Mkuu watu wanapojadili mambo ya maana ambayo watu wamefariki usilete utani wa kipuuzi. Kuna jukwaa la vichekesho huu upuuzi wako peleka kule utapata wachangiaji.
Ndugu yangu akili ndogo inalitazama hili jambo kama la utani...what is happening in the US right now is much greater than two individuals, greater than Donald Trump and definitely greater than Joe Biden. The US is an experiment, the world experiment and
if the US was to collapse, the whole world would be in great danger.
Watu kama
Adolf Hitler hawakutokea hivi hivi, waliwezeshwa na watu wanaoweka matumaini yao kwa individuals badala ya
society as a whole. Historia ipo kutukumbusha, kutuonya na kutufundisha lakini katika kila jamii utakuta watu wasioipa historia haki yake katika kuelimisha na kutuepusha kurudia makosa ya nyuma.
Watu kama Putin wa Urusi hawakuota tu kama uyoga, watu kama Rais wa China hawakuzuka tu ghafla, hapana, jamii ilihusika katika kuwaasisi, kuwalea na kuwajenga hadi wakakua na kupata nguvu walizo nazo. Hiyo ndio sababu taifa kama Marekani ambayo wakazi wake wengi walizikimbia nchi zao za asili inaitwa
the experiment.
Kama Wamarekani weusi ndio wangepanga kuvamia jengo kubwa kuliko yote nchini humo na ulimwengu mzima ambalo ndilo makazi ya serikali ya Marekani na alama ya taifa, kama Waislaam ndio wangepanga kuvamia jengo hilo au kama watetezi wa demokrasia ndio wangethubutu, leo hii vilio vingetanda duniani kote.
Badala yake, si vilio vinasikika Urusi, si vilio vinasikika China, si vilio vinasikika Korea Kaskazini, si vilio vinasikika Iran...ni vicheko na dhihaka. Marekani inachekwa kwa sababu ya wabaguzi wachache wanaochukia demokrasia iliyoweka mamlaka yote mikononi mwa wananchi na si kiongozi wa wabaguzi wa rangi kama ilivyokuwa Afrika Kusini.
Bendera iliyopeperushwa ndani ya jengo hilo inayoitwa
Confederate Flag ni bendera ya waliopinga umoja wa taifa la Marekani uliotaka kuwapa binadamu wote
uhuru, haki na usawa. Walianzisha vita wakipigana na watu waliokuwa wakitetea haki hizo lakini walishindwa. Walikuwa wakitetea utumwa kwa watu weusi uendelee.
Acheni utani ndugu zangu, fuateni kwa makini yanayojiri kwani mnayo mengi ya kujifunza katika sakata hili. Hii si mara ya kwanza Marekani kupitia kipindi kama hiki na nina hakika haitakuwa mara ya mwisho ila mwisho wa siku
the experiment will survive and live on! Hail to liberty in the land of the brave and the free!