Bila kuchuja wanaojiunga kidato cha kwanza, Shule za serikali zitaendelea kufanya vibaya

shikulaushinye

JF-Expert Member
Aug 29, 2014
828
456
Hivi karibuni kumekuwapo lawama kuwa elimu ya Tanzania inashuka kwa kasi hasa kwa kulinganisha matokeo ya miaka ya nyuma, lakini wengi tumesahau kama huko nyuma waliokuwa wanakwenda kujiunga kidato cha kwanza walikuwa wamefanya vizuri sana. Mfano katika mikoa kadhaa nafasi za kiadto cha kwanza zilikuwa 300, hivyo kugawanywa kwa wilaya si chini ya wanafunzi 50-80, hivyo walichaguliwa wale waliofanya vizuri sana kati ya waliofauru mtihani. mfano mtihani ulikuwa ni masomo matatu; LUGHA (English, Kiswahili), MAARIFA (Geo, Hist, siasa, sayansi, na nk) na HISABATI. Kila mtihani ulibeba marks 50. hivyo wengi waliokuwa wanachaguliwa walikuwa lazima wapate kuanzia marks 140-150. Hawa walikuwa very pure. lakini sasa kuna total Marks 500 ikiwa ni KISWAHILI, ENGLISH, MAARIFA, HISABATI, SAYANSI NA HISABATI, kwa sasa wanaochaguliwa ni mpaka marks 100 kati ya 500 huku mitihani ikiwa kuchagua, wengine wanafaulu hata wakiwa ahawajui kusoma wala kuandika.

SHULE BINAFSI:
Shule binafsi hufanya mchujo wa hali ya juu, kwanza hufanya screening ya wale wanaopata nafasi za juu shule wanazotoka harafu wanawapa mitihani mtihani mwingine, ambao hufanya second screening na kupata wanafunzi bora saana. mfano shule za Marian boys na Girls hupokea maombi kati ya 3000-4000 kila mwaka then huchagua 100 tu kila darasa, hapo wanchokifanya ni kusahihisha mitihani ya wale best candidates tu let say 500 wanaoshika nafasi za kwanza shuleni kwao, then huchagua 100 walifanya mtihani wa shule. Shule za serikali lini zinaweza kushindana na shule binafsi? me naona matokeo ya shule binafsi yawe tofauti na shule za serikali.
 
Na jana wamepeleka season 4.Mid term zinaanza na wengine ndo wanaripoti.Full burdan.
 
Ukumbuke kuna UCHANGIAJI elimu eee, ile bure ilikuwa janja tu ya kuwapigisha watu vigelegele.
 
Hoja yako ni ya msingi sana, haiwezekani majority ya wanaoingia kidato cha kwanza waingie na maksi za chini na wengine hawajui hata kusoma vizuri halafu tutarajie miujiza kwenye matokeo ya mwisho!
 
Hoja yako ni ya msingi lakini Darasa la Saba total mark in 250, kila mtihani unachangia 50% na sio 100% kama Kidato cha Nne na Sita. Na mwanafunzi kufaulu ni yule amabae amepata alama 100 out of 250. Nashauri next time ufanya utafiti kidogo kabla ya kuandika kitu kuhusu elimu.
 
Hoja yako ni ya msingi lakini Darasa la Saba total mark in 250, kila mtihani unachangia 50% na sio 100% kama Kidato cha Nne na Sita. Na mwanafunzi kufaulu ni yule amabae amepata alama 100 out of 250. Nashauri next time ufanya utafiti kidogo kabla ya kuandika kitu kuhusu elimu.

Thanks kwa machango ni niombe radhi kwa kukosea takwimu lakini siyo kweli sijafanya utafiti hata mdogo, kukosea ktk data haimaanishi research yote imekosewa, nilichokiandika ndiyo ukweli wenyewe. Kwa hoja yako angalia uwiano wa ufaulu miaka ya nyuma waliokuwa wakifaulu kwenda secondary walikuwa wanaenda kwa marks si chini ya 120 kwenda juu kutegemea mkoa una shule ngapi za secondary, kwa sasa huko vijijini wanachukua hadi alama 70 out of 250 ili kujaza madarasa ya shule za kata. unategemea shule za serikali zishindane na shule za binfasi? Mwaka jana serikali imezuia kufukuzwa kwa wanafunzi wanaoshindwa kufikia alama za kupanda darasa kwa mfano SHULE ZA MARIAN (BOY&GIRLS) ili mwanafunzi apande darasa anataliwa apate wastani wa 80% shule nyingine nyingi za private pass mark ni 50% <, pamoja na kuzuia kufukuzwa kwa sasa shule binafsi zinamrudisha darasa mzazi utamhamisha mwenyewe coz utalipa ada mara ngapi kwa darasa moja, pia mtoto ana athirika ki saikolojia kiasi gani? wenzake wanapanda yeye anarudi harafu anaendelea kusoma hapo hapo unategemea nini?
 
Back
Top Bottom