Wandugu naomba mnivumilie lakini nina hoja ya kuijadili. Kwa muda mrefu tumekuwa tukisikia kashfa na tuhuma mbali mbali dhidi ya viongozi wetu na hata wafanya biashara maarufu nchini wakihusishwa na tuhuma au shutuma mbalimbali za kukosa uadilifu na uhujumu uchumi. Kupitia taarifa hizi, wako ambao wamelazimika kuwajibika na wachache kufikishwa mahakamani. Kupitia taarifa hizi, tumeweza hata sisi kutoa michango yetu kupitia kwenye majukwaa mbalimbali likiwemo hili maarufu la JF. Lakini tumewahi kujiuliza uhuru huu wa kuhoji, kushutumu na kushambulia maovu umetokana na nini na umeanza lini.
Kwa ufahamu wangu hli hii imejitokeza kwa upana huu tunaoufurahia baada ya serikali ya awamu ya nne kuingia madarakani na ni matunda ya juhudi binafsi za JK. Katika awamu iliyopita haya yanayojitokeza leo yalikuwepo, tena kwa kiasi cha kutisha lakini tuliyajua kwa undani na ufasaha baada ya awamu hiyo kuondoka. Katika tawala za kidhalimu huko kwa wenzetu, uhuru huu kwa vyombo vya habari na watu binafsi ni ndoto na hata hapa tumeshuhudia watu wakiadhibiwa kiasi hata cha kunyang'anywa uraia kwa kusema kile walichoamini kwamba ni sahihi. Huko nje hali ni mbaya zaidi kwani wapo wanaopoteza maisha wakiusotoea uhuru huu. Hatutaki hilo litokee hapa na nina uhakika halitatokea maana kama ni kutokea lingeshatokea kwani uhuru huo umefikia hata kushambulia maisha binafsi ya rais na familia yake lakini mambo shwari tu.
Mimi ninavyoamini hili ni matunda ya uvumilivu binafsi wa JK na ni vizuri katika hili tumpe sifa yake, maana kama inafikia kwamba hata mafisadi nao wanapata fursa ya kuongea wakati sasa hivi walitakiwa kuwa wameshalala kule segerea au ukonga, basi hakuna fursa kubwa kuliko hiyo. Waswahili wanasema ukimsifia baba yako kwamba anakimbia sana basi umsifie na yule aliyemkimbiza! Naomba kutoa hoja na samahani kwa wale watakaokwazika.

Samahani kwa jibu langu hili: Bila ya Jk nadhani nchi ingekuwa na matumaini makubwa ya kuwapo kwa amani ya kudumu(siyo ya sasa inayopigiwa debe) maana viongozi wangewajibishwa vilivyo -- mafisadi wangepelekwa wanakostahili -- jela -- na nchi ingeokoa mapesa mengi yanayoibiwa hivo serikali kuweza kutoa huduma vizuri kwa wananchi.
Mimi nawashangaa wale wote wanaompa Kikwete sifa za kufungua nafasi ya demokrasia. Hiyo nafasi Kikwete aliikuta. Angalia jinsi alivyoyatumia magazeti kujipandisha chati na kuwaharibia wote wale aliofikiria kuwa ni maadui/washindani wake. Mtu kama huyu asingeweza kugeuka na kuanza kufuta nafasi aliyoikuta na ambayo ameitumia kwa manufaa.Ni kweli kwamba kuna watu wana-enjoy uhuru ambao hauwastahili kutokana na matendo yao kwa wana wa nchi hii. Lakini hili ni tatizo la karibu nchi zote za kusini mwa jangwa la sahara - kupambana na mnyama anayeitwa impunity ni suala ambalo bado halijawekwa kwenye sehemu inayostahili na hili ni changamoto pia kwa JK, lakini hilo ni somo kwa siku nyingine. Kwa leo lililo wazi ni kwamba score card ya mkubwa huyu kwenye kufungua democratic space na kutufanya tujisikie tuke kwenye taifa huru, iko juu. A pat on the back mkuu!