diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
WAZIRI wa Nishati, Dk Merdad Kalemani amesema Serikali itatumia Sh bilioni 87 kwa ajili ya kupeleka umeme wa gridi mkoani Kigoma ukitokea Tabora na kwamba kazi hiyo itakamilika mwakani. Dk Kalemani alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Nkuba kata ya Kasanda wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma akiwa kwenye ziara ya kiserikali ya siku tatu mkoani Kigoma.
Alisema kuwa tayari utekelezaji wa mradi huo umeanza Desemba mwaka jana na kwamba serikali imedhamiria kuhakikisha mradi huo unakamilika ikapo Aprili mwakani. Serikali imeona ichukue hatua za haraka kuhakikisha umeme wa gridi unaka mkoani Kigoma katika kipindi kifupi kijacho, mahitaji ya umeme mkoani humo ni makubwa hivyo hatua za dharula lazima zifanyike sasa kukabiliana na hilo ambapo umeme wa KVA 130 utasarishwa,” alisema.
Waziri huyo wa nishati alisema kuwa upo mradi wa umeme kutoka Sumbawanga kupitia mkoa wa Katavi ambao utaisha mwaka 2025, upo mradi wa umeme kutoka Nyakanazi utaisha mwaka 2022 ambao ni muda mrefu kwa umeme kuka huko na kwamba mradi wa Tabora ndiyo wa muda mfupi katika mpango huo.
Katika hatua nyingine, Waziri Kalemani amepiga marufuku wakandarasi wa miradi ya umeme vijijini kuruka nyumbani zilizopo kwenye maeneo ya kupatiwa umeme kwa kigezo kuwa nyumbani za nyasi na tembe ambazo hazina bati na badala yake maelekezo yatolewe nyumbani zote zikidhi vigezo.
Alisema kuwa serikali imedhamiria kuona vijiji vyote 149 mkoani Kigoma na vitongoji vyote vinapata umeme ili kutimiza azma ya serikali ya kukisha umeme vijijini uweze kutumika katika kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi. Katika kuhakikisha umeme unafungwa kwenye maeneo yao, Waziri Kalemani aliwataka wananchi kulipia gharama zinazohitajika kulingana na maelekezo ya serikali yaliyotolewa na hakuna gharama za nguzo Wala nyaya ambazo wananchi wanapaswa kulipa.
Akiwa kijijini hapo, Waziri Kalemani alikumbana na malalamiko ya wananchi nyumba zao kurukwa huku wengine wakilalamika kutozwa zaidi ya 150,000 kwa ajili ya nguzo. Alphonce Sabuhoro na Edna Cleophas walisema kuwa malipo ya 150,000 kuwekewa nguzo zimechangia kutopata umeme kwa haraka hivyo wamemuomba Waziri kuingilia kati ili jambo hilo lisiwakwaze.