Bibi wa lulu atua kortini

Gumzo

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
211
7
HUKU kesi ya kushukiwa kuhusika na mauaji ya marehemu Steven Kanumba ikiendelea kumkabili nyota wa filamu za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’, bibi yake na msanii huyo alitinga kortini kusikiliza kesi ya mjukuu wake.
Bibi huyo ambaye alitajwa kwa jina moja la Elizabeth, ilielezwa ni mama mzazi wa mama wa msanii huyo Lucresia Karugila, alitinga katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, juzi, Jumatatu, jijini Dar es Salaam akiwa ameongozana na mwanaye (mama’ke Lulu) na ndugu wengine.
Shauri hilo lilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kusikiliza uamuzi wa kupelekwa Mahakama ya Rufaa, kama mawakili upande wa serikali walivyoomba katika kesi hiyo.
“Huyu ni bibi yake Lulu, amekuja kutokea kijijini Bukoba. Ni mama yangu mzazi. Ameguswa na jambo hili na ameona ni vyema aje kumuona mjukuu wake,” alisema mama Lulu.
Kesi hiyo imehairishwa na Msajili wa Mahakama hiyo, Amiri Msumi, mpaka Agosti 20 mwaka huu kwa vile jaji aliyetakiwa kusikiliza kesi hiyo Twalib Fauz hakufika mahakamani hapo kwa kile kilichoelezwa alikuwa na dharura

KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA GUMZO LA JIJI
 
Back
Top Bottom