Bima ya afya ya Taifa (NHIF) msifanye ufisadi huu

kalaghesye

Member
Jan 16, 2012
79
11
Ni muda mrefu sasa kumekuwepo na wito wa wadau kuutaka mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa kuboresha vitambulisho vya wanachama wake ili kupambana na kughushi ambako kunaupotezea mapato mfuko na kuanza kutishia uwepo wake. Watu wanatibiwa kwa vitambulisho visivyo vya kwao na pia mfumo mzima hauko makini katika kudhibiti malipo endelevu kwa mfano ya watu wanaoripotiwa kuwa walilazwa na wale wenye magonjwa ya kudumu kama Kansa, Kisukari, Shinikizo la Damu na magonjwa ya figo!

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa kunafanyika tafiti kadhaa za kuweka mfumo ulio bora utakaowezesha kufanyika utambuzi sahihi wa wanachama wanapokwenda kupata huduma katika hospitali na maduka ya dawa. Pia kuwezesha watoa huduma walipwe kwa mujibu wa huduma sahihi walizotoa. Hata hivyo jitihada hizi zimekuwa zinavurugwa na vitendo vyenye viashiria vya ufisadi. Kuanzia mwaka 2010 kumefanyika zaidi ya tafiti (Studies) tano na watu kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya kupata uzoefu lakini jitihada zote zilivurugwa pale watu wa kitengo cha TEHAMA, chini ya uongozi wa Mkurugenzi Bwana Ali Othman waliposhindwa kuona upenyo wa kutengeneza fedha haramu.

Hivi karibuni kwa kushirikiana na mpango uliokuwa umeasisiwa na Bwana Jack Gotham akimtumia Rama Mwikalo (ambaye anajulikana kama mshauri mtaalamu wa TEHAMA na alishiriki katika kubuni mradi wa vitambulisho vya Taifa) walikuja na andiko ambalo kwa kiasi kikubwa linaakisi tafiti zilizofanyika huko nyuma! Utekelezaji wa kutengeneza vitambulisho vya Bima ya Afya, kwa mujibu wa andiko hilo, utagharimu zaidi ya Shs. bilioni 50/= ambazo NHIF wanatakiwa wazitoe kwa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ili kutengeneza vitambulisho hivyo! Hapa ndipo ulipo muunganiko wa ufisadi.

Mpango huu umekuwa unaasisiwa kwa siri na umakini mkubwa na pande tatu : (1) NIDA : Mkurugenzi Mkuu wa NIDA aliyesimamishwa Kazi kwa tuhuma za ubadhirifu Bwana Dickson E Maimu na Mkurugenzi wa TEHAMA NIDA Joseph Makani) (2) Kaimu Mkuregenzi Mtendaji NHIF Michael Mhando, Mkuregenzi wa TEHMA NHIF Bw. Ali Othman na Mkurugenzi wa CHF Eugen Mikongoti (3) Wawezeshaji : Jack Gotham na Rama Mwikalo.

Kiasi cha fedha hizi ni kikubwa sana hasa ikizingatiwa kuwa tayari vifaa vya kutengenezea vitambulisho vipo na pia kuna wanachama wa NHIF ambao tunaamini tayari wana vitambulisho vya NHIF hivyo hakutakuwa na haja ya kuwapatia vitambulisho vingine zaidi ya kuweka alama tambulizi kwenye kanzi data husika.

Aidha, NIDA haijaonyesha ufanisi katika utendaji wake maana ukichukua ulinganifu wa utendaji wa kutoa vitambulisho kati ya NIDA na NEC, unaona kuwa NEC wana spidi nzuri. Imewachukua NIDA zaidi ya miaka mitano na bado hawajafikisha idadi ya watu walioandikishwa na NEC ndani ya miezi mitano (pamoja na madhaifu yao) ambayo isingekuwa siasa yanarekebishika. Lakini NIDA wametoa vitambulisho hata kwa watu wasio raia! Je, wakitoa vitambulisho vya NHIF kwa watu wasio raia si mfuko utakufa kwa kulemewa!

Ni vyema Bima ya Afya wakafikiria tena huu mkakatai maana fedha hizo ni nyingi sana na madhumuni ya ushirikiano na NIDA wakizingatia maslahi mapana na muda mrefu ya sera ya Afya ya nchi na kulinda michango ya wananchama ambalo ndilo jukumu kubwa la Mfuko.

Bwana Michael Mhando na Ali Othman kumbukeni kuwa fedha zilizopo NHIF ni michango ya wanachama na hivyo ni lazima zitumike kwa faida. Nyie mmepewa jukumu la kuzilinda. Kuna namna nyingi sana za kutengeneza vitambulisho bora, vya gharama nafuu na vya kisasa kuliko mfumo huo uliobuniwa kwa mashaka na Bwana Joseph Makani na Ali Othman kwa kuwashirikisha viongozi wa Taasisi husika.

Tunashuhudia matatizo yaliyotokea NIDA, matumizi ya zaidi ya Sh. bilioni 179/- na kazi haijaisha, sasa si vyema kabisa NHIF ikajiingiza kwenye mtego wa Jack Gotham na Rama Mwikalo ambao ni waasisi wa NIDA na walibuni mradi uliozaa NIDA kwa kuhakikisha kuwa (kwa kutumia ushawishi wao katika utawala wa Awamu ya 5) Bwana Dickson Maimu kutoka Idara Kuu ya Utumishi, kisha RITA na hatimaye NIDA ambayo leo inaonekana kuwa ni jipu.

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa NHIF, Bwana Michael Mhando usisubiri kutumbuliwa anza mwenyewe kujitumbua na kisha kuyatumbua majipu yaliyopo Bima ya Afya.
 
Back
Top Bottom