Bila Mapinduzi Z’bar ingekuwa kama A. Kusini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bila Mapinduzi Z’bar ingekuwa kama A. Kusini

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, May 5, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Thursday, May 5, 2011,

  Makala na Uchambuzi, Rai


  Na Siyovelwa Hussein

  HIVI karibuni nilizungumzia suala la kuutazama upya uhuru wa nchi za Afrika.
  Miongoni mwa mambo niliyoyasema ni lile la ukweli kwamba hakuna nchi ya Kiafrika iliyopata uhuru wake kwa juhudi zake yenyewe.

  Nchi zote zilipata uhuru kwa utashi wa wakoloni. Mtetereko wa uchumi uliyaandama mataifa ya wakoloni baada ya Vita Kuu ya Pili ndio uliowalazimisha kubuni mtindo mpya wa kuzinyima nchi za Kiafrika bila kuzitawala moja kwa moja.

  Miaka ya mwanzo ya 1960 ikashuhudia nchi nyingi zikijipatia kile kilichoitwa uhuru japokuwa karibia viongozi wote waliopatiwa uhuru huo walikuwa mawakala wa wakoloni.

  Hata hivyo kwa vile uhuru huo ulitolewa kwa hila na kwa maslahi ya wakoloni, aina ya uhuru huu ilitofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine. Wakati katika nchi nyingine wakoloni walilazimika kuwatengeneza watu wa kuwaachia madaraka, popote palipokuwa na matabaka miongoni mwa wananchi waliokabidhiwa uhuru huo walikuwa lile tabaka bora.

  Katika baadhi ya nchi za Kiafrika kulikuwa na aina mbili ya ukoloni kwa wakati mmoja. Kulikuwapo mkoloni mkuu anayetambulika lakini hata miongoni mwa watawaliwa nako kulikuwa na aina nyingine ya ukoloni.

  Matabaka ya mabwana na watwana. Hali hii ambayo ndiyo iliyokuwapo katika Visiwa vya Zanzibar nchi za Afrika ya Kusini kama vile, Namibia na Zimbabwe ambako kundi la walowezi chini ya Cecil Rhodes lilijitwalia mamlaka ya kuitawala nchi baada ya Wakoloni wa Kiingereza. Nchini Afrika Kusini mpaka mwaka 1910 nchi hiyo ilikuwa chini ya ukoloni wa Kiingereza lakini walikuwapo pia makaburu ambao pamoja na kujiita Waafrika ya Kusini lakini hawakuwahi kuwaona watu Weusi wenye asili ya chini hiyo kuwa ni ndugu zao.

  Kama ilivyokuwa kwa Waarabu wa Zanzibar, kilichowafanya makaburu kuendesha harakati za kumwondoa ukoloni wa Kiingereza haikuwa kutaka uhuru wa nchi utakaomaanisha haki na usawa wa kiraia isipokuwa nafasi ya wao kuwatawala wenyeji wa Afrika Kusini. Mara baada ya Waingereza kujiondoa nchini humo tukashuhudia miaka takriban 80 ya ubaguzi, ukandamizaji, ubabe na unyanyasaji wa makaburu kwa raia wa asili wa Afrika Kusini.

  Zimbabwe nako mambo yalikuwa yale yale. Baada ya Waingereza kujiondoa utawala wa nchi ukabaki chini ya Ian Smith na huo ukawa mwanzo wa utawala wa ukandamizaji na ubaguzi kuliko ilivyokuwa wakati wa ukoloni wa mwingereza.
  Kwa bahati mbaya haya ndiyo yaliyotaka kutokea katika Visiwa vya Zanzibar.
  Kuanzia mwaka 1890, Zanzibar iliyokuwa chini ya Sultan Khalifa bin Harub iliwekwa chini ya uangalizi wa Waingereza.

  Sultan akaendelea na utawala wake lakini mambo yote ya kiserikali yakawa chini ya Waingereza mpaka katika miaka ya katikati ya 1950 ambapo harakati za kisiasa zilianza visiwani humo.

  Hata hivyo, katikati ya mgwanyiko uliojengwa na Waingereza chini ya mwamvuli wa Sultan Khalifa aliyefariki dunia mwaka 1960, harakati nyingi za kisiasa ambazo baadae ziligeuka kuwa vyama vya siasa zilifuata makundi ya kiasili.

  Zilikuwapo harakati za Kiarabu ambazo zilikumbatiwa na Sultan na malengo yake makubwa yakiwa kuendeleza utawala wa Kisultan baada ya kuondoka Waingereza.
  Kulikuwapo harakati za kihindi ambazo zililenga zaidi ustawi wao wa kibishara pamoja na harakati za makabila mengine kama Waafrika na Washirazi.

  Mwaka 1957 na Januari 1961, Waingereza waliendesha uchaguzi wa kisiasa katika Zanzibar huku wao wenyewe wakionekana wazi kukipendelea chama kilichokuwa na uhusiano na Sultan.

  Kwa bahati mbaya Sultan Khalifa alikuwa swahiba mkubwa wa Waingereza. Pamoja na ukweli kwamba chama cha ASP kilikuwa na wapiga kura wengi zaidi lakini katika chaguzi zote hizo mbili mshindi alishindwa kupatikana kutokana na hila za wasimamizi wa uchaguzi ambao ni Waingereza. Kila walipokaribia kushinda uchaguzi uliharibiwa na kutakiwa kurudiwa ambapo katika muda wa kusubiri uchaguzi mwingine mambo mengi yalitokea ikiwa ni pamoja na baadhi wa watu kushawishiwa kukihama chama cha ASP na kuhamia vyama vingine au kuunda vyama vipya. Moja ya vyama hivyo ni kama vile ZPPP cha Mohamed Shamte ambacho kilijitoa katika ASP kwa kisingizio kwamba ASP inakumbatia zaidi Uafrika wakati kinajiita ni cha Waafrika na Washirazi.

  Baada ya chaguzi hizo mbili kushindwa kutoa mshindi Waingereza waliandaa uchaguzi mwingine Juni 1961, ambapo kwa hila zile zile ZPPP na ZNP ziliunganisha nguvu zao na kujizolea viti 13 dhidi ya viti 10 vya ASP na kupata haki ya kuunda serikali ya ndani chini ya waziri mkuu Mohamed Shamte.

  Ikumbukwe kwamba pamoja na Shamte kuwa Mwafrika kutokea Pemba lakini alikuwa akiukumbatia sana Uarabu na kwa hila akawa akitumikia maslahi ya Waarabu. Kwa hila ZNP wakamwachia uwaziri mkuu ili kuonekana hawana ubaguzi huku wenyewe wakiendesha mambo kwa mlango wa nyuma.

  Desemba 10, 1963 Waingereza walitoa uhuru kamili kwa visiwa vya Zanzibar chini ya Sultan Jamshid bin Abdulah na Serikali ya Waziri Mkuu Mohamed Shamte. Huu ukawa mwanzo wa ukoloni mwingine kwa waafrika na washirazi waliokuwa wengi katika visiwa vya Zanzibar. Uhuru kama ule wa Afrika Kusini, Zimbawe na Namibia ukatolewa Zanzibar.

  Wakati Afrika Kusini waliopatiwa uhuru walikuwa makaburu na hivyo kujizolea haki ya kuwatawala Waafrika kwa miongo kadhaa visiwani Zanzibar uhuru ukaachwa chini ya mikono ya Sultan.

  Siku sita tu baada ya kupatiwa uhuru kamili Desemba 16, 1964, Shamte akapewa nafasi ya kuhutubia katika Umoja wa Mataifa na punde akapatiwa uanachama na Kenya.

  Kwa vyovyote uhuru huu na hatua zilizofuatia zilikuwa zimepangwa na Waingereza. Ndiyo maana hata hatua za kupata uanachama katika Umoja wa Mataifa zilikwenda haraka haraka.

  Hata hivyo, kwa wananchi wengi wa Zanzibar uhuru huu haukuwa na maslahi kwao.
  Waliuona kama jinamizi jipya baada ya kuondoka lile la Waingereza. Ndipo mipango ya mapinduzi ilipopangwa chini ya mwasisi wake Kasim Hanga, Saleh Sadala, na Abdulaziz Twala.

  Kwa sababu yanayosemwa juu ya mapinduzi ni mengi hatuwezi kuandika kwa uhakika walipata msaada wapi na wapi lakini Januari 12, mwaka 1964 walifanikiwa kufanya mapinduzi na kuing’oa si tu Serikali ya Mohamed Shamte lakini hata utawala wa Sultan Jamshid.

  Pengine cha kujiuliza hapa ni kwamba kama kweli Sultan hakuwa na tatizo na Waafrika ilikuwaje yeye awe wa kwanza kuikimbia nchi wakati waliopinduliwa walikuwa Serikali ya Shamte. Na wala hakuna hata mtu mmoja katika familia ya sultan au mpambe wake aliyeshambuliwa au kukamatwa.

  Kuonyesha urafiki uliokuwapo baina ya Waingereza na usultan, mara baada ya kupinduliwa, wakati viongozi wa Serikali akiwamo Shamte mwenyewe walikamatwa baada ya kujisalimisha.

  Sultan Jamshid alipewa ulinzi na Waingereza na kupelekwa Dar es Salaam ambako alipatiwa usafiri kwenda Uingereza.
  Mara baada ya mapinduzi Uingereza hawakuipenda Serikali mpya kwa vile hawakuwa na imani nayo.

  Tangu awali hawakutaka ASP ishinde katika chaguzi na ilipoingia kwa mapinduzi juhudi zilizofuatia zilikuwa kuibana Serikali mpya hasa baada ya kuonekana imejumuisha makomredi wa chama cha UMMA ambao wao walikiona kilichojaa wanapanduzi wenye mirengo ya Kimaxist na Kikomunisti.

  Kwa mtazamo wao wakaona Zanzibar chini ya Serikali ya Mapinduzi itageuka kuwa Cuba ya Afrika, na hivyo ikawabidi wafanye mbinu zozote kutoiachia kuwa huru baada ya kushindwa majaribio ya kumrejesha Sultan.

  Pengine hizi zikawa sababu za mwanzo za muungano wa Tangayika na Zanzibar.
  Kinyume cha hapo ni lazima tuifikirie ambavyo ingekuwa hali za Zanzibar kama yasingetokea mapinduzi.

  Kwanza pasingetokea muungano kwa vile Zanzibar ingeendela kuwa chini ya utawala wa Sultan, kwa baraka za Uingereza na msaada wa Oman.

  Ikumbukwe kwamba Masultan hawa asili yao ilikuwa Oman ambapo yule kwanza Sayyid Said alikuwa akitawala Oman na Zanzibar. Basi ingekuwaje hali ya Waafrika Weusi na hata makabila mengine kama Washirazi na Wapemba kama Zanzibar ingeendelea kuwa chini ya Sultan. Kwa vyovyote ingekuwa kama Sahara Magharibi ambayo mpaka leo inatawaliwa na Moroco. Ingekuwa kama miaka 80 ya utawala wa makaburu pale Afrika Kusini, Zimbabwe na Namibia. Si kila uhuru ulijali maslahi ya walio wengi. Bado nasisitiza kuungalia upya uhuru wa Afrika.

  uhalisi@yahoo.co.uk
  0787013385/0655013385
   
 2. N

  Nonda JF-Expert Member

  #2
  May 6, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,222
  Likes Received: 1,957
  Trophy Points: 280
  Makala ni nzuri lakini sioni mantiki ya kuendelea kuangalia matukio kabla ya uhuru.
  Mwandishi angetumia muda na kipaji chake kuelezea nini kimefanyika, mafanikio na mapungufu ya nchi za kiafrika baada ya uhuru.

  Nchi hizi zipo ambazo zimetimiza miaka 50 ya uhuru. Je uhuru umeleta nini kwa wananchi wa nchi hizo?
  Bila shaka kila nchi ina makundi ya watu wa aina nyingi, rangi au makabila lakini jee hivi ndio vigezo vya kupimia maendeleo ya nchi huru?
  Au uhuru ulidhamiria kufungua ukurasa mpya na kumpa haki sawa kila mwananchi bila kujali lugha yake,rangi ya ngozi yake.dini au kabila lake?

  Je kizazi kipya kitaendelea kufundishwa haya ya ubwana na utwana badala ya kupewa elimu itakayowasaidia kuiletea maendeleo nchi yao na wao wenyewe?
  Wakati nchi nyengine wanawekeza katika elimu za sayansi na teknolojia sisi tunakumbushana udini, ukabila,weusi na weupe wa ngozi na utumwa, ubwana na utwana?

  Baada ya miaka 25 mengine bado tutakuwa tunakumbushana ubwana, utwana, usultani, uafrika, ukaburu na ulowezi?
  Huku tukiacha kuwashughulikia viongozi wabovu wa nchi zetu na kuunda taasisi za nchi,umma imara?
  Huku tukiyakumbatia makampuni ya kigeni yanayohamisha rasilimali zetu kama vile sisi tuko usingizini?

  Tuache longo longo na alfu lela ulela.
  Tanzania, Tanganyika na Zanzibar tuna viongozi ambao hawawajibiki na wanaopata tabu ni watu wote, umma wote,wananchi wote.
  Waafrika,waarabu,wahindi,weusi,weupe,manjano,wenye rangi ya udongo,wenye rangi ya mchanga.wenye vyama,wasio na vyama. waliosoma na wasiosoma.
  Ni wale wezi tu,mafisadi au wapokea rushwa ndio wenye nafuu.

  Mjasirimali halali anabanwa havuti pumzi vyema.

  Mazingira bado hayajaboreshwa kuwafanya watu wanaopenda kufuata sheria na taratibu kwa kutumia jasho lao kuweza kuyamudu maisha.
  Haya ndio yanayopaswa kuongelewa leo.
   
 3. Washawasha

  Washawasha JF-Expert Member

  #3
  May 6, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,688
  Likes Received: 410
  Trophy Points: 180
  Umesomeka mkuu
   
 4. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #4
  May 6, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Naungana na wewe Mkuu Nonda katika yale ulioyadhukuru. Isitoshe huyu mwandishi inaonekana ni wa mrengo maalum kwa kazi maalum na kwa wakati maalum. Wazanzibari wa sasa walio wengi hawawezi kumuelewa kwa sababu hayo hawana haja nayo pamoja na upotoshaji wake mwingi alioupachika katika makala yake. Labda kwa wasiojua lakini kwa sisi tulioyaona, kufananisha Zanzibar na Africa Kusini, Namibia na Zimbabwe ni upotoshaji mkubwa wa historia ya Zanzibar. Zanzibar ni kweli kulikuwa na matabaka lakini hakukuwa na ubaguzi wa namna hio unaoelezwa katika makala haya. Kuna watu wako tayari kuapa kuwa "heri ya huo ukoloni kuliko sasa".

  Maelezo kama haya ndio ambayo kwa muda mrefu yamekuwa yakitumika kuwagawa Wazanzibari ili wafarakane na ili waweze kutawalika kirahisi. Maneno kama haya ndio yalimkera hata Mwalimu Nyerere na kuwahi kumwambia Marehemu Dr. Omar Ali Juma,

  "Viongozi wetu hawana la maana kuwaeleza wananchi wao, isipokuwa Hizbu,imefanya hili na Sultani alikuwa akifanya lile na lile.Jee, jamani vijana wetu tuliokuwa nao, hivi sasa ni nani anaeijuwa Hizbu ni nani anaemjuwa Sultani? Hivi kweli hamna zaidi ya haya kuwaeleza wananchi?"

  Pamoja na kwamba mwandishi anayo haki yake ya kutoa maoni lakini ni vizuri kuwa ikiwa ni yeye au ametumwa, basi Wazanzibari wa sasa hawadanganyiki tena:


  View attachment 29398
   
 5. takashi

  takashi JF-Expert Member

  #5
  May 6, 2011
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 909
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mimi sina zaidi Mkuu...kazi umeimaliza.
   
 6. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #6
  May 6, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hapo kwenye red, mapinduzi yamefanyika 12/01/1964 na muungano 26/04/1964. Huoni kuwa ulikuwa muda mfupi sana kwa Zanzibar kukubali muungano kwa mtu au nchi ambayo hawakuwa wanamwamini? Uasisi wa muungano mimi naona umeaanza hata kabla ya mapinduzi yenyewe ndo maana kulikuwa na uhusiano wa karibu kati ya Mzee Karume na Mwl. Nyerere. Rejea stori ya usiku wa mapinduzi ya Amani Karume kwamba walichukuliwa na baba yao mpaka Dar usiku wa mapinduzi hadi kwa Mwl Nyerere.
   
 7. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #7
  May 6, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Suala la muungano ni swala litaiumiza serikali ya muungano mpaka wakubali kwa dhati kusikiliza maoni ya wananchi. Kuna ukweli ndani ya muandishi kwamba inawezekana zanzibar ingelikuwa bado iko chini ya sultani wangelikuwa mbali kuliko walivyo sasa. Perhaps tujiulize sisi waafrika tunashindwa nini?
   
 8. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #8
  May 6, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Fitna za Nyerere kwa Zanzibar zilianza zamani toka wakati wa African Association na Shirazi Association.
   
 9. M

  Mtabe JF-Expert Member

  #9
  May 6, 2011
  Joined: Sep 20, 2010
  Messages: 675
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mwandishi huyu ni mpotoshaji mkubwa na ni ktk kukata tamaa na znz sasa ameamua kuleta fitna lkn mara hii hatuwaachi tena mnyoe au musuke muungano basi.
   
 10. A

  Albimany JF-Expert Member

  #10
  May 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Muandishi nakubaliana na hii hoja ya kua uhuru uliotolewa na wakoloni haukua kamili na ndio maana Tanganyika wanaitawala Zanzibar hadi sasa chini ya mwevuli wa muungano na haya yalikua ni matakwa ya wamarekani na waengereza.

  Kuhusu sultan waengerera hawakumpenda bali ulikua muonekano wa nje tu na ndio maana alikua na uwezo wakuyazuia mapinduzi ila hakuyazuia.

  Ukweli hasa nikua MAPINDUZI na MUUNGANO yalipangwa kabla ya uhuru na wapangaji ni wamarwkani na waengereza,walimkabidhi Nyerere kazi hio na kwabahati mbaya hata karume hakujua hilo.

  Karume alishawishiwa na Nyerere akidhani ni rai nzuri yakupindua na baada ya mapinduzi alimuendea na karatasi yenye mambo ya muungano akitaka aungane nae huku akimtisha kua ukikataa utapinduliwa na Wasomi na wafuasi wa kikoministi au sultan atarudi na huku Nyerere akitishia majeshi yake kuyarudisha ndani ya siku tatu kama karume atakataa muungano

  Kwamazingira hayo hakua na budi karume(Zanzibar) kuungana na Tanganyika.
   
 11. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #11
  May 6, 2011
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Badala ya kushukuru ndio mnalalama, huko zanzibar leo kungekuwa kumejaa mikarafuu tu, sana sana the extra produce ingekuwa tende na alwa. Not to mention hile ignorance ya hali ya juu, mijitu mibantu ingejiona pure miarabu maana ingawa tuliwawahi mpaka leo bado tunatafuta dawa ya kuwaweka vichwa sawa wengi wao.
   
 12. A

  Albimany JF-Expert Member

  #12
  May 6, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 279
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  Unamainisha dawa ya kuturudishia fikra za uongo alizopandikiza Nyerere au ya kuendeleea na kuujua ukweli?

  Sisi tayari tusmeshaijua ukweli na sasa haturudi nyima tena,na tunajaribu kuwaamsha na nyinyi ndugu zetu wakitanganyika ili musidanganye huku mukiibiwa mali zenu na wajanja lakini wapi! "sikio la kufa halisikii dawa"

  Nduguzetu amkenuiiiiiii!! komboeni nchi yenu mufaidi rasilimali zenu,Tanganyika ni nchi tajiri ina kila kitu lakini mukikubali kuimbiwa nyimbo za Muungano na Uhuru mutaona tu mutakanyo shika mkia wamaendeleo kama hata huo mutaupata.
   
Loading...