Biden ni mpenda vita kuliko Trump

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
8,991
17,888
Mgombea wa uchaguzi wa Marekani: Biden ni mpenda vita kuliko Trump

Nov 17, 2020 12:21 UTC

Mmoja wa wagombea wa kiti cha Seneti ya Marekani katika uchaguzi wa mwaka huu wa 2020 amesema kuwa siasa za nje za Joe Biden, aliyeshinda urais wa nchi hiyo katika uchaguzi wa hivi karibuni ni za hujuma na kupenda vita zaidi kumliko mpinzani wake Donald Trump, anayeondoka madarakani.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Sputnik, Ibra Taher mgombea wa kiti cha Seneti ya Marekani kwa tiketi ya chama cha kijani cha Marekani amesema kwamba siasa za nje za Joe Biden aliyetangazwa na vyombo vya habari kuwa mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni nchini humo atakuwa na siasa kali na za hujuma kuliko za Trump. Amesema kwamba Wademokrat kiujumla huwa wanatekeleza siasa za nje za kiuhasama na kihujuma dhidi ya nchi nyingine na hasa Russia.

Katika uwanja huo ameashiria siasa za Wademokrat kuhusu matukio mbalimbali ya kimataifa na hasa kuhusiana na suala la Ukraine mwaka 2014 na madai yao kwamba Russia iliingilia kati na kubadilisha matokeo ya uchaguzi wa mwaka 2016 kwa maslahi ya rais aliyekuwa madarakani wakati huo.

Donald Trump

Hii ni katika hali ambayo Russia ilikanusha vibikali madai hayo ya Wademokrat wa Marekani na kusisitiza kuwa haikuwa na sababu yoyote ya kuingilia uchaguzi huo uliofanyika kwa misingi ya demokrasia.
 
Mnamaanisha wale wafanyakaz kwenye viwanda vya silaha na wanasayans wanaoendeleza tafit za silaha watafute shughul nyingine za kufanya???
 
Back
Top Bottom