Bilioni 34 "Zilizopitishiwa" Lugumi Zingenunua Madawati 170,000

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Jeshi La polisi lilingia Mkataba wa kiaina na Kampuni Moja Dubious iitwayo Lugumi Enterprise ili kununua na kufunga mashine za kusoma alama za Vidole. Ikathibitika "Malipo ya 90% ya Bilioni 37 yaani Bilioni 34 yalitolewa.

Mimi naamini Kuwa Fedha hizo ziliibiwa na watu fulani shadowy kupitia kampuni hiyo. Hii Ni sawa na Jinsi ambavyo Mwekezaji hewa (Rwegamalira ambaye hakuwa na mtaji wa shilingi moja IPTL) alitumika kusimania hisa hewa za watu shadowy ambao baadaye walivuna dola Milioni 78 Bila jasho lolote.

Ilikuwa ni Makubaliano ya Kuwaibia wananchi Kwa Ubia wa Mtaji hewa katika IPTL ambao pia mtaji wao ni mdogo sana kulingana na Malipo wanayopewa hadi sasa na Tanesco.

Iwapo fedha hizi zisingeyeyuka, singeweza kutununua Madawati, 170,000 kwa Bei ya 200,000 Kila moja au kujenga Vyoo Vizuri sana Katika Shule Za Msingi 3,400 kwa gharama ya 10,000,000 Kila choo. Au Vitanda ya Hospitali 5,700 vya Hospitali vikiwa na shuka mito na magodoro kwa gharama ya 7,500,000 Kwa Kitanda.

Kama Mh. Magufuli kweli anachukia Ufisadi, Na najua Rafiki yake Kitwanga Yupo, Basi awashughulikie wahusika!
 
Acha wivu wako, kwani hukusikia jinsi Lugumi alivyo mtu mwema katika kusaidia watu? Nasikia wanaomfahamu wanasema hata ukimsimamisha njiani ukamuelewa tatizo inafynguliwa buti ya gari na unasaidiwa papo hapo achilia mbali ukibahatika kukutana naye viwanja. Wananchi hawataishi kwa madawati tu na matumizi mengine ni muhimu!
 
Acha wivu wako, kwani hukusikia jinsi Lugumi alivyo mtu mwema katika kusaidia watu? Nasikia wanaomfahamu wanasema hata ukimsimamisha njiani ukamuelewa tatizo inafynguliwa buti ya gari na unasaidiwa papo hapo achilia mbali ukibahatika kukutana naye viwanja. Wananchi hawataishi kwa madawati tu na matumizi mengine ni muhimu!

Mtu anayegawa hela za Bure ni Dalili ya Kuwa Kazipata Bure au Kiaina, Hivyo Unanisapoti kuwa Kweli yeye ni Mfereji wa Shadowy people Kama Vile alivyo Sonko Kenya na Kabla yake stooge wa "Nyayo" Nicholas Biwott aliyeshukiwa Kuhusika na mauaji ya Dr. Robert Ouko. Hizo pesa za Kugawa Lugumi anapata wapi? Watu wanaozipata fedha zao kwa jasho hawagawi hela!
 
Hilo la mafisadi limemshinda sasa hivi ni kupambana na wapinzani tuu
 
Mkuu madawati,madawa sio muhimu sana kwa viongozi wetu.... maana hapo ni kama wanafunzi 500,000 kwa uchache... but who cares?
Nilikuwa naangalia darasa la shule sehemu moja duniani na wanasema eti wastani wa wanafunzi ni 30 kwenye chumba. Nikachukua picha nyingine kutoka hapa kwetu ndio nikajua kuwa ni bora tungerejesha informal education tuwe na maprofesa kama maji marefu badala ya hawa tunaowahudumia sasa!
 
Back
Top Bottom