Song of Solomon
JF-Expert Member
- Aug 5, 2021
- 2,751
- 5,623
RAIS wa Marekani Joe Biden amewahakikishia wabunge wa Marekani kwamba wanajeshi wa taifa hilo hawatashiriki katika vita vya Ukraine, na hakuna hata mwanajeshi hata mmoja atakayetumwa katika nchi hiyo ya Ulaya Mashariki kupigana na Jeshi la Urusi.
Akihutubia Bunge la Congress Jumanne, Biden alisisitiza kuwa "vikosi vya Marekani havishiriki na havitashiriki katika mzozo na vikosi vya Urusi nchini Ukraine."
Hata hivyo, kiongozi huyo amesema, wanajeshi wa Marekani, vikosi vya anga na meli za kivita zinatumwa mahali pengine ili "kutetea washirika wetu wa NATO ikiwa Putin ataamua kuendeleza (mapambano) katika nchi za magharibi."
Biden alizitaja nchi ambazo Marekani inaimarisha jeshi lake kuwa ni Poland, Romania, Latvia, Lithuania na Estonia.
Rais wa Marekani aliendelea kuionya Moscow kwamba, kwa kuzingatia kanuni ya 5 ya NATO, Washington itaingjia kuwaokoa washirika wake wa NATO ikiwa Urusi itawalenga, na kuongeza kwamba kambi ya kijeshi iko tayari "kulinda kila inchi ya eneo la nchi za NATO na nguvu kamili ya mamlaka yetu ya pamoja."