Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,242
Wakati mwingine huwa napitia Ilani za uchaguzi za CHADEMA za 2005 na 2010 nakujiuliza ni kwa nini watanzania hawakuichagua kuongoza nchi kwenye chaguzi hizo zilizopita. CHADEMA linapokuja swala la mfumo wa utawala wana hoja nzuri sana hata kama wakati mwingine haziko kwenye mpangilio mzuri sana kama alivyochambua Mzee Mwanakijij kwenye bandiko lake "CHADEMA 2010"
Matatizo mengi tuliyonayo watu wanayahusisha na ufujaji wa fedha na mali ya umma,lakini kwa mtazamo wangu tatizo ni aina ya mfumo wa utawala tunaoufuata. Ufujaji kiholela wa mali za umma unatokea kwa sababu hakuna mwananchi wa kawaida ambaye ana njia (access) ya moja kwa moja kwenye kusimamia utendaji wa kila siku wa serikali.
Kama Bunge ambalo ni Mhimili mmojawapo wa dola haliruhusiwi kuona mikataba ambayo serikali imeingia na makampuni kwenye shughuli mbali mbali za uzalishaji mali na uwekezaji, Kwa mwananchi wa kawaida itakuwaje. CHADEMA wanapendekeza Tanzania iongozwe kwa mfumo wa Majimbo na viongozi wa majimbo wachaguliwe na wananchi na siyo kuteuliwa na mtu au chombo chochote kile.
Hata mgogoro wa Tanganyika na Zanzibar utakwisha kwani Pemba litakuwa ni Jimbo na Unguja nalo ni Jimbo linalojitegemea. Tatizo wanasiasa wa Tanzania hawaamini katika kupeleka maradaka kwa wananchi.