Bibi harusi mtarajiwa kakimbia, jirani kanipa bintie ili harusi iendelee

JFK wabongo

JF-Expert Member
Aug 11, 2015
3,887
3,195
Ni tukio la kufedhehesha ila ndo hivyo maisha lazima yaendelee. Mchumba wangu kumpata mzungu kaondoka naye kwenda Ulaya licha ya kuwa nilishalipa mahari. Ilikuwa ngumu kuzoea hiyo hali ila ndo hivyo tena.

Binafsi nilishaamua kutulia kwanza, mzee wangu kamfuata rafiki yake kumuomba bintie awe mbadala ili mipango ya harusi iendelee. Mzee kakubali. Binti huyo licha ya kuwa ni namzidi kama miaka kumi na kitu, sikuwahi hata kumtania kwa lolote.

Kwa sasa binti yuko chuo. Jukumu la kuhakikisha binti anakubali kaachiwa mzee wake. Mara kwa mara najiuliza misingi ya hii ndoa tarajiwa itakuwa nini? Upendo au bahati mbaya?

Updates!
Nimefunga safari kumfuata binti chuoni. Nilivyomuona anaonesha dalili zote za ujauzito. Niliplan ku-extend mazungumzo, ila nimekosa stimu kabisa. Nafikiri hii ni game over.
 
Jamaa linataka kulia kwa second time inasubiri mkweo akutongozee bint yake?
Huyo wa kwanza hakukosea kutoka nduki nina wasiwasi kaka yako au baba yako alikuwa anakutongozea! Stage ya kutongoza na kudate ni yako wazee wanaidhinisha tu kitu ulishakiweka sawa!utapigiwa sana wewe natamani uwe jirani yangu mtu wewe!
 
What a coincidence? Binafsi usiku wa leo nimeota nimemkimbia bwana harusi ambaye sikumpenda siku ya harusi.

BTW epuka sana kumuoa binti ambaye unajua kabisa hana mapenzi nawe,utajuta.
Tena binti mwenyewe yuko chuo? Bora angekuwa wa kijijini huko.
 
Hii nzuri sana...mhimu wote muafiki na mpate muda wa kudate kidogo. Mina rafiki yangu mhindi jamaa anajiandaa kuoa May 18, kila kitu kinafanywa na baba yake. Mzee kamtafuta binti anayeendana na mshikaji kulingana na professional, tabia zake, uwezo wa familia anayotoka binti, na mambo mengi. Kabla ya hapo alishatafutiwa mabinti kama 3 wote hawakuendana ingawa yeye alikuwa anawapenda ila Mzee alimtolea nje. Kwa kifupi, Mkuu una bahati na lazima uimwagilie hiyo ndoa mambo yataenda vizuri tu wala usiwe na wasiwasi.
 
Hii kitu ishawahi kutokea kwa bro wngu kabisa. Wiki mbili kabla ya harusi aligundua kuwa mke ni mjamzito, na yy hahusiki maana hakuwahi kupiga nyama..
Ikabidi wareplace na binti mwingine..
Bro alioa na wanaishi kwa amani sana kwa kuheshimiana 10 years now..
 
What a coincidence? Binafsi usiku wa leo nimeota nimemkimbia bwana harusi ambaye sikumpenda siku ya harusi.

BTW epuka sana kumuoa binti ambaye unajua kabisa hana mapenzi nawe,utajuta.
Tena binti mwenyewe yuko chuo? Bora angekuwa wa kijijini huko.
halafu na Mimi nimeota namkimbiza bibi harusi aliyenikimbia Siku ya ndoa kisa hanipendi dah nafikili utakuwa ndio wewe uliyekuwa unatakiwa kuwa my wife to be but all in all ndoa njema kati yako na uliyemkimbilia à.k.à t.h.e. b.o.l.d
 
What a coincidence? Binafsi usiku wa leo nimeota nimemkimbia bwana harusi ambaye sikumpenda siku ya harusi.

BTW epuka sana kumuoa binti ambaye unajua kabisa hana mapenzi nawe,utajuta.
Tena binti mwenyewe yuko chuo? Bora angekuwa wa kijijini huko.
Mara nyingi Binti haolewi na anayempenda Bali anayeweza kumtunza na kumhudumia kikamilifu! Matunzo na HUDUMA mwananana huchipusha upendo kwa mwanamke taratibu lakini kwa uhakika na mwisho humpenda sana!
Kinyume chake upendo wa mwanamke kwa mume asiye na uwezo wa kumtimizia mahitaji yake huchuja taratibu lakini kwa uhakika na mwisho huwa adui yake!
 
Uko sahihi kabisa mkuu,
Watu wengi hawafahamu jambo hili,
Ndoa ni taasisi nyingine kabisa
Mfano mimi nilikuwa na wapenzi kadhaa ambao kwa wakati ule wa ujana niliamini Ndio ningeowa,
Muda wa kuowa ulipotimia sijui kilichotokea mpaka leo sifahamu ilikuwaje, nilikwenda kijijini kuowa mpaka leo niko na mama chanja wangu na watoto wetu 3 Maisha murua,
Jambo 1 tu nililofanya kabla sijamuowa niliketi nae na kujadili mambo muhimu ya Maisha yetu ya baadae
 
Mkuu huwezi jua yawezekana ndio chaguo Mungu alokupangia, na hadi kufikia mzazi wako kwenda kuomba binti wa rafiki yake yawezekana aliguswa na roho wa Mungu.
 
Kumbe mtu mwenyewe hadi utongozewe, yaani unajisifu kumkabidhi mkweo kazi ya kukutongozea??? Yuko sawa aliyekukimbia
 
Jamaa linataka kulia kwa second time inasubiri mkweo akutongozee bint yake?
Huyo wa kwanza hakukosea kutoka nduki nina wasiwasi kaka yako au baba yako alikuwa anakutongozea! Stage ya kutongoza na kudate ni yako wazee wanaidhinisha tu kitu ulishakiweka sawa!utapigiwa sana wewe natamani uwe jirani yangu mtu wewe!
Hahahaha!! unatamani awe jirani yako ili?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom