Bill Gates anywa maji ya Kinyesi

Bill Gates anywa maji ya Kinyesi

Kilaza

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2013
Posts
3,324
Reaction score
1,378
150107223336_bill_gates_512x288_billgates_nocredit.jpg

Bill Gates akinywa maji yaliotengezwa kutokana na kinyesi

Mmiliki wa kampuni ya Microsoft Bill Gates amekunywa maji yaliotengenezwa kutokana na kinyesi cha binaadamu kama maonyesho ya teknolojia mpya itakayoweza kutoa maji safi katika mataifa yanayoendelea.

Mwanzilishi huyo wa Microsoft amesema kuwa ataisambaza mitambo ya teknolojia hiyo mpya kote duniani baada ya kuifanyia majaribio mwishoni mwa mwaka huu.

Teknolojia hiyo imeungwa mkono na shirika la WaterAid ambalo limesema kuwa itasaidia sana katika maeneo ya miji.

Kulingana na shirika hilo la hisani takriban watu millioni 748 hawana maji safi ya kunywa.

Katika kanda ya video iliyowekwa katika blogu yake, Bwana Bill Gates alishuhudia kinyesi cha Binaadamu kikiingizwa katika mtambo huo kabla ya kunywa maji yaliokuwa yakitoka kutoka kwa kikombe.

''Maji hayo ni mazuri sana ikilinganishwa na maji yoyote yale niliokunywa, na baada ya kusomea teknolojia hii nitayanywa kila siku''.

Maji haya ni salama kabisa'', aliandika katika blogu yake. Kulingana na mtengenezaji wa mtambo huo Peter Janicki, maji taka hayo huchemshwa kabla ya mvuke wa maji hayo kutengwa na taka ngumu.

Taka hizo ngumu baadaye huwekwa katika moto na kutoa mvuke unaoendesha mashine zinazotoa nguvu za umeme kwa mtambo huo na pia kwa wakazi wa eneo hilo.

Maji hayo baadaye hutiwa ndani ya mtambo wa kusafisha maji ili kutoa maji safi ya kunywa.

''lakini kwa nini mtu awe na wazo la kubadilisha uchafu kuwa maji ya kunywa na umeme'', aliuliza Gates.

Jibu aliloandika ni kwamba kwa sababu magonjwa yanayosababishwa na mazingira machafu huwaua watoto 700,000 kila mwaka na huwakinga wengine wengi dhidi ya kuathirika kiakili na kimwili.

Chanzo: BBC
 
Hapo mmegusia kitu cha umeme,itapigwa vita gharama za uendeshaji ni kubwa mno ,wakati wao wanatumia magari yanaokula mafuta mno ,kwa kuwa obey,upanga,masaki maji yanamwagika 24/7 watu wa tabata,kimara,na maeneo mengine ya nchi hawatapewa kipaumbele,ili dawasco isife itabidi mitambo hiyo ipigiwe zengwe hata kama darwasco inaonekana kuelemewa na idad ya watu wanahoitaji huduma toka kwao,Wasofikiria wenzao nawaona wakisimama wazi wazi wakitumia mamlaka yao kuelezea gharama kubwa sana kuziendesha hizi mashine bila kukumbuka kupitia magar yao ya maji wanamuuzia mtanzania dumu moja 500-1000 .Kina bill gates wanatuwazia namna ya kutupunguzia ugumu wa maisha,lakin wasimamizi wetu wanawaza watuumize vipi kila kukicha( bei ya mafuta imeshuka duniani tanzania bado ile ele).SHIKAMOO EDDO KUMWEMBE.
 
Teknolojia safi sana...ila anamoyo kuona kabisa kinaingia kinachujwa kinatoa maji aisee duh mi ningeanza kuumwa kabla ..
 
Kiu ni kiu tu lazima ikatwe, ila kwenye chupa wasiandike wala mtu asiniambie hayo maji yametokana na kinyesi.
 
Mmmmh, kwani huyu baba. Bado ni mmiliki wa Microsoft corp?
Asha drop hata u chairman na ka liquidate his most shares
 
Hii teknolojia si mpya mbona. Nchi zote zilizoendelea wanatumia mfumo huu wa maji safi. Wanaita recycled water. Hata hapa Africa kuna baadhi ya nchi wanatumia mfumo huu kwa miaka sasa.
 
Hii teknolojia si mpya mbona. Nchi zote zilizoendelea wanatumia mfumo huu wa maji safi. Wanaita recycled water. Hata hapa Africa kuna baadhi ya nchi wanatumia mfumo huu kwa miaka sasa.

mkuu hujaelewa sio maji machafu wanayafanyia recycling hapa wanachukua mavi yako wanayageuza maji ya kunywa

hiyo recycling hata bongo Tunafanya
 
kwanini Hisiwe Mji Ya Bahari Au Mikojo?
 
Biashara ni akili. Hapo ni kutangaza biashara na kwa kuwa dunia inona mbona hata Bill gates kayanywa basi ni salama. Kumbe labda alikunywa tofauti baada ya kuingizia faidia utawasikia kiwanda kimefungwa kwa kukiuka tarataibu za usalama wa afya.
 
Back
Top Bottom