Bill Gates amuonya Trump kuhusu Afrika

Bill Gates amuonya Trump kuhusu Afrika

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,302
Tajiri Bill Gates amemuonya rais wa Marekani Donald Trump kwa kauli mbiu yake ya "Marekani Kwanza" kuwa inaweza kuharibu ushawishi wa nchi hiyo kwa bara la Afrika.

Bill Gates ametoa kauli hiyo katika mkutano wa dunia wa uchumi World Economic Forum unaofanyika huko Davos nchini Switzerland ambapo amesema kunatakiwa kuwepo kwa uwiano wa wenye nguvu kubwa na nguvu kidogo na kuanisha kwamba asingependa kuona uwiano huo unapotea.

Bill Gates amesema kwamba Marekani inaweza kupoteza ushawishi wake barani Afrika kwa nchi kama China ambazo zinazidi kuwekeza barani Afrika, Bill Gates ambaye anamfuko wake unaoitwa Bill & Melinda Gates Foundation, umekijihusisha kwa kiasi kikubwa kutoa huduma za afya katika nchi kadhaa barani Afrika.

Lakini rais Trump amesema kwamba atakata msaada wa bajeti wa afya kwa takribani dola bilioni 2.2 katika mfuko wa dunia. Pia Trump aliwakasirisha viongozi wa Afrika bada ya kuyaita mataifa ya Afrika machafu kupindukia.

Kwa hisani ya EATV

Trump.jpg
 
real G Bill Gates ni mpuuzi, Trump yuko sawa na Afrika inabidi tujipange kujisaidia wenyewe, kwangu D.Trump kaletwa na Mungu ili kutuambia ukweli, watu kama Bill Gates ndo maracists wakubwa kwani wanaamini sisi siyo binadamu kamili na tunahitaji kusaidiwa!
 
Hahaha makamu wa papa Francis hajamuwakilisha papa huko Davos, maana papa anajua kilatin pekee.
 
Bill Gates ni mpuuzi, Trump yuko sawa na Afrika inabidi tujipange kujisaidia wenyewe, kwangu D.Trump kaletwa na Mungu ili kutuambia ukweli, watu kama Bill Gates ndo maracists wakubwa kwani wanaamini sisi siyo binadamu kamili na tunahitaji kusaidiwa!

Fvck Bill Gates!
Ume catch
 
Siyo ubinadamu kumudharau mtu wa chini uliyemnyonya kiuchumi na kujitajirisha(Afrika) trump hayuko sahihi,kila mwafrika anakiu ya maendeleo ila sera mbaya za wakoloni
 
Siyo ubinadamu kumudharau mtu wa chini uliyemnyonya kiuchumi na kujitajirisha(Afrika) trump hayuko sahihi,kila mwafrika anakiu ya maendeleo ila sera mbaya za wakoloni
Sio sera mbaya za wakoloni, sema sera mbaya za viongozi wetu.
 
Makini sana Mkuu, mtu anayelilia kuwa tusaidiwe ana maana kuwa sisi hatujiwezi na hatupo sawa na wao wanaoweza kujisimamia wenyewe.

Haya matusi ya kisirisiri ni lazima tuyakatae kama kweli tunataka maendeleo.
 
Siyo ubinadamu kumudharau mtu wa chini uliyemnyonya kiuchumi na kujitajirisha(Afrika) trump hayuko sahihi,kila mwafrika anakiu ya maendeleo ila sera mbaya za wakoloni
Matatizo ya Afrika ni ya Waafrika wenyewe. Ukiishang'amua hilo ndio mwanzo wa maendeleo. maendeleo hayaji kama hisani bali ni struggle. Ukishindwa usimlaumu mwingine.
 
Matatizo ya Afrika ni ya Waafrika wenyewe. Ukiishang'amua hilo ndio mwanzo wa maendeleo. maendeleo hayaji kama hisani bali ni struggle. Ukishindwa usimlaumu mwingine.
Huwezi ku struggle wazungu wakakuacha bora tu africa ibaki na umaskini wake yupo wapi Gaddaf
 
Huwezi ku struggle wazungu wakakuacha bora tu africa ibaki na umaskini wake yupo wapi Gaddaf
Kwanin tusubiri kudra ya Wazungu?kwani sie tunatofauti gani na wale wa Asia waliokuwa kwenye ukoloni kama sie na leo wapo vizuri.

Tatizo kubwa kuliko umaskini ni kujiona mtu duni, mtu asiyeweza, mtu pungufu ya wengine.
 
Sio sera mbaya za wakoloni, sema sera mbaya za viongozi wetu.
Kweli issue sio ukoloni. Issue ni sisi. Wewe kijana akiajuruwa Bandari anawaza kununia Alteza na kufunga maspika na Exsozi kubwa ili mitaa imkome.
Zipo nchi nyingi zilitawaliwa. Lakini leo wapo wapi? Mfano China.
 
Huyu bill atakuwa mchochezi huyu akamatwe.

Masikini Tanzania.
Watanzania daini katiba mpya na tume huru vinginevyo mtapata tabu sana.
Taifa limegawanyika kabisa.
 
Back
Top Bottom