Big Match: Simba 0 - 1 Azam, Lamba lamba waondoka na mkia wa mnyama

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,015
114,360
Wakuu Leo kama mnavyofahamu Mnyama wa Msitu Mnene Simba SC anaenda kukipiga na Wana Rambaramba katika mechi yake ya 20 ya Ligi Kuu ya Vodacom. Mchezo utachezwa uwanja wa Taifa. Mechi ni saa 10 jioni na itarushwa live na Azam TV na kutangaza na TBC Taifa.

Wana Simba tujae kwa wingi huku tukiwa tumetoka KiSimba kuja kuishangilia timu yetu.
simbaa.png


azam.jpeg


Swali la Kizushi
Kwa kuwa rufaa ya Polisi Dar ilikuwa-engineered na Yanga, Je na leo Yanga mtakuja macho kodo kuangalia mapungufu ya kuikatia mechi hii rufaaa?

------------
Dk 90+5, Mpira umekwiiiiiiiishaaaaaaaa. Azam wanaondoka kifua mbele kwa kuchukua zote pointi tatu.

Dk 90+4, Kipa Aishi Manula anaucheza mpira wa kichwa kiustadi na kuwa kona, Simba wanapiga kona bila kuzaa matunda.

Dk90 +3, Mashabiki wa Simba wanakata tamaa na kuanza kuondoka ndani ya uwanja.

Dk 90+1, Simba wanafanya shambulizo moja matata ila mlinda mlango wa Azamu, Aishi Manula anarukwa kwa mbwembwe na kuutoa, inakuwa kona.

Dk 90, Azam wako mbele na wanajitahidi ili kuondoka na point muhimu. Dakika za nyongeza ni 4

DK 88, Simba wanapata mpira wa adhabu unapigwa na Kichuya ila Mavugo anajitwisha ndoo vibaya na mpira unakuwa goal kick.

Dk 85, ya mchezo Simba washarambishwa Ice cream moja.

Dk 83, Azam wanafanya mabadiliko na kumtoa Bocco na kumuingia Kheri

Dk 82, Mwamuzi anampa kadi ya njano Aishi Manula kwa kupoteza muda.

Dk 80, Matokea yanasomeka Simba 0 na Azam FC 1.

Dk 79, Simba wanapata kona lakini mchezaji wa Azam anauondosha. Azam wanafanya shambulizi la kustukiza lakini Yahya anapiga shuti linatoka nje.

Dk 77, Azam wanafanya mabadiliko, anatoka Yahya Mudathir kuchukua nafasi ya Stephen Kingue.

Dk 74, Mchezaji wa Azam Stephane Kingue apiga mpira vibaya na kuanguka chini, mwamuzi anasimamisha mpira na kuita watu wa huduma ya kwanza. Bila shaka hatoweza kuendelea na mchezo.

Dk 71, Yahya wa Azam FC anapiga shuti kali ila linakwenda nje ya lango na kuwa goal kick

DK 70,
Nahodha John Bocco anaipatia Azam goli la kuongoza

DK 66 - 68,
Simba wanafanya mashambulizi ya mfululizo lakini umakini wa Azam unawasaidia kuondosha mipira yote ya hatari langoni kwao.

DK 65,
Mavugo anaingia kuchukua nafasi ya Liuzio

Dk 62,
Yahaya Mohammed anaingia kwa upande wa Azam FC kuchukua nafasi ya Singano

Dk 59, Ibrahim Ajibu anaingia kuchukua nafasi ya Xavier Bokungu

Dk 57, Xavier Bokungu anarejea uwanjani baada ya kupata matibabu.

Dk 55, Mpira unaendelea baada ya kusimama kwa takribani dakika 4, Bokungu kutolewa nje, Ajibu anajiandaa kuchukua nafasi ya Bukungu.

Dk 52, Boko katika kuwania mpira na kupiga shuti lakini anamuangusha Bokungu, mpira umesimama kwa muda ili kumpa huduma ya kwanza.

Dk 48,
Simba wanafanya mashambulizi mfululizo.

Dk 47, Simba wanakosa goli, kazi nzuri ya Aishi Manula kudaka shuti la Liuzio

Dk 46, Mpira umeanza, Shiza Kichuya anaingia kuchukua nafasi ya Mnyate.

Dk 45 +2, Mpira ni mapumziko, Sio Simba wala Azam ambayo imeona lango la mwenzake

Dk 45+, Dakika mbili za nyongeza kipindi cha kwanza.

Dk 43, Ramadhan Singano anapata kadi ya njano.

Dk 40, Matokeo bado ni 0 - 0

Dk 33, Erasto Nyoni analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Pastory Athanas, hii ni kadi ya kwanza ya njano ya mchezo huu

Dk 30, Mpaka sasa hakuna timu iliyoziona nyavu za mpinzani wake.

Dk 23, Yakubu anautoa mpira nje na kuwa kona ya kwanza ya mchezo ambao wanaipata Simba. Inachongwa hapa Azam FC wanaokoa

Dk 13, Bocco anajaribu hapa katika lango la Simba lakini Agyei anakuwa makini na kuudaka mpira huo

Dk 6, Zimbwe wa Simba anatolewa nje baada ya kugongana na Mhundi, anapatiwa matibabu

Dk 1, Mechi imeanza taratibu kabisa huku kila timu ikionekana inataka kuusoma mpira au mbinu za mwenzake kabla ya kuzipambanua zake
 
Back
Top Bottom