diana chumbikino
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 428
- 368
WAKALA wa Barabara (TANROADS) mkoani Pwani unatarajia kutumia Sh bilioni 25.4 kwa ajili ya kufanya matengenezo ya barabara zake mbalimbali. Hayo yamesemwa mjini Kibaha na mhandisi wa wakala huo Zuhura Aman wakati wa kikao cha bodi ya barabara cha mkoani humo na kusema fedha hizo ni za bajeti ya mwaka 2018/2019.
Amesema hadi kukia Septemba 2018 zimepokelewa Sh milioni 958.7 kwa ajili ya matengenezo ya barabara hizo. "Katika kipindi hicho shilingi bilioni mbili zimetumika kufanya matengenezo mbalimbali kwenye barabara kuu," amesema. Alisema kazi ya matengenezo ilichelewa kuanza kutokana na taratibu za manunuzi na uhakiki wa mikataba ambayo huchukua muda mrefu kukamilika, hasa mikataba inayohakikiwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali.
"Mkoa umepanga kufanya miradi ya maendeleo ya barabara zenye urefu wa kilometa 32.5 zenye thamani ya Shilingi bilioni 2.3," alisema. Aidha alisema kwenye miradi hiyo ya maendeleo Sh bilioni 1.3 ni bajeti ambapo Sh milioni 969 ni kutoka mfuko wa barabara. Vilevile bilioni 7.5 ni kutoka serikali zitafanya ukarabati kwa kiwango cha changarawe na udongo. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema ili kuboresha barabara za mkoa huo watendaji wanapaswa kuwa waadilifu. Ndikilo alisema kutokana na mkoa kuwa na viwanda vingi uboreshaji wa miundombinu ya barabara utasaidia kuinua uchumi wa wananchi na taifa