Bilion 100 zapotea BOT baada ya Silvanus Likwellile kutemwa!

Bilion 100 zapotea BOT baada ya Silvanus Likwellile kutemwa!

sirluta

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2012
Posts
6,324
Reaction score
2,494
Ni wiki hii tu kumefanyika mabadiliko ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, leo imeripotiwa kuna bilion 100 zimeyeyuka BOT.

Kuna gazeti limeripoti ngoja litafutwe.

========

CAG_0.jpg

Bilioni 100/- zayeyuka Hazina
SIKU moja baada ya kutimuliwa kazi aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dk. Servacius Likwelile, Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) imebaini ufisadi wa Sh. bilioni 100.5 ambao unaihusisha Hazina na Wizara ya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)

Ufisadi huo ulibainika mjini hapa jana kwenye kikao cha kamati hiyo iliyokuwa ikipitia hesabu za TAMISEMI kwa mwaka wa fedha 2014/15 uliofanyika wakati ofisi hiyo ikiwa chini ya Waziri Mkuu.

Akipitia kitabu cha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) juu ya hesabu za wizara hiyo, Mbunge wa Sikonge, Joseph Kakunda (CCM), alisema vitabu vya hesabu za TAMISEMI vinaonyesha kwa mwaka huo wa fedha, ofisi hiyo ilipewa Sh. bilioni 286 kwa ajili ya miradi ya maendeleo na kwamba asilimia 99.9 ya fedha hizo zilitumika.

Chanzo: Nipashe

Ni wiki hii tu kumefanyika mabadiliko ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, leo imeripotiwa kuna bilion 100 zimeyeyuka BOT.

Kuna gazeti limeripoti ngoja litafutwe.

Soon watakutana na Kitilya KULE.......
 
Ni wiki hii tu kumefanyika mabadiliko ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, leo imeripotiwa kuna bilion 100 zimeyeyuka BOT.

Kuna gazeti limeripoti ngoja litafutwe.

Watuambie Pia Wakati Wa Silvanus Likwellile Pesa Ngapi Zimepotea Hapo BOT, Likwellile Zama Zake Zimeisha Aache Majungu
 
Dah, aliyekuwa Mlipaji Mkuu wa Serikali Dr. Likwelile sasa ataanza kukumbana na mlolongo wa kashfa. Kurasa ya kwanza ndiyo hiyo ya upotevu wa Bilioni 100 BOT. Kurasa zingine tutazisoma baadaye. Hatimaye kufikishwa mahakama mpya ya mafisadi.
 
Ni wiki hii tu kumefanyika mabadiliko ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, leo imeripotiwa kuna bilion 100 zimeyeyuka BOT.

Kuna gazeti limeripoti ngoja litafutwe.
Acha uongo wewe. Gazeti limesema fedha hizo zilipotea huko nyuma na hii imetokana na hesabu za TAMISEMI za mwaka 2014/2015. Usitake kusema kwamba zimepotea baada ya mabadiliko!! Litafute gazeti uandike vizuri badala ya kuhemka
 
HaaAaaaa....B.O.T. EPA ESCROOOO....RICHMOND MLIPAJI MKUBWA B.O.T. NA BADO MTAONA MENGI
 
!
!
scape goat....visingizio kibao. Hii ya majipu ishachuja. Tunataka viwanda Ajira Maisha nafuu Elimu bora Afya Miundombinu haya mapichapicha ya kuhamia Dodoma sijui BOT sijui ufala gani tumechoka.
Tunao jitambua tunapiga kazi ajira baadae na si kukaa na kuisubiri. Kama pesa zinapotea kiasi hicho,kwa nini usijiulize kuwa viwanda vitajengwaje? Muda huu unapinga taarifa za kupotea kwa pesa kana kwamba hutaki ijulikane,unajitambua kweli wewe?
 
Daah bilioni 100!?..yaan mtu akishatoka tu kwenye system hapo mambo ndio yanakua hadharan..sijui kesi IPI ya ufisad itaanza
 
Ni wiki hii tu kumefanyika mabadiliko ya Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, leo imeripotiwa kuna bilion 100 zimeyeyuka BOT.

Kuna gazeti limeripoti ngoja litafutwe.

Acheni uwongo. Likwelile alikuwa naweka hizohela yeye kwenye kabati lake? Fedha za serikali bil 100 zina utaratibu mrefu wa kutolewa na nahisi hata Mh mwenyewe atahusishwa katika kutolewa kwake
 
Acha uongo wewe. Gazeti limesema fedha hizo zilipotea huko nyuma na hii imetokana na hesabu za TAMISEMI za mwaka 2014/2015. Usitake kusema kwamba zimepotea baada ya mabadiliko!! Litafute gazeti uandike vizuri badala ya kuhemka
ni gazeti gani?
 
Nasikia huyu mgeni aliyewekwa ni mtoto wa Dada yake Mkuu.
 
Back
Top Bottom