Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 2,437
- 5,235
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Atembelea Muriet Kufuatia Malalamiko ya Wananchi Kuhusu Kivuko Kibovu
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, leo ametembelea Mtaa wa Muriet, uliopo katika Kata ya Sokoni 1, kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu kushindwa kutekelezwa kwa ahadi ya kujengwa kwa kivuko muhimu kinachounganisha Kata za Muriet, Sinoni, na Lemara.
Wananchi wa eneo hilo wamelalamika kuwa kivuko hicho, chenye urefu wa takribani mita 15 kutoka darajani hadi mtoni, ni kiungo muhimu kinachotumiwa na zaidi ya watu 2,000 kwa siku, wakiwemo wanafunzi zaidi ya 300 wanaoenda shuleni kila asubuhi. Kivuko hicho kwa sasa kimeharibika vibaya, licha ya kujengwa kwa nguvu za wananchi wenyewe, hali inayowalazimu kuvuka kwa taabu au kutumia njia mbadala zinazohatarisha usalama wao.
“Tumechoka na ahadi zisizotekelezwa. Tumeambiwa sana, lakini hatuoni vitendo. Mbunge wetu pia ameshindwa kutimiza ahadi zake. Tunahitaji suluhisho la kweli, na si maneno tena,” alisema mmoja wa wakazi waliokutana na Mkuu wa Mkoa.