Bila Umoja hakuna uhuru, hakuna maendeleo

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Tokea enzi za utumwa mpaka sasa bado tuna changamoto nyingi sana tunakabiliana nazo kama taifa na kama watu weusi. Sababu ambazo zilitupelekea sisi kutaliwa nyingi bado tunazo., tunaishi na kuzilea. Jitihada tunazo zifanya sio za kiwango kikubwa cha kuondokana na shida hizo na changamoto hizo ambazo tulikuwa nazo mwanzo.

Ambazo mababu zetu walikuwa nazo mwanzo. Umaskini, ujinga na maradhi bado yapo.

Watu wetu bado hawajaelimika vya kutosha kujitambua kuelekea kwenye utaifa wao. They do not relate themselves na taifa wao bali na ubinafsi wao, dini zao na kabila zao zaidi kuliko utaifa.

Utaifa upo akilini mwetu kwa kiwango kidogo sana kuliko ubinafsi. Matokeo yake ufisadi unaongezeka. Mambo haya yote ni matokeo ya ubinafsi. Kushindwa kufikiri kuhusu wengine na utaifa na kujiangalia wenyewe. Vitu vinavyopush watu kwenye uongozi sio national interest' Ndio maana viongozi wanajilimbikizia maslahi. Hawana tofauti na wakoloni. Utawala wa sheria ambao unaleta order katika nchi hauzingatiwi kwa kiwango kile kinachohitajika kudhibiti ufisadi na rushwa. Vipaumbele vyetu pia haviko clear difined.

Kuna migawanyiko mkubwa wa uchama na kujiangalia katika uchama bila ya kuwa na national agenda ya pamoja. Bila ya kuwa na vision inayoeleweka bali propaganda, hila na uongo.

Taifa linawezaje kuendelea bila kuwa na vision ya pamoja ambayo iko clear? Katika elimu ni aina gani ya mwanafunzi taifa letu linataka kumzalisha? Mwenye attitude na skill za namna gani?

Kwasababu ili tuendelee lazima tushape mentality za watu wetu. Jinsi wanavyofikiri na kuenenda na kuinduce patriotism. So tunawezaje kuendelea kama hatuheshimu taifa letu?

So inorder to produce a productive citizen lazima kazi ifanyike shuleni na nyumbani. Tujiulize jinsi gani tunawalea vijana wetu ili kuwa raia wenye tija kwa nchi? Sio watu wanao wander bila clear direction?

Serikali wasijidanganye kama wao tu wanaweza kuleta maendeleo pasipo nguvu za wananchi. Lazima wafikiri watawezaje kutumia nguvu kazi tuliyonayo kujiletea maendeleo yetu. There must be a sacrifice sio bure. Mataifa ya ulaya hayakujengwa kwa miujiza walitoil by sweat and blood and great mental sacrifice.

So tumejenga vijana wanaofikiri kuingia kwenye siasa kupata pesa na umaarufu sio kutumikia watu kwa uadilifu na haki. Kama tutakuwa na mtizamo huo mifarakano haitoisha, chuki, wivu, unafiki na unazandiki utaendelea. Watu hawatosimamia ukweli watajipendekeza kwa viongozi ili wateuliwe. There must be a raise of NATIONALISM. Tusikubali kufunikwa na globalism na kuua ukuaji wetu wa ndani. We can relate with other nations and still preserve our identity. Bila kumezwa na ubepari na fikra zao. Kuua ukuaji wetu wa ndani ni kuua our very self. Na kuwa taifa la kuiga iga na kuacha nafsi zetu zisijitambue.

Still wabinafsi Nation consciousness iko chini. Low level of unity of purpose. Ambayo ni force kubwa ya kuleta maendeleo. Still tunafanya kazi kwaajili ya mkate bila vision ya kitaifa. Lazima tujue bila innovation hili taifa halitofikia ndoto yake. What we need as a nation is glory and honor. But we must eradicate some of our behaviours inorder to be productive.

Tunaweza kusema tumefanya baadhi ya mambo, tumejenga bara bara, tunavaa nguo, tunaendesha magari , Nyumba zetu zina umeme na pengine na maji kwa kiwango chake lakini still hatujafikia kiwango cha ukuaji wa watu wetu kiakili kuweza kujitegemea. Hatuna skilled workers wa kutosha wa kuweza kutufanya kujitegemea na wenye ubora na ufanisi unaotakiwa.

Kwahiyo vitu vingi tulivyonavyo ni imported iwe goods au skilled workers wanaokuja kujenga madaraja yetu, barabara na mengine mengi ambayo tunajivunia. Sio kwamba hatuja fanya kitu kabisa tumefanya kiasi. Sio vibaya kujifunza kwa watu wengine lakini utegemezi ukizidi nayo inakuwa sio nzuri sana. Tunapaswa kujifunza kufikiri na kutatua changamoto zetu wenyewe. Na kujifunza kutokana na historia.

Issue ya umoja bado ni changamoto sana ka mataifa mengi ya afrika, watu wetu sio wamoja hatuonani kama watu wamoja ambao wenye mission moja ya kukabiliana na changamoto ambazo wanazo na ambazo mwanzo ziliwapelekea wao kuwa colonise na kuona kamba ni wajibu wao kubadilika ili kubadili destiny yao. Na viongozi wengi hawalioni hili na pengine hawaoni hatari inayoweza kutufikia wanadhani colonisation haiwezi kurudi tena physicaly kwahiyo wana relax na kuponda mali.

Kwamba wazungu wataendelea kutumia puppet kutawala mataifa ya Afrika wakifikiria hivyo watakuwa wanajidanganya sana. Mataifa ya ulaya bado wana nguvu na uwezo wa kuweza kuja tena na kututawala na kutufanya chochote wanachoweza kutufanya, kama hatutajitayarisha kama hatutatumia akili zetu , kama hatutatumia jitiihada zetu za kuwekeza katika maarifa na kuweza kuwa na uwezo wetu wa ndani wa kujilinda na kujitegemea.

Kwahiyo wasijidanganye kwamba wazungu hawawezi kuja tena. Hili jambo tunapaswa kufikiria kwa umakini sana. Migawanyiko yetu ya ndani, kutokuelewana kwetu kama waafrika na kama watanzania hakulisaidii taifa hili. Taifa hili linahitaji sisi kuwa na vision ya moja na malengo ya pamoja. Lengo la kwanza ni kujitegemea kwetu; Kujitegemea kwetu kiakili lakini pia, kiuchumi. Kuweza kuwekeza kimsingi kabisa katika sayansi, masuala ya research and development ili tuwe na uwezo wa ndani wa kutengeneza vitu vyetu wenyewe ili kuweza kufikia at least 80% ya uwezo wa ndani wa kujitegemea wa kuzalisha na kutumia tunachozalisha na sio ku import tu.

Mataifa yote makubwa tunayayaona kinachowafanya yaendelea kuwa makubwa super power kiuchumi na kijeshi, ni uwezo wao wa kufanya inventions ni maendeleo yao katika sayansi. Tunapaswa kuwekeza akili zetu na jitihada zetu huko na kuhamasisha watu wetu katika sayansi bado tuna muda.

Kama msemo wetu wa kiswahili unavyosema penye nia pana njia. Lakini njia hii hatuwezi kuipasua na sisi kupita kama hakuna jitihada na nia ya dhati ya kutaka kujitegemea. Tusipowekeza huko baadae tutakuja kulia tu. Tulitawaliwa mwanzo sababu technologia yetu ilikuwa duni na tutatawaliwa tena sababu ya uwezo mdogo wa kulinda uhuru wetu unaotokana na technologia duni na utegemezi. Sio kwamba hatuwezi lakini ni jinsi gani tuna direct akili zetu kwenye mambo yepi sisi na watoto wetu.

Viongozi wetu na sisi waafrika ni wabinafsi mno. Tunajiangalia sisi lakini hatufikirii pamoja kama taifa. Kuwa na mission ya kitaifa. Kwasababu hili taifa ni kama boti ambalo sisi wote tumepanda na mwelekeo wetu mmoja likitoboka sisi wote tunazama, hakuna hata mmoja atapona, kwahiyo lazima tuwe na vision, sio tu kuwa wabinafsi na kujiangalia sisi, tuwe na mipango thabiti kabisa. Kwenye elimu, kwenye uchumi kwenye kila kitu na jinsi gani tunawatengeneza vijana wetu kifikra kukua katika utaifa na katika uzalendo na kuwa na vision ya kitaifa. Tusipotengeneza watu wenye vision ya kitaifa tukawa na watu wenye mawazo ya kibinafsi binafsi hatutatoka kama taifa.

Na uhuru wetu kama taifa unategemea umoja wetu na maelewano yetu na vision yetu ya pamoja kama taifa. Bila umoja hakuna 'UHURU' nataka watu wafahamu hili. Hatutaweza kulinda uhuru wetu kama watu wetu sio wamoja, kama watu wetu wanaubinafsi kama watu wetu wanawaza kuhusu ubinafsi, hawana vision kama taifa ya pamoja kila mtu anawaza ubinafsi kila mtu anawaza kupata yeye lakini hawafikirii kuhusu utaifa na jinsi gani kuweza kulitoa taifa hili kuweza kujitegemea, na kupata heshima yake miongoni mwa mataifa mengine. Kwasababu hatuwezi kuheshimiwa sisi waafrika kama mchango wetu ni mdogo katika dunia.

Lakini pia bila umoja hakuna maendeleo. Watu lazima waelewe hili. Hatutaweza kulinda uhuru wetu kama watu sio wamoja na wana mawazo ya kibinafsi binafsi yamejaa kwenye akili zao na hawakujengwa katika utaifa na kutumikiana. Kuwa na viongozi mafisadi wasiofikiri kuhusu utaifa . Hatutafikia uhuru wetu wa kiuchumi wala wa kisiasa tukiwa na aina ya mawazo na tabia tulizonazo.

Kuna confusion nyingi katika taifa letu ambazo mwananchi wa kawaida hajui mwelekeo wa taifa lake ambapo kimsingi alipaswa kujua. Siasa zetu bado hazijatoa matumaini ya kutosha kuhusu future yetu kama taifa.
 
Back
Top Bottom