mpenda pombe
JF-Expert Member
- Nov 17, 2010
- 1,410
- 722
Isabel dos Santos, bintiye Rais wa Angola Jose Eduardo Dos Santos, , amekuwa mwanamke wa kwa kwanza wa Afrika kuwa Bilionea .
Hii ni kwa mujibu wa jarida la kiuchumi nchini Marekani la Forbes.
Bi Isabel mwenye umri wa miaka 40 anamilikihisa katika makampuni kadhaa nchini Portugal, ikiwemo kampuni moja ya televisheni na benki moja nchini Angola.
Hisa hizo zote zimefikisha mali anayomiliki kuwa na thamani ya mabilioni na hivyo kumuweka kwenye orodha ya watu wenginewanaomiliki mabilioni barani Afrika.
Kulingana na jarida hilo ambalo huandika zaidi kuhusu watu matajiri duniani, biashara yake ya kwanza ilikuwa ya mkahawa mjini Luanda ulioitwa, Miami Beach.
Watu wengi nchini Angola , nchi yenye utajiri mkubwa, wanaishi kwa kipato cha chini ya dola mbili kwa siku.
Angola inajitahidi kukabiliana na athari za vita vya wenywe kwa wenyewe vilivyodumu miaka 27, baada ya nchi hiyo kujipatia uhuru wake kutoka kwa Portugal.
Alisomea uhandisi katika chuo kikuu cha King's College mjini London, ambako alilelewana mamake.
Vita vya Angola vilikamilika mwaka 2002 na nchi hiyo imeweza kuibuka kama mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika,pamoja na kuwa uchumi wake unakuwa kwa kasi .
Familia ya Rais Jose Eduardo Dos Santos ambaye amekua mamlakani kwa miaka 33 , inadhibiti sehemu kubwa ya uchumi wa nchi hiyo.
Duru zinasema kuwa Bi dos Santosa hapendi sana kujionyesha hadharani licha ya kufanikiwa sana kibiashara.
Tangu mwaka kuanza biashara yake ya mkahawa, mjini, Luanda, mwaka 1997, amekuwa mfanyabiashara mwenye ushawishi mkubwa nchini Angola na Portugal.
Akiwa na asilimia 28.8 ya hisa katika kampuniya Zon, yeye ni mwanachama wa bodi ya kampuni hiyo na mmiliki mkubwa wa hisa zake , kulingana na Forbes.