Bibi wa miaka 80 Abakwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bibi wa miaka 80 Abakwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mama Nim, Feb 10, 2010.

 1. Mama Nim

  Mama Nim Senior Member

  #1
  Feb 10, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  AJUZA wa miaka 80, mkazi wa kitongoji cha Kiwangwa wilayani Bagamoyo amebakwa na kijana mwenye umri wa miaka 35 na kusababishiwa majeraha makali katika sehemu zake za siri.

  Tukio hilo lilitokea saa 8:00 usiku wa kuamkia jana na kwamba kijana aliyehusika na tukio hilo (jina linahifadhiwa), lakini ni mkulima wa Kiwangwa wilayani humu.

  Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Absalom Mwakyoma alidhibitisha tukio hilo na kusema kuwa bibi kizee huyo alibakwa wakati akiwa amelala nyumbani kwake ambapo mtuhumiwa alitumia mbinu ya kuvunja mlango usiku huo na kuingia katika chumba cha ajuza huyo kisha kumbaka kwa nguvu.

  Mwakyoma alisema tukio hilo linasikitisha na kutia aibu vijana kutokana na ukweli kwamba bibi huyo anaishi kwa shida na taabu nyingi.

  "Inavyoonekana huyo jamaa, alikuwa anamvizia ajuza kwa muda mrefu na nadhani alikuwa akimfuatilia kwa karibu ili kujua mwenendo mzima,alipobaini analala mwenyewe ndipo alipotumia mbinu ya kumvizia muda huo na kuvunja mlango na hatimaye kumbaka hata imani za kishirikina zinaweza kuwa ni chanzo,"alisema Mwakyoma.

  Alisema mlalamikaji anaishi mwenyewe kwenye nyumba hiyo na kwamba tayari mtuhumiwa alikamatwa na anaratajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote mara uchunguzi utakapokamilika, mlalamikaji anaendelea vizuri.


  Jamani aibu gani hii?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...