Imekuwa kawaida kwa Dawasco kuleta bili ya maji katikati ya mwezi kipindi ambacho wateja wengi hawana hela za kulipia kwa sababu mishahara hua inatoka mwisho wa mwezi. Matokeo yake wateja wanashindwa kulipa bili na mwisho wake wanakatiwa maji.Gharama ya kuyapata hayo maji tena inakuwa kubwa sana kwa sababu utalipia maji na adhabu vyotex viwili.Awali tuliomba bili za maji ziwe zinaonyesha unit za maji mteja alizitumia na bahati nzuri hilo Dawasco wamelifanyia kazi ni nina uhakika malalamiko mengi juu ya utata wa gharama kutokwenda sambamba na matumizi halisi ya maji hayatakwepo tena.Kulikwepo na malalamiko mengine kuhusu ukataji holela wa maji ukihusishwa na kujipatia mapato ya ziada.Wateja wengi wanapokatiwa maji wafanyakazi wa Dawasco wananufaika maradufu na faida inayotokana na gharama za kurudisha maji.Kwa hiyo wanapoleta bili ya maji katikatika ya mwezi wakati wanafahamu dhahiri watu hawana mishahara wanakuwa wameweka MTEGO wa panya wakijua lazima panya watanasa tu.Wateja watakuwa hawana hela na wengi watakatiwa maji na wakipata mishihara lazima watalipa tu kwa sababu maji ni uhai na wao tayari watakuwa wamevuma kile walichotega.Tunamwomba Meneja mkuu wa Dawasco abadili mfumo huu kuviziana wa kutuma bili katikati ya mwezi kama nia ni kujipatia faida kubwa abuni njia nyingine hii tumeishitukia.