Bibi wa miaka 67 asimulia alivyosifiwa kuwa na mapaja mazuri kisha kubakwa

Sildenafil Citrate

JF-Expert Member
Jan 29, 2021
575
2,559
Kijana mwenye umri wa miaka 48 mkazi wa kijiji cha Mwika wilaya ya Moshi, Stanley Urio aliyemsifia bibi wa miaka 67 kuwa ana mapaja mazuri kabla ya kumpiga mtama na kumbaka, amehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

Hukumu hiyo imetolewa leo Septemba 30, 2022 na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi, Elibariki Philly, akisema ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka wakiongozwa na wakili Nitike Emanuel umethibitisha shitaka hilo.

Ushahidi ukiwemo wa bibi aliyefanyiwa ukatili huo Aprili 30,2021 huko Mwika, ulionyesha kuwa siku hiyo saa 1:45 usiku, bibi huyo alitoka nyumbani kwake akiwa na tochi akielekea kanisani ambalo lipo jirani.

Kwa mujibu wa ushahidi huo, akiwa njiani alipita dukani kwa Mromboo ili kununua betri ndipo alipomuona mshitakiwa na aliweza kumtambua vizuri kwa mwanga wa taa uliokuwepo dukani alipokamilisha mahitaji aliendelea na safari.

Hata hivyo, akiwa njiani akiendelea na safari, mshitakiwa alianza kumfuata kwa nyuma lakini hakuwa na wasiwasi kwani mshitakiwa ni mkazi wa maeneo hayo na anamfahamu vizuri hivyo akaendelea na safari kuelekea kanisani.

Kulingana na ushahidi wa bibi huyo, alipokaribia maeneo ya kanisani eneo la Shokoni, mshitakiwa alianza kumsifia kuwa ana mapaja mazuri na kumuomba amkubalie wafanye mapenzi kwa ahadi ya kumpa Sh20,000.

Bibi huyo alikataa na ndipo mshitakiwa alimpiga ngwala na bibi huyo akadondoka chini na mshitakiwa alimfuata na kumtoa nguo na kumbaka kitendo kilichosababisha bibi huyo kupoteza fahamu na majeraha pia.

Ushahidi wa daktari ulitolewa mahakamani ulithibitisha kuwa bibi huyo alikuwa ameingilia kimwili na kusababishiwa majeraha.

Katika utetezi wake, mshitakiwa alijitetea kuwa siku ya tukio ni kweli alikuwepo dukani hapo kuanzia saa moja usiku akinywa bia aina ya Kilimanjaro, akiwa na mke wake pamoja na muuza duka na hakuwahi kwenda huko Shokoni.

Hata hivyo, Hakimu Philly aliukataa utetezi huo wa kutokuwepo eneo la tukio (alibi) akisema kisheria alipaswa kuutoa mapema kabla ya kesi kuanza kusikilizwa ili upande wa mashtaka uweze kujiandaa na kuleta mashahidi kupangua hilo.

Hakimu Philly alisema hawezi kuupa uzito ushahidi huo wa utetezi hasa ikizingatiwa kuwa bibi huyo alieleza ushahidi wake vizuri na usio acha shaka kuwa ni mshitakiwa na si mtu mwingine aliyembaka na kumsababishia maumivu.

Kutokana na uzito wa ushahidi, alimhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.

Chanzo: Mwananchi
 
Yaani hapakuwa na ushahidi wa kipimo cha manii hakimu ametumia ushahidi wa bibi peke yake?

Nilitegemea alibi ikataliwe kwa ushahidi wa kidaktari badala ya logic ya hakimu.

Halafu miaka 48 ni kijana? Anyway, kama alitenda kosa anastahili adhabu kali.
 
kajala-pic-data.jpg
 
Yaani hapakuwa na ushahidi wa kipimo cha manii hakimu ametumia ushahidi wa bibi peke yake?

Nilitegemea alibi ikataliwe kwa ushahidi wa kidaktari badala ya logic ya hakimu.

Halafu miaka 48 ni kijana? Anyway, kama alitenda kosa anastahili adhabu kali.
Mimi pia nimejiuliza swali kama hilo. Nilitegemea manii zipimwe DNA kisha na huyo jamaa apimwe DNA ili kusiwe na shaka kabisa katika kumtia hatiani.
 
Back
Top Bottom