawa nyingine nikaambiwa nikanunue!
Mnanishauri nini?
Asante Karikenye! Ngoja niugue tena halafu nifuate ushauri wako.Kaka Ndallo kuna fomu ulitakiwa ujaziwe kwenye hicho kituo ulichokosa huduma ukachukue hizo dawa kwenye duka ambalo limesajiliwa na NHIF, kila kituo cha matibabu ambacho kimesajiliwa na Mfuko huo kinatakiwa kuwa na fomu hizo wakiwa hawana dawa lazima ujaziwe ili ukachukue dawa ulizokosa kwenye pharmacy au duka la dawa muhimu lililosajiliwa na Mfuko!!
Mimi ni mmoja wa familia ninayetumia kadi ya bima ya taifa, lakini chakushangaza huduma ya bure niliyoiona ni kua niliandikiwa dawa lakini dawa nilizopewa bure kupitia bima hii ya taifa ni Paracetamol lakini dawa nyingine nikaambiwa nikanunue!
Mnanishauri nini?
wacha kumpotosha mwenzako. wengine wana kadi hiyo ya nhif na wanaishukuru kila kukicha. mwacho aipate ajionee mwenyewe. akishindwa atahamia hizo zingine.
wacha kumpotosha mwenzako. wengine wana kadi hiyo ya nhif na wanaishukuru kila kukicha. mwacho aipate ajionee mwenyewe. akishindwa atahamia hizo zingine.
Nina experience mbaya sana na hii Bima pamoja na kuwa nakatwa hela nyingi sana. Sipati value for money. Ila mtu kama anataka bora kwenda hospitali tu bila huduma bora it is ok. Mie nataka huduma bora maana wanachukua hela zangu nyingi sana. Kama unakaa hospitali hours bila huduma ya maana utasemaje? kama matibabu ni expensive mpaka uende ukaombe upewe kibali. Naomba nini wakati wana hela zangu? Mbona hela zetu wanachukua tu hawaombi kibali kwetu? hii experience niliyoipata nawe utaipata tu siku moja halafu utakubaliana na mimi. Hapa naongelea magonjwa sugu sio magonjwa madogo madogo. Haya mbona hayana shida!!!!
mimi binafsi naishukuru sana bima ya afya ya taifa na hata nikikosa dawa hosptal kuna maduka yana huduma hizo kwa hiyo nikiugua na sina pesa bado ni na amani
Maduka yako mengi sana kwenye karibia miko yote na takribani wilaya zote itategemea wewe uko wapi cha msingi hawa jamaa wana ofisi kila mkoa unaweza ukaenda ofisini kwao wakakupa list of acceredited facilities kwa eneo unaloishi au hata ukiwatumia email watakutumia tumaduka hayo yako wap na wap mzee, inawezekana tukafa na kadi ndani kwa kukosa taarifa, orodhesha kama unayajua mzee.
... maisha yamerahisishwa sana siku hizi kaka, dumbukiza NHIF kunako google search engine utawapata. Rahiiiisi!
Mimi ni mwanachama na nimekuwa nikifaidika na Bima ya Afya Tangu mwaka 2002 na nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mafao ya hawa jamaa. Kitaalamu NHIF au Bima ya afya wanatumia system inayoitwa FEE FOR SERVICE ambayo hakuna kikomo cha gharama kwenye matibabu na unaweza kupata huduma wewe na wategemezi wako watano kwa maana ya wewe,mwenzi wako wa ndoa,watoto wako na wazazi wakoau hata wakwe zake na kuwa na jumla ya wanufaika sita na wote mnapewa vitambulisho ambavyo unaweza kupata huduma popote Tanzania kwenye hospitali zote za serikali,mashirika ya dini,za watu binafsi na na pia wamesajiri pharmacy ili ukienda na kukosa dawa kwenye hospital unapewa form ya kwenda kuchukua dawa. Na gharama ya kujiunga kwa mtu binafsi ni Tshs 964,800 na unapaswa tu kuandika barua kwao na kuwa na wadhamini wawili ambao ni wanachama wa NHIF. Hao wanaokushauri kwenda Private Insurance ni kwamba wao wana tumia capitation Method ambayo ina ceiling limit ya cost za matibabu na wana pima Health status ya wanachama wake na especially kama una mtu mwenye clonic desease wanamkataa hasa kansa,kisukari,figo wakati bima ya afya wao wanasema Organisation yao haiku katika misingi ya kibiashara wala lengo la kutengeneza faida bali kutoa huduma. kwa Dar ofisi zao ziko Makao Makuu ni Kurasini Bendera tatu jirani na makao makuu ya Bandari,Temeke jirani na Hospitali ya Temeke,Kinondoni wako Mwenge njia ya cocacola JOSAM House na Ilala wako Ocean Road hospital au watafute kwenye www.nhif.or.tz au wa email info@nhif.or.tz