Naona huu wimbo wa UDINI....UDUNI....umeendelea kushika kasi .....tena naona kasi yake inazidi kuwa kubwa ziadi. CDM kinasemekana kuwa ni cha kikristo....CUF kinaonekana kuwa ni cha kiislamu....sijasikia TLP, NCCR, TADEA, UDP n.k. Lakini kikubwa sijasikia CCM ni chama cha mlengo gani....au chenyewe ndio hakina dini.....halafu kibaya zaidi aliyeanzisha wimbo wa UDINI ni KIKWETE....sasa mbona tunasahau kusema CCM ni chama cha dini gani....???
Baada ya kuona kuwa mtaji wa Kasi zaidi, Ari zaidi and Nguvu zaidi haimpi ushindi, Kikwete aliasisi UDINI ili kukinyima kura Chadema na Cuf. Mtu anayesema wenzake ni wadini, yeye ndiye MDINI MKUU, ndiyo maana amekuwa na upeo mkubwa wa kuwatambua wengine kuwa ni WADINI. Kwa maana nyingine kubwa na inayoeleweka, KIKWETE ndiyo MDINI KUU. Kama JK ni mdini, CCM inajinusuru vipi na udini? Na tunasemaje kama mwenyekiti wa chama ni mdini, tena MUISLAMU, Tunapata utata gani kusema kuwa CCM ni chama cha KIISLAMU? Au tuanze kuchambua team yake ya kampeni mwaka 2010? au tuanze kuangalia watu wa dini yake aliowapa madaraka kwa dini yake? au tuhesabu wakuu wa mikoa na wilaya, makatibu wa ccm mkoa na wilaya, wakurugenzi wa majiji, halmashari za mji na wilaya na vingine vingi? Si vema kuyafanya yote haya kwa sababu siku yakitokea ya kutokea, tutaathirika wote kwa kiwango sawa, hakutakuwa na mwanaCCM wala CUF au hata mwana CHADEMA ambaye atabaki salama, dhambi hii ya ubaguzi itatutafuna sote.
NINI FUFANYE......
Kikwete na CCM yake watapita....Mbowe na CDM yake watapita.....Lipumba na CUF watapita.....NCCR na mbatia itapita....TLP na Mrema watapita....LAKINI TANZANIA NA WATANZANIA wataendelea kuwepo hadi Mungu atakaposema ni mwisho wa kila kitu hapa duniani. Kufikiri mambo ya siasa kwa mtazamo wa dini fulani, ni kuishia kisera na maono ya kuongoza nchi...nafikiri wote mnaona CCM ilipotufikisha na Kikwete wake na udini anaousema. Nafikiri mnaona sera za CCM ya leo, juzi tumezisikia ARUMERU, hapo ndipo CCM ilipofika. Kuendelea na chama hiki kikiwa na viongozi aina ya akina Sitta, Lowasa, Vuai Nohodha, Hussein Mwinyi, Bernard Membe, Mwakyembe, na wengine wengi kutoka CCM mwaka 2015 ni kuliangamiza Taifa na kuzidi kuutambulisha UMBUMBUMBU WETU KTK anga za KIMATAIFA NA MAJIRANI ZETU. Wote tunanunua katika maduka yale yale, wote watoto wetu wanasoma Saint Kayumba, wote tunaishi nyumba zinazofanana, kifupi wote tunaishi maisha yanayofanana, ukiwatoa wachache ambao wanafaidi keki ya Taifa....sasa mtu maskini kama mimi anapata wapi ujasiri wa kushabikia CCM ilihali yote haya yamesababishwa na CCM?
TAIFA hil litajengwa na watanzania wote bila kujali itikadi zetu za dini na vyama. Tusipounganisha nguvu zetu kama watanzania, tutaendelea kuyasikia maendeleo kwenye nchi za wenzetu....Kama chama Tawala bado kinatoa ahadi hadi leo....maana yake hakuna ambacho wamefanya miaka yote ya uhuru....maana ya ahadi ni kupanga kufanya katika wakati ujao...CCM bado wanaahidi maji, bado wanaahidi umeme, bado waaahidi maisha bora, sasa wamefanya nini miaka yote ya uhuru....?
Kazi kweli, ndiyo maana wengine TUNAVUMILIA KUWA WATANZANIA na kamwe HATUJIVUNII KUWA WATANZNIA. Utajivunia nini katika nchi ya tatu kwa kukopa duniani ilihali kila siku wazungu wanaondoka na tani nyingi za dhahabu, almasi, gesi, magogo na sasa hadi wanyama.....KWELI KUSHABIKIA CCM LAZIME UWE NA MTINDIO WA UBONGO...