Bila kutenganisha Uwaziri na Ubunge Maendeleo tutaendelea kuyaona Kwenye Sinema tu!

Nitamuomba mbunge wangu wa jimbo la Kawe mh Gwajima apeleke mswada Binafsi

Yafanyike marekebisho Madogo ya Katiba ya JMT ili kuondoa kipengele kinacholazimisha Waziri kuwa mbunge

Kwamba Waziri ateuliwe na Rais wa JMT kisha akathibitishwe na Bunge

Naomba mniunge mkono

Mlale Unono!
Hata shujaa wako hakuleta maendeleo??
 
Nakuunga mkono kwa hili.
Pia na viongozi wa serikali kuanzia mwenyekiti wa serikali ya mtaa mpaka Rais wa JMT nao waweze kushitakiwa wakiwa uongozini au wakitoka.
 
Nitamuomba mbunge wangu wa jimbo la Kawe mh Gwajima apeleke mswada Binafsi

Yafanyike marekebisho Madogo ya Katiba ya JMT ili kuondoa kipengele kinacholazimisha Waziri kuwa mbunge

Kwamba Waziri ateuliwe na Rais wa JMT kisha akathibitishwe na Bunge

Naomba mniunge mkono

Mlale Unono!
Acha uongo wewe mbunge wako ni yule demu wa Iringa mjini!
 
Mozambique pesa yao ilipanda baada ya kuweka sheria ya wabunge wasiwe mawazili!
 
Bila kuweka wazi wasipotimiza wajibu watawajibishwa au kuvuliwa madaraka, wakifanya ufisadi kupelekwa mahakamani. Itakuwa vigumu kupata viongozi waadilifu.

Kila waziri anakuwa amewekewa malengo kila miezi mitatu anaitwa na kuhojiwa bungeni na kamati ya uwajibikaji kwa viongozi wa umma. Kama hajatimiza malengo bila sababu ya msingi anapigiwa kura ya kuendelea na kazi au kufutwa kazi.
 
Point of correction:. Bila kuifuta ccm ktk nchi hii maendeleo tutaendelea kuyaona kwenye TV tu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom